Mwakalinga Bujo
JF-Expert Member
- Oct 22, 2008
- 2,719
- 1,440
Kuna habari Michuzi blog inasema hivi:
"Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw Rene Meza akieleza jinsi Vodacom ilivyochangia zaidi ya shilingi billion 700 katika malipo ya kodi ya serikali alipokutana na waandishi wa habari mjini Dodoma".
Tarehe 28/08/2011 Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisoma bungeni orodha ya makampuni 15 yanayoongoza kwa kulipa kodi;
1.TBL(Tsh bilioni 165.4)
2.NMB(Tsh bilioni 108.6)
3.TCC (Tsh bilioni 92.1)
4.NBC (Tsh bilioni 89.9)
5.CRDB Bank Ltd(Tsh bilioni 79.2)
6.Tanzani Ports Authority(Tsh bilioni 76.8)
7.Tanzania Portland Authority(Tsh 73.4 bilioni)
8.Airtel(T) Ltd(Tsh bilioni 63.6)
9.Tanga cement company Ltd(Tsh 43.6)
10.Standard chartered Bank Ltd(Tsh bilioni 40)
11.Citibank(T) Ltd(Tsh bilioni 35.7)
12.Resolute(T) Ltd(Tsh bilioni 32.1)
13.TICTS(Tsh bilioni 25.9)
14.Tanzania Distillers Ltd(Tsh bilioni 13.4)
15.Group five international(PTY) Ltd(Tsh bilioni 9.5)
Je, Inawezekana Waziri Mkuu alitumia wrong data? Maana kama Vodacom wamelipa kodi shs 700 billion walitakuwa wawe Number 1. Hapa kuna mkanganyiko.
Kuna mambo yanachanganya sana ,VODACOM wameona biashara ya tel. ina-kodi zilizowazi wamehama na wameweka nguvu kubwa sana kwenye M-PESA .Ndio ujiulize inakuwa VODACOM haipo kwenye topten!!!!
Mpaka serikali itambue mchezo mchafu wa hizi kampuni za simu ,VODACOM ikiwa ndio kinara kwenye sekta ya mobile money tutakuwa tumebaki masikini wa kutupa.Wanalipa kodi bil 700 tokea kampuni ianzishwe wakati misamaha ya kodi tunayosamehe ni zaidi ya 1.2 Tril.,hii ni akili ama matope?.Misamaha mingi ya kodi inayotolewa ni kwa hizi kampuni za simu,kwa ujanja ujanja wa kudanganya kuwa kuna shughuli wanachangia kwenye maendeleo ya jamii (social responsibility)...mfano Miss Vodacom ni social responsibility !!!!!!