Ni chakula gani hupendi, mimi sipendi ndizi za kupika

ndizi gani? za bukoba au za mbeya au za kilimanjaro?
na za kupika na maharage au nyama au zipi unasemea maana ndizi zipo aina nyingi na mapishi tofauti tofauti kama viazi
Ndizi zozote zile ili mradi ziwe za kupika hata mpishi azipike akiwa uchi sizipendi, ziwe za nyama au maharage sijui utumbo nk nk sizipendi.
 
Makande aisee.wakati nipo boarding school (mkoa wa kilimanjaro) kila siku mchana na jioni tunakula makande sio kama yale niliyozoea kwetu Tanga coz mahindi mazima mazima na maharage daah.

Kabla ya mwaka kuisha nilihama sababu ya maswala ya academics na hali ya baridi lakini mpk sasa sina hamu tena ya makande miaka 10 imepita nilishakinai kila nilivyojaribu kula makande nimeshindwa.
 
kuna makande yanapikwa kama pilau achana na hayo maharage yaani ukipikiwa na wataalam kama sisi utahamia.
ujue hakuna chakula kibaya sema ni mapishi na ulle mpangilio wa kula .chakula chochote ukila kila siku unakinai .chakula kilekile mapishi yale yale ndo tatizo la waafrica
 
Back
Top Bottom