Maoni yetu Maamuzi ya Serikali Kuhusu Zao la Korosho - Zitto Kabwe

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Maoni yetu Maamuzi ya Serikali Kuhusu Zao la Korosho

Mtakumbuka Oktoba 28 tulipofanya mkutano na Wanahabari juu ya suala la Korosho na tulipendekeza kuwa,
“Serikali inunue Korosho yote kwa wakulima ili kuwalinda na bei ndogo kutokana na kushuka kwa bei ya korosho kwenye soko la dunia. Kwa vile malengo ya serikali hayatakuwa kupata faida bali kufidia gharama za manunuzi, bei ya korosho haitashuka sana. Kisha Serikali iwauzie wanunuzi kwa namna wanaona inafaa. Lengo hapa ni kumlinda Mkulima kwa kumpa bei nzuri”.

Chama cha ACT Wazalendo tunakaribisha uamuzi wa Serikali kununua kwa bei nzuri korosho zote za Wakulima wa Korosho kama tulivyopendekeza, pamoja na hayo tuna yafuatayo ya kueleza:

1. UZALISHAJI KUPUNGUA: Ni muhimu umma ujue kuwa Uzalishaji wa Korosho kwa msimu wa 2018 unatarajiwa kushuka kwa 43%, kutoka uzalishaji wa tani 350,000 wa mwaka 2017 mpaka uzalishaji wa tani 200,000 unaotarajiwa kwa mwaka huu. Kushuka kwa uzalishaji huu kuna mahusiano makubwa na hatua ya Serikali kupora fedha za wakulima wa korosho zitokanazo na Export Levy (jambo ambalo tulilipinga wakati wa Bunge la Bajeti). Licha ya Serikali kutoa sababu ya Hali ya hewa kama sababu ya uzalishaji kupungua, sababu kubwa ni Wakulima kukosa pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu.

2. ATHARI ZA KIMAPATO: Hatua ya Kuzinunua Korosho ni hatua sahihi ili kunusuru wakulima. Lakini ni muhimu kueleza kuwa kwa mwaka huu tutakosa Mapato ya Fedha za Kigeni ambazo ni muhimu Katika kutunza thamani ya sarafu yetu. Pia wapo Watanzania wengi watakaoathirika kutokana na kutokuwepo kwa mnyororo wa korosho (Value Chain) kuanzia wenye magari ya usafirishaji, wamiliki wa nyumba za wageni, wenye mikahawa, makuli, mawakala wa meli pamoja na wamiliki wa maghala. Watu wote hawa ni walipa Kodi, hivyo Serikali itakosa mapato. Pia Serikali itakosa mapato ya kodi ya Export Levy pamoja na mapato ya Kodi ya Halmashauri za miji inayolima korosho. Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba itaathirika zaidi kwani ilitarajiwa kupata shs 5 bilioni mwaka huu. Hii itaathiri sana mikopo kwa Vijana na Wanawake ambao hupata 10% ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa.

3. TADB HAINA FEDHA: Maagizo ya kuwa Benki ya Kilimo Nchini (TADB) ndio wanapaswa kununua Korosho yameleta mashaka kidogo kwetu. Uwezo wa mtaji wa kifedha wa TADB ni shilingi 200 bilioni tu, zinazoweza kununua 30% tu ya korosho zinazotarajiwa kuvunwa, ili kununua Korosho zote, tani 200,000 wanahitaji shilingi 660 bilioni. Serikali inataka kuwakopa wakulima wa Korosho? Tunatoa tahadhari kuwa iwapo Serikali itawapa Fedha TADB kwa shughuli hii lazima ifuate Sheria. Tuna mashaka kuwa Benki Kuu itatoa Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo kwenye akaunti zake na kuwapa TADB. Jambo hili likifanyika bila kufuata sheria itakuwa ni wizi kama wizi mwengine wowote. Tutaendelea kufuatilia kwa kina suala hili ili kuhakikisha Serikali haitumii fedha za umma hovyo ili kufunika makosa yake yenyewe.

4. Magari ya Jeshi yatahitaji mafuta, wanajeshi wetu nao watahitaji kulipwa posho za kujikimu wakati wote ambao watakuwa wanatimiza wajibu huu, lakini pia maamuzi ya uendelezaji wa Kiwanda kilichotaifishwa cha Ubanguaji wa Korosho cha BUKO kilichoko Lindi ni mambo yanayohitaji fedha. Bunge halikupitisha Bajeti ya yote haya, ni imani yetu kuwa Serikali itafuata Katiba kwa kuleta Bungeni nyongeza ya Bajeti ili kuruhusu matumizi haya.

HITIMISHO:

ACT Wazalendo tunawapongeza wote walioshirikiana nasi kuhakikisha tunaisimamia Serikali ili itimize wajibu wake wa kulinda Ustawi wa Wakulima wetu, kuanzia Wakulima wenyewe, Vyama vya Upinzani, Wabunge wote kutoka mikoa inayolima Korosho, Vyama vya Ushirika vya Wakulima wa Korosho, pamoja na Asasi za Kijamii kama Mviwata na Ansaf. Ni muhimu sana kuendeleza ushirkiano wetu ili kuibana Serikali ifuate Sheria ya Matumizi ya Fedha za Umma kwenye ununuzi huu wa korosho za Wakulima wetu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Novemba 12, 2018
 
Safi kabisa rais wa mioyo ya watu
 
Mbona hueleweki wewe Zitto Kabwe uko upande gani? Mwanzo uliponda sana Rais kuingilia hili swala la korosho, lakini usilolitegemea leo limetokea (serikali kuazimia rasmi kununua korosho yote kwa bei yenye tija kwa mkulima). Sasa tena hapa unadandia treni nyingine, oh sijui fedha hazipo blah, blah, blah. Acha kutaga mayai hovyo!

Nguvu anayotumia Zitto kupigania Korosho angeitumia kupigania Mawese ya kule kwao Kigoma ingekuwa Poa Sana

Rais kakosea kujiingiza kwenye Biashara Kama alivyokosea Zitto Na ACT yake kushauri hivyo

The best approach ni kuacha price mechanism i take place then Govt ku compasate Kwa njia ya subsidies sio kununua

Leo Hii Korosho zote zitanunuliwa Kwa fixed price regardless ya madaraja yao lakin sokoni haziuzwi hivyo
 
Achilia mbali issue ya fedha za TADB, ni wapi kwingine duniani serikali imewahi fanya biashara na ikapata faida?
Mkuu fanyeni mnavofanya lakini serikali kuanza kuingiza mkono wake moja Kwa moja ni threat Kwa other important players kwenye uchumi.. I know you know this...
Mara zote tunasema serikali ni incompetent kufanya biashara, so inatakiwa iwe regulator au iwasaidie wajasiriamali kuweza kufanya biashara ili wailipe Kodi.....
Majanga ni pale utakapoona kifo cha TADB na ka escrow kengine kadogo kanajitokeza.....

Macho yetu na masikio yapo Mtwara na Lindi Kwa sasa...till next time tuone sustainability ya serikali kwenye hili ikoje...
 
Maoni yetu Maamuzi ya Serikali Kuhusu Zao la Korosho

Mtakumbuka Oktoba 28 tulipofanya mkutano na Wanahabari juu ya suala la Korosho na tulipendekeza kuwa,
“Serikali inunue Korosho yote kwa wakulima ili kuwalinda na bei ndogo kutokana na kushuka kwa bei ya korosho kwenye soko la dunia. Kwa vile malengo ya serikali hayatakuwa kupata faida bali kufidia gharama za manunuzi, bei ya korosho haitashuka sana. Kisha Serikali iwauzie wanunuzi kwa namna wanaona inafaa. Lengo hapa ni kumlinda Mkulima kwa kumpa bei nzuri”.

Chama cha ACT Wazalendo tunakaribisha uamuzi wa Serikali kununua kwa bei nzuri korosho zote za Wakulima wa Korosho kama tulivyopendekeza, pamoja na hayo tuna yafuatayo ya kueleza:

1. UZALISHAJI KUPUNGUA: Ni muhimu umma ujue kuwa Uzalishaji wa Korosho kwa msimu wa 2018 unatarajiwa kushuka kwa 43%, kutoka uzalishaji wa tani 350,000 wa mwaka 2017 mpaka uzalishaji wa tani 200,000 unaotarajiwa kwa mwaka huu. Kushuka kwa uzalishaji huu kuna mahusiano makubwa na hatua ya Serikali kupora fedha za wakulima wa korosho zitokanazo na Export Levy (jambo ambalo tulilipinga wakati wa Bunge la Bajeti). Licha ya Serikali kutoa sababu ya Hali ya hewa kama sababu ya uzalishaji kupungua, sababu kubwa ni Wakulima kukosa pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu.

2. ATHARI ZA KIMAPATO: Hatua ya Kuzinunua Korosho ni hatua sahihi ili kunusuru wakulima. Lakini ni muhimu kueleza kuwa kwa mwaka huu tutakosa Mapato ya Fedha za Kigeni ambazo ni muhimu Katika kutunza thamani ya sarafu yetu. Pia wapo Watanzania wengi watakaoathirika kutokana na kutokuwepo kwa mnyororo wa korosho (Value Chain) kuanzia wenye magari ya usafirishaji, wamiliki wa nyumba za wageni, wenye mikahawa, makuli, mawakala wa meli pamoja na wamiliki wa maghala. Watu wote hawa ni walipa Kodi, hivyo Serikali itakosa mapato. Pia Serikali itakosa mapato ya kodi ya Export Levy pamoja na mapato ya Kodi ya Halmashauri za miji inayolima korosho. Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba itaathirika zaidi kwani ilitarajiwa kupata shs 5 bilioni mwaka huu. Hii itaathiri sana mikopo kwa Vijana na Wanawake ambao hupata 10% ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa.

3. TADB HAINA FEDHA: Maagizo ya kuwa Benki ya Kilimo Nchini (TADB) ndio wanapaswa kununua Korosho yameleta mashaka kidogo kwetu. Uwezo wa mtaji wa kifedha wa TADB ni shilingi 200 bilioni tu, zinazoweza kununua 30% tu ya korosho zinazotarajiwa kuvunwa, ili kununua Korosho zote, tani 200,000 wanahitaji shilingi 660 bilioni. Serikali inataka kuwakopa wakulima wa Korosho? Tunatoa tahadhari kuwa iwapo Serikali itawapa Fedha TADB kwa shughuli hii lazima ifuate Sheria. Tuna mashaka kuwa Benki Kuu itatoa Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo kwenye akaunti zake na kuwapa TADB. Jambo hili likifanyika bila kufuata sheria itakuwa ni wizi kama wizi mwengine wowote. Tutaendelea kufuatilia kwa kina suala hili ili kuhakikisha Serikali haitumii fedha za umma hovyo ili kufunika makosa yake yenyewe.

4. Magari ya Jeshi yatahitaji mafuta, wanajeshi wetu nao watahitaji kulipwa posho za kujikimu wakati wote ambao watakuwa wanatimiza wajibu huu, lakini pia maamuzi ya uendelezaji wa Kiwanda kilichotaifishwa cha Ubanguaji wa Korosho cha BUKO kilichoko Lindi ni mambo yanayohitaji fedha. Bunge halikupitisha Bajeti ya yote haya, ni imani yetu kuwa Serikali itafuata Katiba kwa kuleta Bungeni nyongeza ya Bajeti ili kuruhusu matumizi haya.

HITIMISHO:

ACT Wazalendo tunawapongeza wote walioshirikiana nasi kuhakikisha tunaisimamia Serikali ili itimize wajibu wake wa kulinda Ustawi wa Wakulima wetu, kuanzia Wakulima wenyewe, Vyama vya Upinzani, Wabunge wote kutoka mikoa inayolima Korosho, Vyama vya Ushirika vya Wakulima wa Korosho, pamoja na Asasi za Kijamii kama Mviwata na Ansaf. Ni muhimu sana kuendeleza ushirkiano wetu ili kuibana Serikali ifuate Sheria ya Matumizi ya Fedha za Umma kwenye ununuzi huu wa korosho za Wakulima wetu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Novemba 12, 2018
Mkuu Zitto Hizi akili hazipo CCM wala Chato...ungekubali nawe kuunga juhudi Mhutu angekuhonga Bandari zote kama si Migodi yote!
 
Mbona hueleweki wewe Zitto Kabwe uko upande gani? Mwanzo uliponda sana Rais kuingilia hili swala la korosho, lakini usilolitegemea leo limetokea (serikali kuazimia rasmi kununua korosho yote kwa bei yenye tija kwa mkulima). Sasa tena hapa unadandia treni nyingine, oh sijui fedha hazipo blah, blah, blah. Acha kutaga mayai hovyo!
dinasour.jpg

Bora hata lingetaga mayai ya dinasoour tukajua limnyama linatisha!
 
Zitto nakushauri nenda kalee familia yako na mkeo. Maisha ya siasa yamekushinda.

Vipi kuhusi lile ghorofa lako pale Dodoma karibia Martin Lutha, hujui umelijenga barabarani!?
Halafu wewe Zitto, umeshindwa kufanya planning ya mambo yako binafsi utaweza kweli hizi issue kubwa kubwa!?

Ghorofa lako la pale Dodoma ni la kishamba kweli. Eti unajiita mchumi!! Wenzio wanatumia technology mpya kujenga majengo. Wanatumia vioo nasiyo hilo lako unajenga matofari kuanzia chini mpaka juu tena kandokando ya barabara. Mchumi gani wewe umeshindwa kufanya planning mambo yako binafsi!!?

Kwenye jimbo lako hushughuliki na kero za waha unachumia tumbo lako tu. Hivi unadhani sisi wananchi ni wajinga!? Vitu unavyovifanya havitakusaidia.
 
Maoni yetu Maamuzi ya Serikali Kuhusu Zao la Korosho

Mtakumbuka Oktoba 28 tulipofanya mkutano na Wanahabari juu ya suala la Korosho na tulipendekeza kuwa,
“Serikali inunue Korosho yote kwa wakulima ili kuwalinda na bei ndogo kutokana na kushuka kwa bei ya korosho kwenye soko la dunia. Kwa vile malengo ya serikali hayatakuwa kupata faida bali kufidia gharama za manunuzi, bei ya korosho haitashuka sana. Kisha Serikali iwauzie wanunuzi kwa namna wanaona inafaa. Lengo hapa ni kumlinda Mkulima kwa kumpa bei nzuri”.

Chama cha ACT Wazalendo tunakaribisha uamuzi wa Serikali kununua kwa bei nzuri korosho zote za Wakulima wa Korosho kama tulivyopendekeza, pamoja na hayo tuna yafuatayo ya kueleza:

1. UZALISHAJI KUPUNGUA: Ni muhimu umma ujue kuwa Uzalishaji wa Korosho kwa msimu wa 2018 unatarajiwa kushuka kwa 43%, kutoka uzalishaji wa tani 350,000 wa mwaka 2017 mpaka uzalishaji wa tani 200,000 unaotarajiwa kwa mwaka huu. Kushuka kwa uzalishaji huu kuna mahusiano makubwa na hatua ya Serikali kupora fedha za wakulima wa korosho zitokanazo na Export Levy (jambo ambalo tulilipinga wakati wa Bunge la Bajeti). Licha ya Serikali kutoa sababu ya Hali ya hewa kama sababu ya uzalishaji kupungua, sababu kubwa ni Wakulima kukosa pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu.

2. ATHARI ZA KIMAPATO: Hatua ya Kuzinunua Korosho ni hatua sahihi ili kunusuru wakulima. Lakini ni muhimu kueleza kuwa kwa mwaka huu tutakosa Mapato ya Fedha za Kigeni ambazo ni muhimu Katika kutunza thamani ya sarafu yetu. Pia wapo Watanzania wengi watakaoathirika kutokana na kutokuwepo kwa mnyororo wa korosho (Value Chain) kuanzia wenye magari ya usafirishaji, wamiliki wa nyumba za wageni, wenye mikahawa, makuli, mawakala wa meli pamoja na wamiliki wa maghala. Watu wote hawa ni walipa Kodi, hivyo Serikali itakosa mapato. Pia Serikali itakosa mapato ya kodi ya Export Levy pamoja na mapato ya Kodi ya Halmashauri za miji inayolima korosho. Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba itaathirika zaidi kwani ilitarajiwa kupata shs 5 bilioni mwaka huu. Hii itaathiri sana mikopo kwa Vijana na Wanawake ambao hupata 10% ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa.

3. TADB HAINA FEDHA: Maagizo ya kuwa Benki ya Kilimo Nchini (TADB) ndio wanapaswa kununua Korosho yameleta mashaka kidogo kwetu. Uwezo wa mtaji wa kifedha wa TADB ni shilingi 200 bilioni tu, zinazoweza kununua 30% tu ya korosho zinazotarajiwa kuvunwa, ili kununua Korosho zote, tani 200,000 wanahitaji shilingi 660 bilioni. Serikali inataka kuwakopa wakulima wa Korosho? Tunatoa tahadhari kuwa iwapo Serikali itawapa Fedha TADB kwa shughuli hii lazima ifuate Sheria. Tuna mashaka kuwa Benki Kuu itatoa Fedha za Mashirika ya Umma zilizopo kwenye akaunti zake na kuwapa TADB. Jambo hili likifanyika bila kufuata sheria itakuwa ni wizi kama wizi mwengine wowote. Tutaendelea kufuatilia kwa kina suala hili ili kuhakikisha Serikali haitumii fedha za umma hovyo ili kufunika makosa yake yenyewe.

4. Magari ya Jeshi yatahitaji mafuta, wanajeshi wetu nao watahitaji kulipwa posho za kujikimu wakati wote ambao watakuwa wanatimiza wajibu huu, lakini pia maamuzi ya uendelezaji wa Kiwanda kilichotaifishwa cha Ubanguaji wa Korosho cha BUKO kilichoko Lindi ni mambo yanayohitaji fedha. Bunge halikupitisha Bajeti ya yote haya, ni imani yetu kuwa Serikali itafuata Katiba kwa kuleta Bungeni nyongeza ya Bajeti ili kuruhusu matumizi haya.

HITIMISHO:

ACT Wazalendo tunawapongeza wote walioshirikiana nasi kuhakikisha tunaisimamia Serikali ili itimize wajibu wake wa kulinda Ustawi wa Wakulima wetu, kuanzia Wakulima wenyewe, Vyama vya Upinzani, Wabunge wote kutoka mikoa inayolima Korosho, Vyama vya Ushirika vya Wakulima wa Korosho, pamoja na Asasi za Kijamii kama Mviwata na Ansaf. Ni muhimu sana kuendeleza ushirkiano wetu ili kuibana Serikali ifuate Sheria ya Matumizi ya Fedha za Umma kwenye ununuzi huu wa korosho za Wakulima wetu.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
Novemba 12, 2018
Tunasubiri na tamko la Mbowe wa Ufipa!
 
Zitto nakushauri nenda kalee familia yako na mkeo. Maisha ya siasa yamekushinda.

Vipi kuhusi lile ghorofa lako pale Dodoma karibia Martin Lutha, hujui umelijenga barabarani!?
Halafu wewe Zitto, umeshindwa kufanya planning ya mambo yako binafsi utaweza kweli hizi issue kubwa kubwa!?

Ghorofa lako la pale Dodoma ni la kishamba kweli. Eti unajiita mchumi!! Wenzio wanatumia technology mpya kujenga majengo. Wanatumia vioo nasiyo hilo lako unajenga matofari kuanzia chini mpaka juu tena kandokando ya barabara. Mchumi gani wewe umeshindwa kufanya planning mambo yako binafsi!!?

Kwenye jimbo lako hushughuliki na kero za waha unachumia tumbo lako tu. Hivi unadhani sisi wananchi ni wajinga!? Vitu unavyovifanya havitakusaidia.
Kilaza kweli wewe! Hata kwenye makinikia ilikuwa hivi hivi ila sasa kimya.
 
Back
Top Bottom