Vodacom, tigo na Zantel tuwape adhabu gani ili iwe mfano?

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
Baada ya kusoma makampuni bora kwa ulipaji kodi

Mheshimiwa Spika,
Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011.

Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:

i. Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4);
ii. National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6);

iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1);

iv. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9);

v. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2);

vi. Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8);

vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4);

viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6);
ix. Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6);

x. Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0);

xi. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7);

xii. Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1);

xiii. TICTS (Shilingi Bilioni 25.9);

xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4); na

xv. Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5).

Kutokana na vodacom kusema kila siku wao ni kampuni kubwa/mama ya mawasilino ya simu na internet nchi , inapokuja kwenye suhara la kodi wanakuwa sio kampuni mama/kubwa nchini, hapa wananchi tunakila sababu ya kuwa wajibisha hawa watu maana uwezo tunao.

Tutoe mfano kwa haya makamuni ya simu na tuipe support Airtel kwa uzalendo wao na hii itaijengea nchi heshima, sisi sio shamba la bibi tukubaliane chakufanya dhidi ya haya makapuni au waje hapa watueleze TATIZO ni nini?

Nawasilisha

Naunga mkono mimi tangu siku nyingi nilishaona Vodacon tunamchangia Rostam tuuu!!!si kwa faida ya taifa letu

Kwa kukwepa kodi wazawa ni noma!voda ina mkono wa wazawa sana ikiongozwa na gwiji RA,

Wakati sehemu hiyo inasomwa nilitegemea kusikia Vodacom ndio inaongoza kwa kulipa kodi kwa sababu ina wateja zaidi ya milioni 10 kumbe ndio hivyo . TRA wafuatilieni hawa jamaa. Tena ndio kampuni ya simu inayoongoza kwa kuwa na wateja wengi.

Nyinyi munadhani kwa nini hawataki kupeleka list kamili ya wateja wao? Kwa sababu hawataki kupigiwa mahesabu ya kulipa kodi.

Lakini kweli ni lazima watupatie maelezo ya kueleweka KODI ZETU HUWA ZINAKWENDA WAPI?

Na siku hizi mpesa inawaingizia faida kama utani na haipo kwenye kodi zao.

Baada ya kusoma makampuni bora kwa ulipaji kodi

Kutokana na vodacom kusema kila siku wao ni kampuni kubwa/mama ya mawasilino ya simu na internet nchi , inapokuja kwenye suhara la kodi wanakuwa sio kampuni mama/kubwa nchini, hapa wananchi tunakila sababu ya kuwa wajibisha hawa watu maana uwezo tunao.

Tutoe mfano kwa haya makamuni ya simu na tuipe support Airtel kwa uzalendo wao na hii itaijengea nchi heshima, sisi sio shamba la bibi tukubaliane chakufanya dhidi ya haya makapuni au waje hapa watueleze TATIZO ni nini?

Nawasilisha.

We vodacom walikuambia wanaongoza kwa kulipa kodi? Mtu akifanya marketing bila kuvunja sheria sioni

Shida hapo

Nyinyi munadhani kwa nini hawataki kupeleka list kamili ya wateja wao? Kwa sababu hawataki kupigiwa mahesabu ya kulipa kodi.

Lakini kweli ni lazima watupatie maelezo ya kueleweka KODI ZETU HUWA ZINAKWENDA WAPI?

Na siku hizi mpesa inawaingizia faida kama utani na haipo kwenye kodi zao.

nina hakika kila vocha ina VAT sasa nayo awapeleki, na azam naye ana udhuru gani? bidhaa zake zimejaa kila kona
ya masoko hapa nchi.

dawa kugomea bidhaa za makapuni kama haya itasaidia kuinua uchumi wa nchi, twende kwa wanaolipa kodi

We vodacom walikuambia wanaongoza kwa kulipa kodi? Mtu akifanya marketing bila kuvunja sheria sioni

Shida hapo

sio issue ya marketing to ni kweli kitakwimu wana wateja wengi hiyo haipingi,
na kama wanafanya uongo kwenye marketing zao huo nao ni ukweli ninataka kuujua
mkuu najua marketing kuliko unavyoweza ku image hakuna marketing hapo kuna ukwepaji kodi
full stop
VODA wa huduma ngapi wanatoa katika nchi hii ukiweka na bahati na sibu wanazochezecha kila kukicha

Nyinyi munadhani kwa nini hawataki kupeleka list kamili ya wateja wao? Kwa sababu hawataki kupigiwa mahesabu ya kulipa kodi.

Lakini kweli ni lazima watupatie maelezo ya kueleweka KODI ZETU HUWA ZINAKWENDA WAPI?
Na siku hizi mpesa inawaingizia faida kama utani na haipo kwenye kodi zao.
mkuu wanafanya REPATRIATION OF INCOME, mambo yote RA anapokelea bondeniiiiiii.......!

Tatizo ni kwamba kodi nyingi zinazolipwa zinaishia mifukoni mwa wachache na si kwa masilahi ya uma.

tuna matatizo lukuki ndani ya nchi yetu. Umeme wa uhakika hatuna, dawa hospitali hakuna kitanda kimoja wagonjwa wawili na wengine wanalala chini, elimu duni madawati hakuna waalimu wa voda fasta, maji ya uhakika hakuna miundo mbinu duni na mambo mengine mengi. hivi katika mazingira kama hayo hata kama ungekuwa wewe ni hamasa ipi ambayo ingekusukuma kulipa kodi!

Kuna mswada uliletwa bungeni i think in 2009 kwa hisia ya makampuni ya simu yawelisted kwenye soko la hisa ili wananchi waweze nao kunufaika kwani wanachangia kwa kiasi kikubwa makamuni haya....wajanja chini chini wakaizima na huo mswada ukazimwa lakini wabunge wachache walioshtukia wakatulizwa...mswada huu hasa ulikuwa unailenga campuni ya vodacom kwani mapato mengi yanopatikana yananufaisha makaburu na wajanja wa mjini(wahuni wa nchii hii).

Huo mswada umepigwa vita sana na Vodacom. Kuna kitu kinaitwa CONSUMER POWER - Na nadhani kama watanzania tunataka nchi hii ielekee kwenye mstari sahihi hatuna budi kuchukua hatua. Hama. Vodacom wanatamba kila siku na kauli ya 'Tanzania leading cellular network' sasa wanaongoza nini? Na kumbuka hawa Voda wana-corporate clients wengi sana ambao wanalipa vizuri mno. Haiwezekani under the sun Airtel walipe kodi kubwa kuliko Vodacom. Hapa kuna wizi wa mchana kweupe.

Mnauliza kodi ya Vodacom iko wapi ? wakati wa uchaguzi mliona bango la Voda ? mabango yao yote yalishushwa na kupandishwa ya mgombea mmoja hivi,halafu zile kofia,fulana na kanga mnadhani zilitoka wapi ? TRA wana ubavu wa ku-deal na Voda ?

una maana jk, sasa kama ndio mpango wenyewe wamepingwa bao , sisi wananchi tutawachukulia hatua ili akili iwakae sawa

Nafikiri watu wakijua majority share zinamilikiwa na nani, na composition ya bodi ya wakurugenzi wanamuelekeo wa chama gani, utapata jibu kwanini hawakutokea ktk top five na huku wanapata faida kubwa

kuwa kampuni kubwa haina maana kupata faida kubwa.

hii ni biashara gani unaongerea? Tunaongea biashara ya simu ambayo kuna kampuni imepata faidi wao kama wanapata hasara wanamudu vipi ushindani?

Wewe sema wamejificha kwenye udhamini wa matamasha kisha kusema wametumia mabilioni huko na hivyo kuiba kodi ya nchi hakuna kingine wanatumia udhamini kuiba kodi

Back
Top Bottom