Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,805
- 1,873
Wakatoliki ndio wameamua kuichafua CCM na CUF, kwa kupitia njia kama hizo.Lugha ya huo waraka ina 'harufu' ya wafitini wa Kanisa Katoliki. Sijawahi kuona Kanisa Katoliki likiandika waraka unaosambazwa kwa maaksofu, mapadre na wachungaji na usio na jina la mwandishi wala publisher. Ni lini Kanisa Katoliki likawa na wachungaji? Ni akina nani hawa? Na mwandishi ni nani: maaskofu, mapadre au wachungaji?
Ila tukinusanusa tutakuja kugundua kwamba walioutunga ni wale wanaousambaza pia!
Hawawezi kuandika waraka ulio wazi kama ule wa mwanzo, kwa sababu joto yake ya ule wa mwanzo walishaupata. Kwa vile lengo lao bado halijatimia basi watakuja kwa rangi tofauti na kutumia watu aina tofauti ikibidi hata wasio wakatoliki.
Watanzania wameamka si wale waliokuwa wakidanganywadanganywa kila siku, hususan kwa kutumia mapadre, maaskofu na makadinali.
Ninachoamini ni kwamba, huo waraka umeandikwa na viongozi wa kanisa katoliki, lakini unawezekana kuwa si wa kiofisi. Ninamaanisha kuwa umeandikwa na viongozi bila kupitia taratibu maalum za kanisa. Kuna uwezekano kuwa kitengo cha propaganda hapo makao makuu ndicho kilichotumika kufanya kazi hiyo, kwani lengo la safari ya barua ya kwanza iliyoanza mwezi wa 7 bado halijatimia.
Janja yao imegundulika. Tuachieni TZ yetu ya amani.