Sipendi ugali kabisa na ninaishi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,908
Katika vyakula ambavyo huwa sivishobokei ni Ugali mimi siupendi kabisa yaani sina stim nao kabisa.

Sazingine huwa nakula tu ndo wife au beki3 kaandaa lakini kiukweli ugali sio chakula nachokipa thamani japo familia yangu mke na watoto wanaupenda balaa.

Ni mara kibao nikirudi nyumbani nikikuta wamepika ugali nitapitiliza tu chumbani kulala au nitaomba wanitafutie mbadala.

Na mara nyingi wakiwa wanaandaa huwa wanajua kabisa kwahiyo mbadala lazima iwepo.

Sazingine huwa nakula tu ili siku ipite lakini ni chakula cha hovyo kabisa, mimi naweza kukaa hata mwaka nisile ugali na nikaona fresh kabisa.

Ni kawaida kwangu siku hizi kukaa wiki au wiki mbili bila kuutia ugali mdomoni.

Kuna kitu huwa kinanishangaza sana, kuna watu wanakula ugali mchana na usiku tena siku 7 za wiki duuuh tena ugali na yale madagaa ya ziwa victoria!! Sio kwa nia mbaya au nina ego hapana mimi ugali hapana bora nile ndizi mwezi nzima lakini sio ugali.
 
Hata hivyo Ugali umedumaza sana Ubongo za watu wengi na jinsi ulivyo wengi wanaamini ni chakula ya Mtu mweusi kumbe nayo ilililetwa na Mabeberu zipo Nchi nyingi Afrika Ugali sio kipaumbele chao kama hapa kwetu...
Halafu huwa nawaambia watu hili jambo wanashindwa kuamini, ugali uliletwa na mabeberu na mahindi yaliletwa na wareno kama sikosei, hata kama ugali ulikua ukiliwa Africa sidhani kama ni huu ugali wa dona

Mtaalam ambao watu weusi wengi wanaomuamini kama mzalendo Dr sebi alishawahi kusema ugali wa dona ni sumu na unadumaza akili
 
Madogo hamjui historia ya wabantu...kabla ya mahindi babu zetu walikua wanakula ugali wa nafaka mbalimbali...Tatizo madogo ujuaji mwingi na elimu zenu za degree.
 
Aah! basi watu tunatofautiana sana

Kiukweli Mimi nisipokuta ugali(nguna) nyumbani siwaelewi kbs, wapike vyakula vyao wanavyotaka lkn ugali wa baba huo lzm uwepo.

Ugali dagaa, ugali samaki, ugali nyama choma hapo hunitoi mzee. Nakula hata mwaka mzima bila kubadili na sioni noma yoyote.
 
Sasa wewe ndio mbantu alisia.
 
Back
Top Bottom