Hawa ndio walipa kodi wakubwa nchini; NMB yabwaga Benki zote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jackbauer, Aug 27, 2011.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,893
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  Kwa ufupi:eek:nly one mining company,one telecom company,no gas/fuel company!!

  1.TBL(Tsh bilioni 165.4)

  2.NMB(Tsh bilioni 108.6)

  3.TCC (Tsh bilioni 92.1)

  4.NBC (Tsh bilioni 89.9)

  5.CRDB Bank Ltd(Tsh bilioni 79.2)

  6.Tanzani Ports Authority(Tsh bilioni 76.8)

  7.Tanzania Portland Authority(Tsh 73.4 bilioni)

  8.Airtel(T) Ltd(Tsh bilioni 63.6)

  9.Tanga cement company Ltd(Tsh 43.6)

  10.Standard chartered Bank Ltd(Tsh bilioni 40)

  11.Citibank(T) Ltd(Tsh bilioni 35.7)

  12.Resolute(T) Ltd(Tsh bilioni 32.1)

  13.TICTS(Tsh bilioni 25.9)

  14.Tanzania Distillers Ltd(Tsh bilioni 13.4)

  15.Group five international(PTY) Ltd(Tsh bilioni 9.5)

  source:hotuba ya waziri mkuu bungeni tarehe 28/8/2011.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,893
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 38
  Nashangazwa na performance ya haya makampuni katika ulipaji kodi.je yanakwepa kodi?kwa nini hajaingia top ten?
  MeTL,Azam,IPP,Vodacom,pepsi,serengeti brewries,barick gold mining etc.
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,331
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 38
  bado sana makampuni ya simu na migodi yanatakiwa kulipa zaidi ya hapo
   
 4. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 2,800
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 48
  Wajinga ndio waliwao..sasa kama dhahabu imefikia dola 1950 kwa ounce why Barrick haimo?!!
   
 5. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,086
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 36
  Hotuba ya waziri Mkuu haiko sawa kwasababu:

  Huo ndo mgodi mdogo wa dhahabu kuliko yote Tanzania, naongelea productionwise. Je, ni kiasi gani migodi ya Barrick Bulyankulu, Tulawaka, North Mara na Buzwagi imelipa kama kodi Serikalini?

  Je, GGM imelipa kiasi gani kwa kipindi hicho?

  Mbona Tanzania ndio mzalishaji mkubwa wa 3 wa dhahabu duniani na migodi inayoongoza hapa Tz, ni ile ya GGM na Barrick wakati kwenye ripoti ya PM, hawapo?
   
 6. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 20,852
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 63
  ipp mtamuonea bure,si anauza bodycare na mosguito coil.in short hana mawe
   
 7. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 18
  Hivi kwa nini Tanesco haiongozi?
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,985
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wakuu,Salaam!

  Kwa wale mliofuatilia Hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa kuahirisha Bunge Jana alitoa pongezi na kuzitaja Makampuni au Mashirika yanayoongoza kwa kulipa Kodi hapa nchini.

  Alisema kwa kipindi Cha mwaka 2005 na 2011 Makampuni hayo yamekuwa yakifanya vizuri katika ulipaji Kodi.

  Aliyataja Makampuni hayo Kama ifuatavyo


  "Mheshimiwa Spika,
  Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011.

  Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:


  i. Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);
  ii. National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);

  iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);

  iv. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);

  v. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);

  vi. Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);

  vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);

  viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);

  ix. Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);

  x. Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);

  xi. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);

  xii. Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);

  xiii. TICTS (Shilingi Bilioni 25.9);

  xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na

  xv. Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5)."  Source: Speech ya Waziri Mkuu Bungeni

  Haya Wakuu na tujadili na kutoa maoni yetu...
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,495
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Where's Vodacom, Geita Gold, Bulyanhulu, Artumas, Songas,North Mara, Buzwagi????????
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,495
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yaani group five inalipa kodi zaidi ya Barrick???????????? Kweli Tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 11. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 3,833
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 48
  Simon Group siioni hapo!
   
 12. m

  mkolosai JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 18
  PM nae kichekesho. Kamati ya bunge hesabu za serikali imedanganywa katika hili. Wapi vodacom na tigo? Na zinatunganya eti vodacom a leading cellular network na sasa hivi kazi ni kwako. Tigo nao wezi watupu. Kamati ya bunge husika ifuatilie hili suala kwa ukaribu
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga JF Platinum Member

  #13
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 11,136
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 38
  Ina maana watu wa madini hawalipi kodi au serikali haikusanyi kodi toka kwa makampuni hayo hasa hili kampuni kichefuchefu linalomiliki Nyamongo gold. Ni wakati muafaka sasa tuchukue migodi yetu tuiendeshe wenyewe huenda tukapata kodi toka huko.

  Sitaki kuziamini hizo data za pm. Kama ni kweli basi madini tuwape akina mafuru au kimei ili tupate kodi
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  Aug 27, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,651
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 38
  mmmmmh! hii kali, nimeshikwa na kigugumizi kwakweli
   
 15. W

  We can JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 672
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kuleta hasira tu kwa wa Tanzania. NMB ya walala hoi ndo inaongoza hata haya ma migodi? Sasa si tubaki na benki tu na kuwafukuza wawekezaji kwenye madini?

  Halafu, jana PM anasema mikoa mitano ya mwisho kwa uchumi wa watu wake kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kigoma, nk, huku akitaja fursa zilizopo kwenye mikoa hiyo kuwa ni pamoja na kilimo cha pamba, ufugaji, nk (hakutaja madini), ALINIUDHI MIMI? Yaani unawezaje kuitaja Shinyanga bila kueleza fursa za madini? Au madini haya kweli si ya kwetu, ooo my God.

  USANII MTUPU HAPA
   
 16. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 18
  TBL ya kwanza wanalipa 165 B kodi baada ya faida asilimia kubwa ya wateja wao ni wanywa bia duh watanzania tunakunywa pombe si mchezo hiyo na kampuni moja tu ya bia !
   
 17. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,568
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Wapi Vodacom,Barrick Gold, Azam na Presionair? Bandari yetu inazidiwa na wauza sigara?
   
 18. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 2,111
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 38
  Wapi Azam?
   
 19. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duh sijaona Vodacom, Tigo, Serengeti lazima hizi kampuni kuna mikono ya mafisadi badala ya kwenda serikalini kodi hizo wao ndo wanakula. Hawa Voda si wanajigamba ndo wenye wateja wengi TZ iweje wamepitwa na airtel katika ulipaji kodi??
   
 20. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,878
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 38
  pamoja na makamuni kama voda na ya madini kutoonekana kwenye ubora wa kulipa kodi
  lakini namba sita alitakiwa kuwa juu , hapo bandarini kuna kazi kubwa inatakiwa

  na wizi wanaofanya voda na makapuni ya madini ukomeshwe
   
 21. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #21
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inaonekana sekta ya madini hailipi kwa hakika,
  Serikali isimamishe uvunaji/uchimbaji wa madini kwa wawekezaji mara moja,
  Tusubiri baada ya miaka mitano ndio tuaangalie jinsi ya kuwekeza kwenye hii sekta ya madini.
  Eneo lingine ambalo linasikitisha ni UTALII, sekta hii inaiingiza pesa nyingi
  Uwezekano ni kuwa wakusanya kodi hawafuatilii au zinapenya kwa wajanja, nayo iangaliwe upya
   
 22. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #22
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,652
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 38
  Where is TANESCO ?! Where is Quality group! , where is Lafarge aka Mbeya cement ?
   
 23. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #23
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,985
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Dhahabu yetu inapotea bure,haisaidii uchumi wala kustabilize shilingi yetu!
   
 24. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #24
  Aug 27, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,975
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huko kwenye dhahabu ndo unanitonosha kidonda changu kilicho anza kupona.
  Jamaa hawa wanao jidai ndo wenye nchi wameziba pamba masikioni dhahabu jamaa wanasafirisha matani na matani.
  Inatia aibu mpaka mchanga nao wanasafirisha hayo mashimo watakuja kufukia na nini? Kama mpaka mchanga wanasafirisha.
   
 25. Nditu

  Nditu Senior Member

  #25
  Aug 27, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukiifuatilia hii nchi unaweza kujinyonga kwa maudhi. Kumbe kuna makampuni kibao yanayofanya kazi ya kutuibia tu hapa nchini na si vinginevyo! Hata hao wanaokusanya kodi ni vichwa vya wendawazimu kwani hawazishtukii kampuni kama Vodacom ambayo kwa vigezo vyovyote ndiyo wanaoongoza kwa uwingi wa wateja na bei ya bidhaa zao, Tigo ambayo hivi karibuni imesomba wateja wengi kwelikweli na ambayo bidhaa zake zinatozwa sawa kabisa na Zain na hata Vodacom?
  Halafu kuna faida gani kwa madini yetu kuchimbwa kwa fujo namna hii kama tunachopata kama mchango kwenye kodi ni kiduchu namna hii na hakiingii hata katika fungu la kumi la mapato yetu kitaifa? Kwa lugha rahisi ni kwamba kumbe tungeweza kufunga migodi yoye bila athari kubwa kwenye uchumi wetu. Ni aibu kwa wakusanya kodi na ni tusi kwa taifa kusikia kikampuni kama Group five kipo kwenye kumi na tano bora za walipa kodi wakuu huku kampuni kama Vodacom inayomgusa karibu kila mwananchi ikiwa mbaali kabisa!
  Mi nashauri tufanye yafuatayo:
  i. Iundwe tume huru ya wachumi waliobobea wakiwemo wabunge haswa wa upinzani chini ya jopo la majaji watatu kuchunguza makampuni yoote yanayokwepa kodi. (Kwa vile hawa wa CCM tayari wameshindwa kwa miaka yote hii kubaini wizi huu na inawezekana makampuni yanayokwepa kodi kama Vodacom yanalipa sehemu fulani CCM).
  ii. Kampuni itakayobainika kukwepa kodi ifilisiwe mali zake zote kufidia hasara waliyolipatia taifa.
  iii. TRA iundwe upya na Mkurugenzi wake awajibike kwa Bunge.
  iv. Watakaobainika katika TRA ya sasa kufunikafunika uhalifu huu wafunguliwe ya uhujumu uchumi.
  v. Mwisho wa yote tudai uwajibishwaji wa wahalifu hawa waliojificha kwenye chama kinachonuka rushwa cha CCM na serikali yao.
   
 26. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #26
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kila Jumanne na Alhamisi tofali za dhahabu zenye ukubwa wa tofali la kuchoma na uzito wa gramu 12000 zipatazo 400 husafirishwa kwenda nje ya nchi, Hebu jiulize Gramu 1 ya dhahabu huuzwa Tsh 65,000. Je ni kiasi gani cha fedha kinakwenda nje na je kinaweza kukidhi bajeti yetu? Pigeni hesabu kisha mnijulishe...! Je hii pesa haiweza kutuokoa na u-ombaomba kwa wazungu?


  Hiyo hesabu ni kwa GGM pekee, bado wapo NORTH MARA, KAHAMA, ULYANKULU, BIHARAMULO.

  Kwa nini pamoja na ukwasi huo bado tunaishi kimaskini?

  MAWAZO YAKO YANAWEZA KUTUPA DIRA TUKAEPUKA KUIBIWA

  MIMI NAAMINI KAMA TUKIKUSANYA KODI KWA MADINI PEKEE, MAISHA MAZURI KWA WATZ YATAPATIKANA BILA KWERE
   
 27. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #27
  Aug 27, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 1,327
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 48
  Is this information correct? Ina maana kodi kwenye mafuta hazilipwi kwa kiwango kikubwa? by the way, on monthly basis, which sector contributes more in revenue collection?
   
 28. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #28
  Aug 27, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 7,520
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwanadam anatawaliwa na mwanadamu mwenzake kwa hasara yake, si maneno yangu.
   
 29. ntagunga

  ntagunga JF-Expert Member

  #29
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Misingi ya makampuni kutokulipa kodi, ipo katika sheria za kifisadi kama vile SHERIA YA MADINI 2010, na SHERIA YA UWEKEZAJI TANZANIA. UKIZISOMA UTAPATA MAJIBU YA SERIKALI LEGELEGE KUSHINDWA KUKUSANYA KODI.

  SHERIA HIZO NDO CHANZO CHA MAKAMPUNI KUBADILISHA MAJINA KILA UCHWAO LEO.

  UDHAIFU UNAOPATIKANA KATIKA SHERIA HIZO, NI WAWEKEZAJI KULIPA KODI BAADA YA WAO KUTANGAZA KUPATA FAIDA. NANI ATATANGAZA KUPATA FAIDA KATIKA MAZINGIRA HAYA?
  HAPA KWETU WENYEJI TUNALIPA KODI KULIKO WAWEKEZAJI.

  WIZI MTUPU.

   
 30. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #30
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 23,914
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 63
  Hawalipi kodi, bado wanajiendesha kwa hasara
   

Share This Page