MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA imetoa taarifa inayoonyesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Bandari ya Dar es Salaam kwa mwaka jana.
Akiongea mbele ya Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Plasduce Mkeli Mbossa amesema katika kipindi cha Julai hadi Disemba mwaka jana TPA imeweza kuvuka malengo yake kwa kuhudumia meli 979 ambalo ni ongezeko la meli zaidi ya 200 kutoka lengo la awali la meli 792.
Mbossa amesema katika kipindi hcho lengo jingine liliwekwa kuhudumia takriban makasha 500 lakini lengo lilivukwa na kufikia makasha 900 huku tani za mizigo milioni 17.2 kutoka tani milioni 15.6 zilizokusudiwa awali.
Amesema hayo ni mafanikio makubwa ambayo mamlaka imeyafikia hatua hiyo ikiwa imechangiwa na mpango mkubwa wa TPA kuboresha huduma kwenye bandari zote nchini.
Mkurugenzi huyo pia amefafanua kuwa mpango huo ndio umechangia hatua za maboresho ya bandari ya Dar es Salaam na kuweza kuleta mafanikio na sasa meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja na kuongeza wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja kutoka meli 70 kwa mwezi hapo awali.
Kuhusu kampuni ya Dubai, DP WORLD Mbossa amesema Kampuni hiyo itaanza shughuli zake kwenye Bandari ya Dar es Salaam robo ya kwanza ya mwaka ya mwaka huu pale itakapokamilisha taratibu za kisheria.
Mkurugenzi amesema kuna taratibu ambazo hazijakamilika kama vile ukataji wa leseni ya kuendesha Bandari, pamoja na uundwaji wa kampuni ya pamoja kati yake na serikali kama makubaliano yanavyoelekeza.
"Kwahiyo mategemeo yetu ni kwamba tutaanza katika nusu ya mwaka huu wa kifedha taratibu zikikamilika, tutatoa taarifa rasmi ya tarehe ambayo wataanza kazi" Amesema Mbossa
Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app