Waraka wasambazwa kuitafuna CCM 2010, kanisa Katoliki laukana

Salva Rweyemamu kazi yake hiyo na huo waraka umeandaliwa na jamaa mmoja ktk ofisi ya akina salva na miongoni mwa aliyeupeleka same ni dogo mmoja hivi anaishi kigurunyembe moro.
 
Huu waraka umeandikwa na wabaya wa CHADEMA iwe ni CCM, NCCR au vikundi fulani vya waislam nk, lakini lengo kubwa si kuchafua kanisa katoliki bali kuchafua chadema. Hisia zinaniambia Mhe. Makamba anajua huu waraka unatoka wapi. Tungekuwa na vyombo vya upelelezi makini kama FBI ni wiki moja mchawi angepatikana.
Acha kuwazulia watu, watanzania ndio maana hampati maendeleo; kuzuliana tu. Wazo jema hapa ni kuvitaka vyombo husika vichukue hatua za kumbaini huyu mchonganishi wa watanzania, au huoni kuwa waraka huu unachangisha dini mbili kwa kutumia siasa?
 
Salva Rweyemamu kazi yake hiyo na huo waraka umeandaliwa na jamaa mmoja ktk ofisi ya akina salva na miongoni mwa aliyeupeleka same ni dogo mmoja hivi anaishi kigurunyembe moro.
Hii 2010 mbona inakuja vibaya!!!?
 
JK hana sababu ya kuonewa huruma kwani yeye mwenyewe anajitosheleza kwa ukakamavu na uongozi thabiti,tatizo lenu mliomadogma mkipumbazwa tuu mmepambazishwa!Mtasema sana lakini ukweli utabaki palepale JK ndiye chaguo la watanzania wengi wenye kutaka amani na utulivu sasa kama nyie mnataka fujo(na tayari tunawajua kawaida yenu ni fujo hata mashuleni mlifahamika) ameni nchi na mwende kwa ndugu yenu M7 tuachieni nchi yetu
pengo lete mawazo ujenge nchi yako. JF siyo uwanja wa matusi. hapa unatakiwa umwage points kwa hoja zipi unafikiri waraka huo siyo propaganda za hao wanaosemwa. hapo utaonekana kuwa mwana tafakuri na hujawa personally dogmasified.
 
huu waraka ndio uliompeleka methodius kilaini BUKOBA!........STUKA

Hizi ni fikra duni sana. Hii ni mara ya pili waraka wa aina hii kusambazwa na 'System' kwa lengo la kuiharibia Chadema ili kionekane kuwa chama cha kidini zaidi kama ilivyo CUF. Kanisa Katoliki lina wasomi waliobobea na ni 'very understanding', Kamwe hawawezi kuandika ujinga kama huo. Hivi ndivyo watu wetu wa 'system' wanavyotumika. This is very unfortunate!
 
Huu waraka lazima umeandikwa na propaganda machinery ya CCM ili kuwadumaza wananchi waone kana kwamba Kanisa linamuonea Kikwete kwa hiyo apate sympathy ya waislamu na ndio maana umesambazwa misikitini!! Waraka wa wakisto husambazwa kanisani na unawahusu wakisto na si vinginevyo; hizi spin za watu wa aina ya Salva Rweyemamu!!

Kwa hili tunatumia "kana kwamba Kikwete anaonewa"? Kwani si kauli zetu na tunaamini kwa dhati kuwa Kikwete anastahiki anayoambiwa kwenye waraka huu? Si tunaamini kuwa hapendwi na wananchi kwa vile hajawatendea chochote?
Pengine kuna watu ndani ya hilo kanisa waliokwenda mbali juu ya mtizamo wao na hao ndio wachawi na si CCM.
 
Hapa hakuna cha Methodius Kilaini wala nani...ni machinery ya ccm at peak of work!

Wanatafuta legitimacy kwa mbinu ya kijinga hawa., na bahati mbaya imestukiwa...Hizo ni alama za nyakati kwao, na wakae wakijua kwamba wakati wao wa kuwepo unahojiwa na watu...!

Mwenye macho na aone!

Kila mtu atabeba msalaba wake! Hii ndio matokeo ya umbelembele. Tatizo ni kuwa likshakuganda tabu kulinasua. Kanisa walielew hilo.
 
Pia Kanisa Katoliki wangehusika na waraka huu wangesema wazi, maana hawana tabia ya kujificha, hasa inapokuja orientation yao ya masuala ya hatima ya nchi hii. These guys are bold and they never operate in darkness for a sensitive matter like this!

Pia Kanisa hilo hilo lina walio na msimamo mkali zaidi. Kama kanisa halihusiki basi lijisahihishe kwani unapofanya jambo na kutaka sifa wabaya wako ni rahisi kutumia sifa hiyo kukumaliza.
 
Acha kuwazulia watu, watanzania ndio maana hampati maendeleo; kuzuliana tu. Wazo jema hapa ni kuvitaka vyombo husika vichukue hatua za kumbaini huyu mchonganishi wa watanzania, au huoni kuwa waraka huu unachangisha dini mbili kwa kutumia siasa?

Walioandika wanajuwa kuwa hiyo dini nyengine haina ubavu kwani waraka original ulikuwa na matokeo gani? Walioundika ni dini moja ikijipendelea kwa kuona wanachohitaji wa dini ya pili si stahiki kwa vile matakwa ya upande mmoja ndio yanayofaa kusikilizwa.
 
Hizi ni fikra duni sana. Hii ni mara ya pili waraka wa aina hii kusambazwa na 'System' kwa lengo la kuiharibia Chadema ili kionekane kuwa chama cha kidini zaidi kama ilivyo CUF. Kanisa Katoliki lina wasomi waliobobea na ni 'very understanding', Kamwe hawawezi kuandika ujinga kama huo. Hivi ndivyo watu wetu wa 'system' wanavyotumika. This is very unfortunate!

Mzee naona kama huna tofauti na hao waliotowa waraka.
 
President Kikwete is The Best of The Best! Has nothing to go antagonistically with Catholic Church, neither a Mosque! Kilaini transfer is normal staffing procedure of the Church strategic level. Waraka huo ni wa wahuni si wa kanisa.
 
Kwani huu waraka una sahihi za nani ? Maana nyaraka za wakatoliki zina sahihi za watu special wanao utoa . Chadema leo uchaga umeisha sasa wanalia na udini ? Kitu gani nitafanya Chadema kuwa chama cha kanisa na CCM isiwe chama cha msikiti kwa mpangilio ule ule ?Malumbano ya kijinga na dawa kwa CCM ni ku deliever na kuwapa watu maisha stahiki na si ujinga huu kila kukicha .
 
Waraka huo unaendelea kudai kuwa chini ya awamu ya tatu ya Rais Alli Hassan Mwinyi, kanisa liliweza kudhibiti na kurudisha heshima yake lakini katika awamu ya nne kumekuwa na udhalilishaji wa kanisa wa kiwango cha juu.

apo kwenye red,waraka feki ndo umechemsha,au ni mwananchi.....
 
JK hana sababu ya kuonewa huruma kwani yeye mwenyewe anajitosheleza kwa ukakamavu na uongozi thabiti,tatizo lenu mliomadogma mkipumbazwa tuu mmepambazishwa!Mtasema sana lakini ukweli utabaki palepale JK ndiye chaguo la watanzania wengi wenye kutaka amani na utulivu sasa kama nyie mnataka fujo(na tayari tunawajua kawaida yenu ni fujo hata mashuleni mlifahamika) ameni nchi na mwende kwa ndugu yenu M7 tuachieni nchi yetu

Ndugu yangu Pengo
Acha jaziba, kama JK ni chaguo la watanzania mbona CCM haijiamini sasa hadi ianze kuandika waraka wa uongo? mbona hata wewe hujiamini unataka watu waende kwa M7 wakuachie nchi, unataka wakuachie wewe na nani, utaiweza? au kwa vile una keyboard ya kubonyeza tu.

Aliyeutunga huo waraka alifikiri anaandikia mbumbumbu wasiojua kitu. Kwanza timing yake , location, na watu wanaoueneza inaonesha kabisa mlengwa ni nani kwa sababu uko biased tofati na Waraka halisi uliotolewa kanisani. Sasa kama ni wa wananchi wote kwanini utolewe kwa siri na mtoaji mwenyewe si muhusika?
 
Unajua wazi kwamba serikali ina mkono mrefu hivyo haiwezi kuamini mambo kama ya Mwananchi. Kanisa katoliki halifanyi mambo kiholela wala kwa kutaharuki. Kanisa lina taratibu zake na uchukua mkondo wa ngazi zote.Kama ni kupinga mahakama ya kazi ili lilifanyika bila kificho na waraka kuhusu uchaguzi 2010 upo madukani unauzwa.

Katika gazeti la kiongozi la wiki hii Mwenyekiti wa Baraza la TEC Askofu Rwaiichi ametoa wito kwa watu kuzingatia maoni ya Waraka wa kanisa ( kwa wanaotaka) katika kuchagua viongozi 2010 bila kumungunya maneno. Sasa waraka huu wa siri ni wa nini. Mwananchi walitaka kuuza gazeti na isingewezekana kuuza bila kuingiza kanisa katoliki.What a shame!
 
..hii ni kazi ya wanamtandao.

..wamezoea kupata madaraka kwa njia za ulaghai.
 
Waraka huu umeandikwa na wakatoliki kuendeleza mikakati yao kama kawaida,
Hawa jamaa wanamambo mengi ambayo mengine hivi karibuni yameshtukiwa na wa Tanzania, kamavile kusaini memorandam za siri na serikali, nk

Sasa dili lililo kuwa la siri kwa mapadre, limeshtukiwa sasa wanalikataa, mengi yatajitokeza na siri nyingi zitafumbuka, na mtawatamani sana viongozi waliokuwa wanailinda Catholic party warudi!!

This is transparency Gorverenment, ujinga wote utajulikana, na catholic mtakana mengi, unafiki unaanza kufichuka.

Yote yaliyoandikwa kwenye waraka yalikuwa tayari yanafahamika kwa watanzania anyway! sas wanakana nini? No more excuse!!!!!!
 
CCM wana kikosi kazi chao kinachoendeleza propaganda na total chaos ili kuweka mambo sawa kwa upande wao.
Hivyo watakuja na mbinu chafu zaidi ya hizi na zaidi ya zile za idi amini alizotumia kuwatuhumu wapinzani wake......

FUNGUKA
 
Wakuu
Hapa inabidi kufikiri zaidi. CCM huwa kuna kamati ya Fitna. Na hii kamati kazi yake ndiyo hii ya kufitinisha ili kuchanganya watu.

Pamoja na haya, nafikiri zaidi ifuatavyo:
-Wilaya ya Mwanga, kuna Waislamu wengi kuliko Wakiristo
-Mbunge wao ni Mwislamu
-Anaonekana kukabwa koo na mgombea Mkristo
-Kawaida ya watu wa Mwanga hawana udini katika uchaguzi
-Watu wa Mwanga huwa wana ugonjwa wa "Ugweno" na "Usangi"

Kwa hiyo, waraka huu feki kautafuta Profesa Maghembe ili kumwaga fitna ili kuokoa jahazi.

BTW: Huu waraka feki ulishajadaliwa hapa jamvini kipindi tunajadili waraka wa Kanisa Katoliki. Kilizuka kikundi fulani DSM kikaandika huu feki ili kupotosha ule wa wazi. Profesa ameukimbilia ili umwokoe lakini si mpya na ndiyo maana umesomwa msikitini na msomaji alikuwa Profesa mwenyewe. Habari ndiyo hiyo.
 
Waraka huu umeandikwa na wakatoliki kuendeleza mikakati yao kama kawaida,
Hawa jamaa wanamambo mengi ambayo mengine hivi karibuni yameshtukiwa na wa Tanzania, kamavile kusaini memorandam za siri na serikali, nk

Sasa dili lililo kuwa la siri kwa mapadre, limeshtukiwa sasa wanalikataa, mengi yatajitokeza na siri nyingi zitafumbuka, na mtawatamani sana viongozi waliokuwa wanailinda Catholic party warudi!!

This is transparency Gorverenment, ujinga wote utajulikana, na catholic mtakana mengi, unafiki unaanza kufichuka.

Yote yaliyoandikwa kwenye waraka yalikuwa tayari yanafahamika kwa watanzania anyway! sas wanakana nini? No more excuse!!!!!!

Wanataka kukimbia upuuzi wao, kanisa katoliki ndio limeandika huu waraka likazambaza kwa siri kuona joto linaendaje

Christian fundementalist at work! shame on them, wamezoea "Kupendelewa" hawataki justice lol
 
Back
Top Bottom