TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Hapo sasa.

Watu wengi hawawezi kukuelewa unachosema hapa.

Hii serikali ni ya ujanja ujanja sana. Ina ulaghai mwingi sana. Ni watu wachache sana, kama Tundu Lissu wanaoweza kutambua ulaghai mwingi unaotumiwa na watu hawa..

Hata Mbowe bila shaka bado kanasa kwenye kokolo la hawa walaghai wakubwa!

Kila jambo, wao ni ujanja ujanja tu, hakuna wanachokwambia cha ukweli moja kwa moja!.
Royal Tour hadi leo ni kitendawili. Wamasai wanahamishwa kule ili wapishe mawindo ya wenye pesa;. hakuna anayejua pesa za ujenzi wa zile nyumba Handeni zilitoka wapi!

Hii ni serikali inayouza wananchi wake utumwani wao wakichekelea kwa kudai wamewapa wananchi ajira!
Hii ni balaa!
 
Yajayo yanafurahisha. Kwanza tunapigwa na MATOZO YA KUFA MTU. TUNAKOPA KAMA TUNAKUFA KESHO. TUNAWAPA MIKATABA HAO WALIOWAFANYA WATUMWA BABU NA BIBI ZETU.
TWAULIZA VIONGOZI WETU NI WATANZANIA AU WAGENI??!!!
😭😭😭😭😭😭😭😭😭
 
Wachangiaji wengi humu ni wajinga. Nchi haikurupuki tu bila deep scrutiny. Bandari yetu kwa sasa inanifaisha wachache. Pia inafanya kazi chini sana ya kiwango na kwa gharama kubwa. Ni lazma awepo mwekezaji kama huyo ili kuweka tija. Sioni anaeshauri nini kifanyike mbali ya KUHARISHA NGONJERA TUPU. Hovyo kabisa
 
Serikali imechukua mkopo kuboresha Bandari ya DSM ikiwemo kuongeza kina ili meli kubwa zaidi ziweze kutua. Baada ya maboresho hayo kabla taifa halijafaidi matunda yake anakodishwa mwarabu. Kwa hiyo serikali ilienda kukopa ili imfaidishe muarabu ama??!!
 
Tarehe 5 Juni 2023, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitoa Taarifa kwa Umma kuhusu mwaliko wa Wadau wote kutoa maoni kuhusu Azimio la Bunge la mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii kwa ajili ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania la Mwaka 2023.

Kufuatia Taarifa hiyo kwa Umma iliyotolewa kupitia tovuti ya Bunge, kumekuwa na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kwamba "Serikali imepanga kuipa kampuni ya DP World ya Falme ya Dubai kandarasi ya undeshaji wa shughuli za Bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa miaka mia moja (100)".

Kufuatia kusambaa kwa taarifa hizo, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau wa Kitaifa a Kimataifa na Umma kwa jumla kwamba, taarifa hizo sio sahihi, ni upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na watu wenye nia ovu ya kukwamisha mipango thabiti ya Nchi katika kuongeza ufanisi wa Sekta ya Bandari Nchini kwa maslahi mapana ya Taifa.

Taarifa sahihi ni kuwa, Azimio la Bunge linahusu Mkataba ambao Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaingia na Serikali ya Dubai wenye ukomo wa miezi kumi na mbili (12) kwa ajili ya kutoa nafasi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliana na Serikali ya Dubai kuhusu maeneo ambayo Serikali hizo mbili zinaweza kushirikiana katika boreshaji na endelezaji wa Sekta ya Bandari Nchini Tanzania.

Ushirikiano wa Nchi mbili za Dubai a Tanzania una lengo la kongeza ufanisi wa huduma za Bandari Nchini, kukuza ajira za Watanzania na kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji kwenye baadhi ya maeneo ya Bandari ya Dares Salaam, maeneo huru ya kiuchumi na viwanda (Special Economic and Industrial Zones) kwa kujenga viwanda pamoja na uwekezaji katika mnyororo mzima wa usafirishaji kutoka Bandari za Tanzania kwenda chi za jirani ambazo zinatumia Bandari zetu.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inawaomba Wateja, Wadau na Umma kutambua kwamba, jitihada zote na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuvutia wekezaji Nchini hususan kwenye maeneo ya Banadari, zinalenga kumaliza changamoto za muda mrefu ikiwemo ucheleweshwaji wa meli, mizigo na kukosekana kwa ufanisi katika Bandari zetu.

View attachment 2648437View attachment 2648438

Pia soma: Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam

Hivi wananchi watatoaje mawazo yao bila kuweka mkataba wazi. Wanatoa mawazo ya nini hasa? Yaani wananchi wakubali tu bila kujua tunanufaika vipi na mkataba ni wa muda gani? Badala ya kujibu waweke mkataba hapa
 
Wachangiaji wengi humu ni wajinga. Nchi haikurupuki tu bila deep scrutiny. Bandari yetu kwa sasa inanifaisha wachache. Pia inafanya kazi chini sana ya kiwango na kwa gharama kubwa. Ni lazma awepo mwekezaji kama huyo ili kuweka tija. Sioni anaeshauri nini kifanyike mbali ya KUHARISHA NGONJERA TUPU. Hovyo kabisa
Mambo watakaofanya hao waarabu ni mepesi sana hata sisi tunaweza kufanya
 
Mpaka sasa hakuna kiongozi wa upinzani kaongea lolote sijui vijana ccm akili zenu zipo matakoni
Kuna upotoshwaji mkubwa sana unafanywa juu ya mkataba unaotaka kusainiwa kati ya serikali na kampuni ya DP World na wanasiasa wa upinzani na watu wasio na taarifa sahihi kuhusu jambo hili.

Watu wetu wamezoea kutokusoma mambo na kuokota mambo mitandaoni na kutafanya kuwa ndiyo rasmi. Nimesoma makubaliano haya kurasa zote 33 sijaona mahali palipotajwa miaka 100 imekubaliwa kukodishwa DP World bandari.

Sijajua wanaosema bandari imekodishwa miaka 100 wanatoa wapi hizi taarifa! Ni tabia ile ile ya kuzusha mambo na kupayuka bila kuwa na ushahidi. Tabia hii inaleta taharuki sana kwa watanzania bila sababu za msingi.

Wote ni mashahidi wa jinsi TICTS na akina Karamagi wamefanya kazi bandarini kwa miaka 26 na hakuna uwekezaji wamefanya mpaka wamepelekea bandari ya Dar Es Salaam pamoja na umuhimu wake kuzidiwa na bandari mpaka ya Mombasa kwa sababu huduma mbovu na TICTS hawakuwa wanawekeza kwenyw kununua vifaa kwa miaka yote 26 ya mkataba wao. Hatuwezi kuwa na bandari haina vifaa na meli zinasubiri siku 14-21 kupakua mizigo wakati jambo hilo kilitakiwa kufanywa kwa masaa 12-24 tu na hicho ndicho kiwango cha kimataifa cha ufanisi wa bandari kupakua mizigo.

Nani aliwahi kuhoji miaka 26 ya TICTS kuwa watoa huduma hapo bandarini? Nani aliwahi kuwaza na kujua TICTS wamekaa hapo bandarini kwa miaka 26? Marais wangapi wamepita na hawakuwa na uthubutu wa kuwaondoa TICTS pamoja na utapeli wao?

Awamu hii iliamua kuifanya bandari kuwa lango kuu wa uchumi na wakaamua kutafuta muwekezaji mwenye uzoefu na mwenye hela ya kufanya kazi na DP World wakawa chaguo.

Serikali imeenda mbali zaidi kufanya mambo wazi na kupeleka bungeni kujadili jambo hili, nataka watu wanaopinga DP World waje hapa watuambie lini TICTS na mikataba yao ilijadiliwa bungeni kwa uwazi huu?

Haikuwa hivyo kwa kuwa TICTS walikuwa wanagawa rushwa haswa na Karamagi ndiye alikuwa kinara na viongozi wengi wakiopita walikuwa wanufaika.

Serikali hii imekuwa jasiri kuliko zote na kuwang'oa TICTS kwa sababu walikuwa wanadharau mkataba wao na hakuna kitu cha maana wamefanya na bado walikuwa wanapewa kikataba kihovyo hovyo tu na kwa kugawa rushwa.

Upotoshaji unaofanywa kuhusu DP World ni jambo la hovyo na aibu sana. DP World wanakwenda kuifanya bandari ya Dar Es Salaam kuwa ya kisasa na yenye ufanisi sana kutokana na aina ya uwekezaji na fedha wanakwenda kuweka na kufanya mabadiliko kwenye hii bandari.
 
TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Mh...!!
 
Kwa hiyo walichosema TPA ni uongo?.
 
Vipi mkuu, siku hizi sikuoni kijiwe cha kahawa Uhuru Kariakoo.
 
Hoja zetu watanzania hapa mtandaoni ni nzuri na zenye mashiko , zingepata nguvu kama zingesindikizwa na maandamano kadhaa walao ingeonyesha tupo sirious kidogo.
 
TPA haina uwezo wa kulisemea jambo hili , acheni kujipendekeza , hili msemaji wake ni lazima iwe serikali yenyewe .

Kwanza nyie TPA kila siku mnatimuliwa na wanawekwa watu wapya mnawezaje kuwa wasemaji wa Jambo la Kitaifa ?
Uko sahihi kabisa. TPA jambo hili haliwahusu wao ni robot tu hawana capacity ya kulisemea
 
Back
Top Bottom