Kushindanisha UDOM na UDSM ni kutokitendea haki UDSM. Baadhi ya waadhiri wengi wa UDOM ni product ya UDSM na bado UDOM haijaweza kuwa na wadhadhiri au maprofesa wa kusema wamesheheni kila idara. Wengi wa wahadhiri wake wana uzoefu chini ya miaka kumi. Ukihesabu wenye machapisho ya utafiti zaidi ya 10 ni wachache sana kwa UDOM. Kama tukiwa objective kwa Tanzania chuo cha kulinganisha na UDSM ni SUA, Muhimbili, Mzumbe na IFM. Na kwa mbali vyuo vya ST. Augustine na Tumaini. Lakini kwa kuangalia kozi wanazotoa kila chuo kinakuwa kizuri kwa aina ya kozi zake. SUA kilimo na kozi za wanyama mfano BVM, Mzumbe kwa kozi za uongozi, UDSM, kwa kozi za sheria, ualimu, uandisi, etc.