Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Tarehe 5 Juni 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.

Kufuatia Taarifa hiyo kwa Umma iliyotolewa kupitia tovuti ya Bunge, kumekuwa na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kwamba "Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya undeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka mia moja (100)".

Kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau wa Kitaifa a Kimataifa na Umma kwa jumla kwamba, taarifa hizo sio sahihi, ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu ya kukwamisha mipango thabiti ya Nchi katika kuongeza ufanisi wa Sekta ya Bandari Nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.

Taarifa sahihi ni kuwa, Azimio la Bunge linahusu Mkataba ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi kumi na mbili (12) kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika boreshaji na endelezaji wa Sekta ya Bandari Nchini Tanzania.

Ushirikiano wa Nchi mbili za Dubai a Tanzania una lengo la kongeza ufanisi wa huduma za Bandari Nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dares Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda (Special Economic and Industrial Zones) kwa kujenga viwanda pamoja na uwekezaji katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Bandari za Tanzania kwenda chi za jirani ambazo zinatumia Bandari zetu.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawaomba Wateja, Wadau na Umma kutambua kwamba, jitihada zote na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuvutia wekezaji Nchini hususan kwenye maeneo ya Banadari, zinalenga kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli, mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika Bandari zetu.

IMG_7494.jpeg
IMG_7495.jpeg


Pia soma: Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam
 
Tanzania ina bandari muhimu kama vile Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni kiungo muhimu katika biashara ya kimataifa. Kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza sekta hii, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya mazungumzo na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii.

Ushirikiano huu unalenga kuongeza ufanisi na uboreshaji wa utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Lengo kuu ni kuboresha miundombinu ya bandari, kufanya uwekezaji katika teknolojia ya kisasa, na kuongeza uwezo wa bandari kukabiliana na mahitaji ya biashara ya kimataifa.

Hata hivyo, kumekuwa na uvumi na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kuhusu azimio hili la ushirikiano. Taarifa potofu zimeenea kwamba Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya uendeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka 100.

TPA inasisitiza kuwa taarifa hizo sio sahihi na ni upotoshaji unaofanywa kwa nia mbaya. Azimio hili la Bunge linahusu mkataba wa ushirikiano ambao una ukomo wa miezi 12 tu. Lengo la mkataba huo ni kutoa fursa kwa Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kujadiliana kwa kina kuhusu maeneo ya ushirikiano katika uboreshaji na uendelezaji wa sekta ya bandari nchini.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania inatoa wito kwa wateja, wadau wa kitaifa na kimataifa, na umma kwa ujumla kutokuamini taarifa potofu zinazosambazwa. Wanasisitiza kuwa azimio hili linalenga kuleta maendeleo na ufanisi katika sekta ya bandari nchini kwa faida ya taifa letu.

Ni muhimu kwa umma kuwa na uelewa sahihi kuhusu azimio hili na kusubiri taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka husika. Ushirikiano wa kimataifa na uboreshaji wa sekta ya bandari ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wetu na ustawi wa taifa letu kwa ujumla.
WhatsApp Image 2023-06-06 at 11.15.01 PM.jpeg
 
Cha Cha mboga mboga kinapaswa kuachia hii nchi maana wanauza nchi kwa maslahi ya matumbo Yao na sio umma wa Watanzania.

Alafu hawa wanao jiita mamlaka ya bandari toka lini wamekuwa wasemaji wa serikali ? Waache ujinga watanzania sio wapumbavu.
 
91d629f8-4bee-4cd1-926e-a1fb51a260a2.jpg


Bunge la Tanzania linaalika umma kutoa maoni juu ya azimio lake kuhusu mapendekezo ya kuridhia makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai juu ya uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari nchini Tanzania.

Kuna tuhuma nzito katika mitandao ya kijamii kuwa Serikali inataka kuikodisha Bandari kwa taifa Hilo la Uarabuni kwa muda wa miaka 100. Tuhuma hizo zinazidi kutatanisha zaidi hasa pale zinapotaja kuhusu Wabunge 'kuwekwa sawa' ili wapitishe hoja hiyo. Kama tuhuma hizo zina ukweli basi tutakuwa tumefikishwa mahali pabaya sana kama taifa.

Kukodisha Bandari kwa miaka 100 ni sawa na kuuza Bandari kwani kati ya wote tuliopo sasa na watakaozaliwa kesho, hakuna atakayefikia miaka 100 akiwa na nguvu. Uamuzi wa aina hiyo unatakiwa ufikiwe kwa uwazi na uelewa wa hali ya juu. Haiwezekani Wabunge ambao waliingia Bungeni kwa nguvu ya Dola lakini pia waliokosa ridhaa ya wananchi walio wengi ndio wapewe jukumu la kuamua kuhusu hatima ya jambo kubwa kama hilo.

Sisi Askofu Mwamakula tunapenda kutoa wito kwa Serikali yetu kutoka hadharani na kuzitolea ufafanuzi tuhuma hizo kabla ya kuendelea na jambo hilo. Lakini pia, tunatoa wito kwa umma wa Watanzania kuungana kwa maslahi mapana ya taifa na vizazi vijavyo kuitaka Serikali uwazi kuhusu mikataba hiyo. Kadharika, tunatoa wito kwa Bunge na Serikali kutofanya haraka katika kuingia mikataba ambayo umma haijaielewa.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

Dar es Salaam, 6 Juni 2023.
 
Back
Top Bottom