- Thread starter
- #21
Kuna kitu kimenistua sana kuhusu waandishi wa habari. Naweka habari yote toka mwananchi na Tanzania Daima. Habari zinafanana utadhani zimeandikwa na mtu mmoja. Nani ameendika hii habari? Na hakuna jina la mwandishi kwa magazeti yote mawali! Kuna nini hapa?
Gazeti la mwananchi
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania inatarajia kuchangia jumla ya Sh130 bilioni kama malipo ya kodi kwa katika mwaka wa fedha 2012/13.
Malipo hayo yataifanya Vodacom kufikisha zaidi ya Sh700 bilioni ilizokwishalipa kama kodi tangu mwaka 2001.
Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa, baada ya kukutana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza alisema malipo ya kodi kwa serikali yamefikia zaidi ya asilimia 60 ya jumla ya uwekezaji wa Vodacom wa Sh 1.13 trilioni tangu mwaka 2001.
Meza alisema kampuni yak ina mipango wa kutumia zaidi ya Sh120 bilioni katika kuboresha mtandao, huduma na maendeleo ya uanzishwaji wa teknolojia mpya katika mwaka wa 2012.
Alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kuendelea kulipa kodi ipasavyo kwa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Hivi punde tumeboresha mtandao kwa zaidi ya Sh100 bilioni kufikia mwishoni mwa Machi 2012, na tunao mpango wa kuwekeza zaidi ya Sh120 bilioni ili kuendelea kuimarisha mtandao wetu nchi nzima.
Vodacom pia imetengeneza ajira 450,000 ikiwa ni pamoja na za mawakala wa M- Pesa, wauzaji wa jumla na wadogo pamoja na waajiriwa wengine 450 wa moja kwa moja katika kampuni, alisema Meza.
Aliongeza kuwa kampuni pia imetoa zaidi ya Sh3.4 bilioni kwa serikali kama mchango katika Mfuko wa Maendeleo ya Huduma za Mawasiliano Vijijini, wa kuisaidia jamii kuwa na mipango ya uwekezaji katika katika nyanja ya mazingira na wanyama pori, elimu, afya na ustawi wa jamii.
Gazeti la Tanzania Daima
KAMPUNI ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, inategemea kuchangia jumla ya sh bilioni 130 kama malipo ya kodi katika mwaka wa fedha wa 2012/13.
Malipo hayo yataifanya Vodacom kufikisha zaidi ya sh bilioni 700 ilizokwisha lipa kama kodi tangu mwaka 2001.
Akizungumza jana baada ya kukutana na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, alisema kuwa malipo ya kodi kwa serikali yamefikia zaidi ya asilimia 60 ya jumla ya uwekezaji katika shughuli zake kuanzia mwaka 2001 ambayo inafikia jumla ya sh trilioni 1.13.
Aidha, Meza alisema kampuni ina mipango wa kutumia zaidi ya sh bilioni 120 katika kuboresha mtandao, huduma na maendeleo ya uanzishwaji wa teknolojia mpya katika mwaka wa 2012/13.
Meza alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo katika kuendelea kulipa malipo yake ya kodi ipasavyo kwa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Hivi punde tumeboresha mtandao kwa zaidi ya sh bilioni 100 kufikia mwishoni mwa Machi mwaka huu, na tunao mpango wa kuwekeza zaidi ya sh bilioni 120 ili kuendelea kuimarisha mtandao wetu nchi nzima, alisema Meza.
Aliongeza kuwa, Vodacom pia imetengeneza ajira 450,000 ikiwa ni pamoja na mawakala wa M-Pesa, wauzaji wa jumla na wadogo pamoja na waajiriwa 450 moja kwa moja na kampuni.
Kwamba kampuni pia imetoa zaidi ya sh bilioni 3.4 kwa serikali kama mchango katika Mfuko wa Maendeleo ya Huduma za Mawasiliano Vijijini, ikiwemo kuisaidia jamii na kuwa na mipango ya uwekezaji katika jamii kwenye nyanja ya mazingira, wanyama pori, elimu, afya na ustawi wa jamii.
Meza aliongeza kuwa, kupitia kampeni ya moyo ambayo ina lengo la kutokomeza fistula na uboreshaji wa huduma za afya kwa wajawazito nchini, Vodacom imewekeza zaidi ya sh bilioni 21 kutoka kampuni mama ya Vodafone na Vodacom duniani.