JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza anuai mpya ya COVID-19 iitwayo EG.5 - iliyopewa jina lisilo rasmi "Eris" huku likishauri kila nchi kuchukua hatua mahsusi za kufuatilia uwepo wake. Lakini shirika hilo linasema inaleta hatari ndogo kwa afya ya umma, bila ushahidi kwamba husababisha ugonjwa mbaya zaidi kuliko lahaja zingine zinazozunguka kwa sasa.
Kizza Besigye na Yoweri Museveni walikuwa marafiki walioshibana wakati wa Vita ya Msituni Uganda kumuondoa Milton Obote miaka ya 1980, na Dkt. Besigye aliwahi kuwa daktari binafsi wa Museveni na wanajeshi wengine waliokuwa msituni pamoja na Museveni Rais Museveni na Winnie Byanyima walikuwa wachumba kati ya 1981 na 1986, Bi Byanyima alikuwa pamoja na Museveni alipoingia Kampala akiwa mkuu wa jeshi la waasi mwaka 1986. Lakini Museveni hakuwa tayari kumuacha mkewe, Janet, na Bi Byanyima akafukuzwa. Hatimaye aliolewa na Dkt. Besigye 1998. Inadaiwa kitendo kile kilimuuma sana Rais Museveni, kwanza akataifisha ranchi ya babake Winnie Byanyima, Mzee Boniface Byanyima. Pia matukio hayo ya ngono na usaliti yalijenga uadui mkubwa kati ya...
Kuna maeneo fulani nimepita ya mkoa wa dodoma wilayani huko; nimekuta kuna msururu mrefu sana wa vyombo vya moto kwenye moja ya petrol station. Nikajaribu kuuliza kuna shida gani hapa? Wenyeji wanasema mafuta ya petrol hamna kabisa wilayani hapo. Baadhi ya vituo vya mafuta vimesitisha huduma. Pia majuzi nilisikia kuna sehemu hapa tz pia kuna shida ya mafuta.
Habari ndio hiyo wakuu, Mpaka Tanganyika inapata uhuru wake mwaka 1961, ni wananchi wawili tu walikuwa wamesoma kwa kiwango cha shahada ya kwanza(Degree). Wa kwanza alikuwa ni Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa ni Rais wa kwanza na baba wa Taifa. Mwalimu Nyerere alikuwa na Degree ya Uchumi, akachanganya sheria na mambo mengine. Mtu wa pili alikuwa mzee mmoja wa Kisambaa, jina limenitoka. Huyu mzee alikuwa na shahada ya kwanza ya Uhandisi(engineering). Asante sana
Miongoni mwa Wabunge wa Tanzania waliobahatika kuteuliwa kufanya ziara ya siri huko Dubai, yumo mbunge wa Jimbo la Msalala la Mkoani Shinyanga. Taarifa zinaonesha kwamba Mbunge huyu alivyorudi tu yeye hakutaka kununua gari la kuandika jina lake kama alivyofanya Musukuma, bali yeye ameamua kugawa nyama ya ng'ombe kila kijiji, ambako kijiji kimoja kimeambulia ng'ombe kubwa mbili. Ikumbukwe kwamba Jimbo la Msalala lina kata 18, ambapo kila kata ina vijiji 6, unadhani wabunge walioenda kule walilipwa bei gani kila mmoja na kwanini walipwe vitita vyote hivyo? Toa Maoni yako.
Licha ya kuwa Mazoezi husaidia kujenga na kulinda Afya, kuna masuala muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanza mazoezi ikiwemo kuchagua eneo la kufanyia mazoezi ambalo litakuwa salama kimiundombinu na kimazingira. Katika siku za hivi karibuni watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi katika maeneo ya jirani au pembezoni mwa Barabara zinazotumiwa na Vyombo vya Moto (Magari, Pikipiki Bajaj na Mitambo mbalimbali) hali inayodaiwa kuwa watu hao huvuta hewa chafu. Je kuna ukweli wowote hapo?
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazohusisha taasisi na watu maarufu duniani kuwa na mpango wa kupunguza idadi ya watu duniani. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na Bill Gates kuelezwa kuandika katika mitandao wa kijamii akimshauri kiongozi wa World Economic Forums (WEF), Klaus Schwab juu ya matumizi ya "death panels" kupunguza watu duniani. Lakini pia, video nyingine ambayo imesambaa mtandaoni inamuonesha Mtendaji Mkuu wa Pfizer, Albert Bourla, akidaiwa kusema wanatazamia kufanikisha kupunguza idadi ya watu duniani kwa 50%. Je, taarifa hizi zina ukweli?
Hoja ya Serikali ya Tanzania kufanya Makubaliano ya awali na kampuni ya DP World ya Dubai kwenye kuendeleza bandari ya Dar Es Salaam imezua mambo mengi yanayojadiliwa sana. Mojawapo ya Mambo hayo ni kuhusisha Bandari kuwa miongoni mwa masuala ya Muungano. Baadhi ya watu wamekuwa wanadai kuwa Bandari ni Suala la Muungano huku wengine wakipinga. Ukweli upoje?
Rais Mstaafu Joseph Kabila inasemekana hakuwa mtoto halisi(Biological Son) wa Rais Mstaafu Joseph Desire Kabila. Inasemekana jina halisi la Joseph Kabila ni Hypolite Kanambe Kazemberembe akiwa na asili ya Kitusi kutoka nchi ya Rwanda. Pamoja na machapisho mengi kumtambua Joseph Kabila kama mtoto halisi (Biological son) wa Hayati Joseph Desire Kabila, baadhi ya machapisho yamehabarisha kuwa baba mzazi wa Joseph Kabila Kabange anajulikana kama Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje. Maswali ambayo wakongo wengi wanajiuliza, ilikuwaje wakatawaliwa na Rais aliyezaliwa Rwanda na mwenye asili ya Kitusi kutoka Rwanda huku Moise Katumbi aliyezaliwa Congo DR na Mama Mkongo na Baba Mgiriki akiwekewa...
Wiki mbili zilizopita kwenye mitandao mbalimbali ilionekana mwendesha bodaboda asiye na woga akiwaacha wengi katika mshangao baada ya kupita kwa utulivu katikati ya kundi simba wenye njaa wanaokula mnyama waliyemuua. Inasemekana baada ya kuwapita Simba, pikipiki yake ilipata hitilafu ambapo alishindwa kuendelea na safari ndipo Simba waliweza kumshambulia na kujipatia kitoweo. Picha ya mwisho iliyobandikwa ilionyesha simba wakiwa wamekaa pembeni ya pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba na ndizi, lakini mtu huyo hakupatikana, jambo ambalo liliwashangaza wengi na kuamini kuwa ameliwa na simba hao. VIDEO: Simba wakizunguka pikipiki huku dereva akiwa haonekani. Katika Mtandao wa Twitter, mtumiaji mmoja maarufu kama Mwaisa MtuMbad...
Jamani kichwa kinajieleza. Kwanza ni kweli mende anazalisha maziwa? Mende hawa hawa tunaowaona chooni? Sasa maziwa yenye yanakaa wapi na wanakamuaje? Halafu eti inasemekana maziwa ya mende yanavirutubisho kuliko ya ng'ombe, si makubwa haya! Mende walivyo wachafu na wanavyoogopesha leo mtu ukanywe sijui ule maziwa yake, yaani sitaki hata kupata picha kwakweli. Wakuu hili ni kweli?
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…