Wafanyakazi watakaokataa kujiunga na DP World watapelekwa kufanya kazi bandari nyingine. Je, TPA wamekabidhi bandari yote Dar kwa DPW?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Tangazo la TPA la ufafanuzi linasema wafanyakazi watakaobaki TPA watakwenda kufanya kazi bandari nyingine nje ya DSm. Kwa kauli hii maana yake hakuna mfanyakazi wa TPA atakayebaki bandari ya DSM baada ya DP world kuanza kazi?

Tangazo lao na ufafanuzi uliowakutolewa hapo awali ulionyesha ni baadhi ya gat zitapewa DP World, Leo kwenye taarifa kwa umma hakuna Sehemu uma unaambiwa gat gani itaendelea chini ya TPA badala yake watumishi wote wanaelekezwa kuchagua moja kati ya kwenda TPA mikoani au kubaki na DP World.

Naomba TPA watuambie ni wafanyakazi gani watabaki chini ya TPA wakisimamia bandari ya DSM? Au hadi management inaondoka kwenda kusimamia bandari za mikoa? Nauliza kwa sababu kuna tatizo la wakuu wa idara kuona kama wao siyo waajiriwa, tunafahamu watumishi wote wa TPA ni waajiriwa je mabosi nao wanakwenda kuajiriwa na DP world?

Pia soma Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam
 
Hakuna private sector inaweza kuwa na ufanisi ikikabidhiwa mali za umma, private sector always inachowaza nikuiba iwezavyo itengeneze faida kubwa kabla ya mkataba kuisha

Na hapo kwenye faida kubwa ndipo uzaliwa siasa chafu za uendeshaji, rushwa, ukwepaji kodi nk

Ni lini tumewahi kunufaika na madini? Lakini pamoja na kutonufaika unafahamu watanzania wanavyonyanyasika migodini? Wanabanwa si kwa .aslahi ya nchi, wanabanwa kwa maslahi ya mabeberu.

Same applies to DP world investment, tutegemee watu wetu kuwa watumwa huku RAIA wa kigeni wakiishi kama wafalme. Tutegemee sehemu zote za ukwepaji kodi tukiambiwa hakuna mtanzania anaweza kufanya kazi eneo hili watafanya wageni

Tutegemee mafunzo yatakayotolewa kwa watanzania yasiwe na tija kwao ili waweze kupata uncolified individuals kwa kigezo cha kusaka qualified from abroad

Tanzania tunaua nchi yetu kwa kufikiri misaada na kukabidhi mali za umma kwa wageni . Ipo siku tutashindwa kulipa hata salaries za watumishi kwa sababu vyanzo vyote vimeshikwa na wageni
 
Hakuna private sector inaweza kuwa na ufanisi ikikabidhiwa mali za umma, private sector always inachowaza nikuiba iwezavyo itengeneze faida kubwa kabla ya mkataba kuisha

Na hapo kwenye faida kubwa ndipo uzaliwa siasa chafu za uendeshaji, rushwa, ukwepaji kodi nk

Ni lini tumewahi kunufaika na madini? Lakini pamoja na kutonufaika unafahamu watanzania wanavyonyanyasika migodini? Wanabanwa si kwa .aslahi ya nchi, wanabanwa kwa maslahi ya mabeberu.

Same applies to DP world investment, tutegemee watu wetu kuwa watumwa huku RAIA wa kigeni wakiishi kama wafalme. Tutegemee sehemu zote za ukwepaji kodi tukiambiwa hakuna mtanzania anaweza kufanya kazi eneo hili watafanya wageni

Tutegemee mafunzo yatakayotolewa kwa watanzania yasiwe na tija kwao ili waweze kupata uncolified individuals kwa kigezo cha kusaka qualified from abroad

Tanzania tunaua nchi yetu kwa kufikiri misaada na kukabidhi mali za umma kwa wageni . Ipo siku tutashindwa kulipa hata salaries za watumishi kwa sababu vyanzo vyote vimeshikwa na wageni.
Tumeliona hili kwenye mashirika mengi ya umma yaliyokufa.
 
Back
Top Bottom