JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kama ilivyozoeleka kwenye jamii nyingi kuwa ukiwa Rastafarian basi kwa asilimia kubwa utakuwa unatumia bangi/marijuana na majina mengine lukuki kama inavyojulikana. Leo kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa kuna meme inasambaa ikiwa na ujumbe "Wakati Lucky Dube anaimba "Born to Suffer" me nilidhani ni sababu anavuta bangi" Meme hii ikanikumbusha article niliyowahi kusoma kuwa Lucky Dube alijiepusha na matumizi ya bangi, pombe na sigara ili kuwa mfano mzuri kwenye jamii.
Baada ya kauli ya CDF wa Tanzania Jenerali Mkunda kusema kuwa 'Baadhi ya Wakimbizi wamepewa teuzi Serikalini katika nafasi zenye maamuzi' imenifikirisha sana nikakumbuka nilishawahi kusikia tetesi kuwa Paul Kagame wakati akiwa mkimbizi nchini Uganda, aliwahi kuhudumu kwenye jeshi la nchi hiyo na mpaka kufikia cheo cha Mkuu wa usalama wa Jeshi Uganda. Mpaka sasa tunaona jinsi Kagame anavyoisumbua Uganda labda kutokana na ukweli kuwa anaijua nje ndani. Je, ni kweli Paul Kagame aliweza kuaminiwa na kupewa cheo nyeti kwenye Jeshi la Uganda?
𝐋𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐉𝐈𝐓𝐎𝐒𝐀 𝐊𝐔𝐆𝐎𝐌𝐁𝐄𝐀 𝐔𝐁𝐔𝐍𝐆𝐄 , 𝐀𝐏𝐈𝐍𝐆𝐀 𝐀𝐉𝐄𝐍𝐃𝐀 𝐘𝐀 "𝐍𝐎 𝐑𝐄𝐅𝐎𝐑𝐌𝐒, 𝐍𝐎 𝐄𝐋𝐄𝐂𝐓𝐈𝐎𝐍" Kupitia ukurasa wake wa Twitter (X), Godbless Lema ametangaza kuwa ameungana na wanachama wengi wa CHADEMA wanaopinga ajenda ya No Reforms, No Election. Lema ameweka wazi msimamo wake wa kushiriki kwenye uchaguzi akisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kupigania mabadiliko ndani ya mfumo wa kisiasa kupitia ushiriki wa moja kwa moja kwenye uchaguzi. Aidha, amethibitisha kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha Mjini.
Huku kwetu kila kukicha deni linazidi kupaa na maisha kuzidi kuwa magumu. Na hapo tunajinasibu kuwa na amani na utulivu. Burkina Faso mbali ya kuwa katika machafuko kwa muda mrefu, kwa miaka 2 tu Traore kaweza kulipa deni la taifa la Dola Bil. 4. Halafu Tanzania Wasira anajisifu kuwa deni ni la enzi na enzi huku Bi. Mkubwa akijisifia kupokea 'vijisenti' vya mkopo ambavyo hata la maana hatulioni zaidi ya anasa za Mama hiki na Mama kile. Millard Ayo hawezi kuripoti habari kama hii. Media za bongo kazi ni kusifia upumbavu tu.
Magonjwa mbalimbali yametufanya binadamu kubuni tiba aina mbalimbali ambazo zitatusaidia kuondokana na magonjwa hayo. Moja ya tiba iliyobuniwa na binadamu ni pamoja na mkoja wa binadamu kama tiba ya magonjwa mbalimbali. Tena unaambiwa ukipata mkojo wa asubuhi ndio kiboko ya magonjwa kama anavyosema mdau hapa wa mtandao wa JF kuwa Mkojo wa asubuhi ni dawa murua Shuhuda ni nyingi sana, moja ikiwa ni ya mdau huyu wa JF kutibu maumivu ya meno kwa kunywa mkojo wa asubuhi Miaka ya 2013-2016 nchini Tanzania kulitokea kundi la wanunuaji wa mkojo wa binadamu kwa madai kuwa unaenda kutumika kama dawa. Katika ukuaji wangu, mimi ni mmoja wa walioshawishika kutumia mkojo kwa kunywa au kupaka. Kwa kutokuzingatia suala la afya, nimewahi pia kunywa...
Wakuu nimeona hii taarifa kuwa Mbunge wa Chadema wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenan, ametangaza kuwa atashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu, akipinga kaulimbiu ya chama chake ya "No Reform, No Election," inayosisitizwa na Mwenyekiti Tundu Lissu. Taarifa imeongeza kuwa akizungumza na wananchi wa jimbo lake, Khenan alisema kaulimbiu hiyo haina mashiko kwani ni msimamo wa mwenyekiti pekee na si wa wanachama wote. Alibainisha kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema hawaungi mkono kususia uchaguzi, wakiona kuwa hatua hiyo inakiuka sheria na kuwanyima wananchi haki yao ya kupiga kura. Kama kweli, basi atakuwa amekisaliti chama kilichompa dhamana.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…