Katika kile kinachoonekana kama tukio la kihistoria na lisilotarajiwa katika ulimwengu wa Kiislamu, taarifa kutoka Mashariki ya Kati zinaeleza kuwa mwana wa kifalme kutoka familia ya kifalme ya Kuwait, anayefahamika kwa jina la Prince Abdullah Al-Sabah, ametangaza hadharani kuwa ameokoka na sasa ni mfuasi wa Yesu Kristo.
Katika faili la sauti lililorushwa kupitia kituo cha televisheni ya Kikristo cha Al-Haqiqa, kinachorusha matangazo kwa lugha ya Kiarabu, sauti inayodaiwa kuwa ya Prince Abdullah inasikika akitangaza kwa ujasiri kuwa amemkubali Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.
Katika ujumbe huo wa sauti, Prince Abdullah anasema kwa uthabiti kwamba:
“Iwapo nitauliwa kwa sababu ya rekodi hii ninayozungumzia wokovu...