Mpatanishi
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,810
- 623
Sasa ndugu, kama madaktari wanatakiwa kuwa ''humble and low'', na kwamba wanatakiwa wasichague kazi zenye kipato kikubwa, basi kwa nini usingewashauri waendelee kuwa humble tu katika kazi yao ya udaktari, na wasigome, eti unataka wabadilishe fani na wafanye kazi zingine...huko ndio unataka wawe humble, na wakubali kipato kidogo!!Hahaaaa!!
Huwezi kuwa serious katika hilo.., in that way you have not solved anything.
Mimi nimesikitishwa tu na content ya kauli yao ya kuomba msamaha, haiko mature enough..ni kama wameelekezwa cha kusema, lakini tendo lenyewe kwa jinsi nilivyoona walivyoachwa hewani na wenzao wajanja, wasingeliepuka. Tena naona wamechelewa sana, walitakiwa wafanye hivyo mara tu walipoona wenzao wameshindwa kuwaunga mkono, wangetangaza kusitisha mgomo na wangeomba serikali irudi mezani wajadili wakati wapo kazini.
All in all, tusiwadanganye watu waanze movement yoyote (iwe na haki au la) bila back-up. Kwa nchi yetu ni hatari sana.
Wananchi wenyewe hawakuwa tayari kusapoti madai ya madaktari. Cha kushangaza wale seniors wala hawakujishughulisha kulinda heshima ya fani yao kwa kutoa matamko kulaani chochote katika kile kilichotokea.
Watu wamekaa mtaani miezi 3, wale walioko kazini wanapongezwa kwa uvumilivu wao, nao bila aibu wanasema asante bila kuonesha kwamba sio sahihi wao kufanya kazi bila interns.
.....waacheni tu watu watapetape wanavyoweza na wananchi tujifunze kusaidiana kuishauri serikali itatue matatizo yetu ya msingi.
Tumia akili wewe, wameambiwa wajishushe kwa sasa huku wakisubiri HAKI ipatikane. Kuliko kulamba miguu ya watawala wanaotudhulumu. Utaombaje msamaha kwa madai uliyoyasimamia mwanzo hadi kusababisha vifo? Je leo wanakana madai yao? Sasa why waligoma?