Tamko la Jumuiya ya Madaktari Tanzania

lengo la mwanzo kabisa wakati mgomo unaanza ni kuwaondoa viongozi wa wizara ya afya na walitajwa kwa majina(jitahidi kuwa na kumbukumbu)
mwangosi na mwanahalisi wametajwa kama sehemu au kumbukumbu ya unyama aliofanyiwa ulimboka.

Kuhusu Mwangosi na Mwanahalisi hujajibu swali, swali siyo kwanini wametajwa swali ni time factor, why now? why not yesterday or last week? why not tomorrow or next week? Kwa hiyo jumuiya ya madaktari inaendeshwa na matukio, baada ya interns kulalamika kusalitiwa ndipo wakakumbuka kumpa pole Mwangosi na kuikemea serikali kulifunga Mwanahalisi.
 
Sasa hapo utasema wamekomboa sekta ya afya au wamejikomboa wenyewe? Sio madaktari wote wenye nia na uwezo wa kufundisha, etc...Hapo mi niseme tu...ALL DOCTORS HAVE LOST THIS BATTLE. They needed to be one, strategic, unyielding untill they succeed. Mimi nimeguswa sana na mambo ya madaktari na nimefatilia kwa ukaribu kupitia jamaa zangu, tatizo kubwa nimegundua ni lack of solidarity and poor communication and clear plan kabla hawakuanza mgomo. Walimu walijitahidi sana ki-mkakati, ingawa wao pia walipungukiwa mahali, lakini nakwambia wao walikuwa wako vizuri kuliko madaktari.

siliza hata walimu wapo waliotusaliti wapo walioingia madarasani na kufundisha ila hii haikuturudisha nyuma tuliokua tumeamua Kugoma. Na muda si mrefu goma litaamshwa tena mpaka haki ipatikane.
Suluhisho ni serikali kutatua matatizo ya watumishi. Kuwanunua Interns wachache kuwasaliti wenzao ni Upuuzi tu
 
Kuhusu Mwangosi na Mwanahalisi hujajibu swali, swali siyo kwanini wametajwa swali ni time factor, why now? why not yesterday or last week? why not tomorrow or next week? Kwa hiyo jumuiya ya madaktari inaendeshwa na matukio, baada ya interns kulalamika kusalitiwa ndipo wakakumbuka kumpa pole Mwangosi na kuikemea serikali kulifunga Mwanahalisi.
kwani Tamko lililenga nini?...naamini unajua Tamko halikumlenga mwangosi wala mwanahalisi ,hawa wametajwa kama sehemu ya kumbukumbu au reference!
 
Sasa hapo utasema wamekomboa sekta ya afya au wamejikomboa wenyewe? Sio madaktari wote wenye nia na uwezo wa kufundisha, etc...Hapo mi niseme tu...ALL DOCTORS HAVE LOST THIS BATTLE. They needed to be one, strategic, unyielding untill they succeed. Mimi nimeguswa sana na mambo ya madaktari na nimefatilia kwa ukaribu kupitia jamaa zangu, tatizo kubwa nimegundua ni lack of solidarity and poor communication and clear plan kabla hawakuanza mgomo. Walimu walijitahidi sana ki-mkakati, ingawa wao pia walipungukiwa mahali, lakini nakwambia wao walikuwa wako vizuri kuliko madaktari.


Mkuu mengi uliyosema ni sahihi.

Kuhusu tatizo kubwa lililosabaisha failure ya mgomo ni kukosekana kwa nia njema.

Madaktari ni watu wenye moyo wa uvumilivu wa hali ya juu. Ni watu wenye umakini mkubwa katika kupanga na kutekeleza malengo yao.

Nina uhakika wa aslimia mia moja kuwa madaktari wakiwa na lengo lolote kwa nia njema ni LAZIMA lengo hilo watalitimiza kwa muda walioupanga.

Katika mgomo huu nia njema ilikosekana. Madaktari waliochallenge uhalali na ulazima wa mgomo wakajengewa propaganda za kisiasa ili wasisikilizwe, wale wasio na nia njema wakawa vinara na kuongoza kikundi kidogo kwenda mahali kusikofaa huku wakijipa majina ya uongozi wa the so called jumuiya ya madaktari. Watu hao hawajachaguliwa na madaktari na kimsingi hawakuwa na mandate ya kuwakilisha madaktari.

Lakini kutokana na maarifa na umakini wa madaktari wakagundua kuwa wanakoelekea siko wanakostahili huelekea. Wakarudi kazini kuwahudumia watanzania wenzao.

Swala la interns ni tofauti kidogo kwa sababu mkataba wao sio wa ajira, ndio maana wameishia hapo walipo. Otherwise na wao wangerudi kazini kujenga taifa muda mrefu tu.
 
''serikali haifanyi kazi kwa huruma bali kwa kanuni,taratibu,sheria,miongozo na ubabe'
nashukuru madaktari kwa kutambua hili.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
wewe ndiye mwoga na msaliti namba moja!kwa nini hutaki kuona sekta ya afya nchini ikiboreka?kwa nini usitumie elimu yako kuishauri serikali badala yake unafanya propaganda kurudisha nyuma juhudi za madaktari wenzako?mpango mlioandaa umeshindwa na sasa una backfire!stay tuned!mmelianzisha wenyewe!


Na hakika kumekuchaaaaaaa! Watajua mbivu na mbichi!
 
Mkuu Maundumula, kwani wakitoa POLE na kuonyesha kuguswa kuhusu hayo kuna shida, mbona Mh. Rais anatoa pole na kutuma salamu za rambi rambi nje lakini ndani ya nchi yake mwenyewe anashindwa kutoa pole??!

Sasa si kila kitu lazima tumuige Mh.Rais, kama yeye alishindwa au hakuguswa kabisa, wapo watanzania wanaoguswa katika haya..Je, ubaya katika hili uko wapi mkuu?

Mkubwa,

Hawa jamaa ni madaktari tunategemea wawe kitaaluma zaidi na wawe wana uwezo wa kupima mambo. Kushabikia maswala ya kisiasa ndio kunasababisha wanakuwa na mgawanyiko. Wewe fuatilia migomo kwenye nchi za wenzetu ndio utajua kuwa hawa wanachemka. Ishu kama za kufungiwa kwa Mwanahalisi na maswala ya Mwangosi ni very very irrelevant na mahitaji yao,hayo wangewaachia Chadema . Wanasema wanaamini waliotajwa na Mwanahalisi ndio wahusika wakati huo huo Dr Ulimboka ameshasema ukweli anaujua yeye mwenyewe tu!

Hawa madaktari wamekuwa kama watoto wa shule ya msingi yani hata hawajui nini wanafanya na nini wanataka!
 
Mkuu Maundumula,

Katika KAMATI ya madaktari(iliyotoa tamko jana) bado Dr. Ulimboka ni mwenyekiti wake, ila hawezi kurejea kuwa hadharani kwa ajili ya afya na usalama..hili la kwanza.

Pili, iwapo katika tamko walilolitoa wasingeongelea jambo la msingi(kilichojiri siku moja kabla ya kutoa tamko) yaani trh 17.09.2012..kweli wangekuwa wanasiasa, lakini kwa mtazamo wangu BINAFSI sijaona ubaya katika;

1.Kutoa pole na salamu za rambirambi. (KAMA BINADAMU)

2.Kutambua hali iliyopo nchini( KAMA WATANZANIA PIA)

Sijaelewa mwishoni unaposema hujui ni nini wanataka, kwa sababu(kwa mtazamo wangu again) nilivyowaelewa ni kuweka clarification ya mambo kama:

1. Si intern doctors wote walioomba msamaha.
2. Hakuna kurubuniwa au kushawishiwa kuliko tumika.
3. Shutuma dhidi ya chama chao cha kitaaluma si za kweli.
4. Madai ni ya msingi(na hata kama hayatatekelezwa haimaaniashi inapunguza UMUHIMU wake.

Au wewe ulielewaje Mkuu.
 
Nlipotazama tbc nkaona yule intern yuko peke yake akiwaombea msamaha ma dr wote ambao kwa kawaida uwa ni umati pindi wanapokutana kutoa tamko. Nikajua tu dogo kashaahidiwa vinono akahaharibu. Dogo Tahaira anakiri kusababisha vifo kwa wagonjwa alaf kova anakaa na kuchekelea...ivi anayekiri kuua sheria inamsamehe?mbona dogo hadi dakika hii hajakamatwa kwa kukiri kuua wagonjwa?je madai yao kumbe yalikuwa hewa?je kama yalikuwepo yametekelezwa-?je kama uligoma upewe haki,ushapewa unaenda kuomba msamaha?uyu intern ni tahaira!
 
Sijui kwanini mnabishana na mtu kama huyu! mwachieni ***** wake otherwise anaelekea kufanikiwa kuhamisha attention ya mjadala! Madaktari jadilini mustakabari wenu msitolewe povu na wasaliti wachache kama hawa!
 
Baada ya ile "radhi" ya wale wasaliti hii ndio nilikuwa naisubiria.............................nimeona kitu wengi tunadhani hili ni tukio kumbe ni mchakato Jumuiya ya Madaktari wamesema vyema
 
Mimi nilikuwa nasubiri kusikia kauli ya MAT ama jumuiya ya madaktari iliyokuwa chini ya Dr. Ulimboka.
Usaliti umekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida ya mtanzania. Madaktari wameasalitiana kama waandishi wa habari wanavyosalitiana juu ya kifo cha mwenzao marehemu Daudi Mwangosi. Walikubaliana kwamba wasiripoti habari za polisi walau kwa siku hizi arobaini lakini wapi kesho yake tu wengine wakaanza kutiririka na kauli za marpc.

Njaa kali, chezea tanzania wewe!
 
Mkuu mengi uliyosema ni sahihi.

Kuhusu tatizo kubwa lililosabaisha failure ya mgomo ni kukosekana kwa nia njema.

Madaktari ni watu wenye moyo wa uvumilivu wa hali ya juu. Ni watu wenye umakini mkubwa katika kupanga na kutekeleza malengo yao.

Nina uhakika wa aslimia mia moja kuwa madaktari wakiwa na lengo lolote kwa nia njema ni LAZIMA lengo hilo watalitimiza kwa muda walioupanga.

Katika mgomo huu nia njema ilikosekana. Madaktari waliochallenge uhalali na ulazima wa mgomo wakajengewa propaganda za kisiasa ili wasisikilizwe, wale wasio na nia njema wakawa vinara na kuongoza kikundi kidogo kwenda mahali kusikofaa huku wakijipa majina ya uongozi wa the so called jumuiya ya madaktari. Watu hao hawajachaguliwa na madaktari na kimsingi hawakuwa na mandate ya kuwakilisha madaktari.

Lakini kutokana na maarifa na umakini wa madaktari wakagundua kuwa wanakoelekea siko wanakostahili huelekea. Wakarudi kazini kuwahudumia watanzania wenzao.

Swala la interns ni tofauti kidogo kwa sababu mkataba wao sio wa ajira, ndio maana wameishia hapo walipo. Otherwise na wao wangerudi kazini kujenga taifa muda mrefu tu.

Kuna ukweli asilimia fulani katika ulichosema,labda zaidi mimi niliona viongozi wao kuna wakati walipepesuliwa na upepo wa kisiasa ingawa nadhani sababu ya kugoma walikuwa nayo.Ila viongozi wao walikuwa hasty kufanya maamuzi bila kuweka mazingira salama kwanza kwa wanachama wao. Nao pia kuna wakati hatukuwasikia kabisa wakitoa matamko mbalimbali walau kuonesha umma kwamba mgomo bado upo na hali bado si shwari mahospitalini. So ukimya ule ulifanya watu waanze kusahau mambo ya madaktari, hata Dr. Ulimboka alivyorudi, ukimya wake pia umepunguza nguvu ya mapambano kwa wale waliohitaji kuwa motivated.
......
Hapo penye rangi nyekundu, mi nadhani ilikuwa ni ONE OF THE SUCCESSFUL GAME the govt played. Divide and Rule. It is said they knew if they sacked the interns the doctors will divide knowing that in every community kuna watu tofauti...kuna waoga, wasio na misimamo, wanaoshika dini, etc. Wakajua watatatofautiana tu. Kwa hiyo kuna kundi litabaki kazini tu. Wengi walioajiriwa hawakuchukuliwa hatua kwa makusudi ili kwanza waone serikali iko serious, nao pia wakaingia mtegoni, wakatulia makazini, wakajaza vitabu vya mahudhurio, wakawa salama, wakajikomboa nafsi zao(nani alisema intelijensia ya nchi ni mbovu?..cheza na TISS wewe!!).
....
All in all, madaktari wameshashindwa hii movement (ingawa kurudi kuwasaidia wagonjwa sio failure...ni nia njema na busara). Lakini cha msingi ni kujua tu kwamba next time WAKIWA NA MSUKUMO WA NIA NJEMA, wajaribu kufata taratibu zote za kisheria wakati wanadai, kugoma iwe hatua ya mwisho. Mimi pia naamini serikali itafikia mahali itawapa stahili yao tu.
....
Serikali nayo inapaswa kuacha kutumia mbinu za kuzima movement tu badala ya kujaribu kusolve yale yanayodaiwa kwa nia njema pia.Ili watu wajivunie nchi yao na serikali yao.
Kwani itapata hasara gani ikijaribu kujenga mazingira bora kwa wafanyakazi wake?
 
Wale walioomba msamaa njaa ilikuwa inauma ndio maana ilikuwa taabu hata kujieleza!!!!!!!!!!!!!!
 
Wewe unaongea kwa urahisi sana, wenzako wale wa jana hawana kazi, unajua huu ni mwezi wa ngapi? Wengi wao wamekuje mjini kwa sababu ya Chuo na wengi walikuwa pale MNH. Nani anawpa pesa ya kujikim? ni MAT au Jumuiya ya Madaktrai? Ni rahisi kusema hivyo kwa kuwa wewe unakula mshahara wako mwisho wa mwezi! Wenzako wananjaa! Wafanyeje? Na wengine kumbuka walikuwa wameanza kutegemewa. Mkakati walishaukosea Madaktari toka mwanzo, kwani walitakiwa wote kwa pamoja, Interns, REgistrars, Residents na Ma Chief wote wakaze buti. Hali ilipofikia ya kuwatoa kafara Interns ni upuuzi tu. Kumbuka, mwisho wa siku kila mtu anatafuta maisha yake na familia yake!
Wewe kukaa miezi miwili ndo imekuwa nongwa? Kuhusu Registrars Mbeya wapo Registrars waliosimamishwa, Residents wapo waliolimwa barua za Onyo na wakuu wa idara hapo MUHAS ila wasingeweza kuwafukuza kwa sababu wao ni wanafunzi wa MUHAS si MNH. Specialists walishiriki mgomo huo kikamilifu na si haki kuwabeza kirahisi hivyo! tukubali tu kuwa serikali ilitumia nguvu kubwa kuuzima huu mgomo. Kitendo cha Intens wachache kuomba radhi hakikuwa sahihi kwani kada nyingine za madaktari hata baadhi ya interns hawakushirikishwa.

Cha Muhimu hawa wasaliti waombe radhi kwa madaktari wengine na kujipanga kwa next episode ya mgomo. Kwani pamoja na kuomba radhi CMO ameshatoa kauli kuwa taratibu za kisheria zitafuatwa na hivyo kila aliyeomba radhi amerahisisha kazi ya hakimu!!!!
 
Kamati ya Jumuiya ya Madaktari Nchini, kwanza inapenda kutoa pole kwa Wanahabari wote nchini kwa kitendo cha kinyama ambacho Mwanaharakati na Mwandishi wa habari, Marehemu David Mwangosi alifanyiwa, hii ni ishara kuwa Jeshi la Polisi wameamua kutumia njia ya kuua raia ili kujenga hofu na woga miongoni mwa wapenda demokrasia na maendeleo nchini.
Pia tunapenda kulaani kitendo cha Serikali kupitia Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni kulifungia gezeti makini la Mwanahalisi kwa sababu ya kutoa taarifa za ukweli juu ya waliotaka kukatiza uhai wa Dr.Ulimboka Stephen, Jamii ya Madaktari na watanzania wengi bado wanaamini kuwa waliotajwa na gazeti la Mwanahalisi ni miongoni mwa waliohusika na kutekwa, kuteswa na kutelekezwa kwake na si yule anayesemekana kuwa na matatizo ya akili aliyedaiwa kukamatwa na Suleimani Kova. Hivyo tunalitaka Jeshi la Polisi litoe ripoti yake ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa taarifa hii.
Pia, tunachukua nafasi hii kupongeza mshikamano ambao Madaktari wameendelea kuuonyesha licha ya changamoto nyingi tunazopitia, ni vema ikafaamika kuwa ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa MAT na MAT imefunguliwa kesi 2 mahakamani, Ni katika kipindi hiki ambacho zaidi ya interns 300 wanasubiri kuitwa kuhojiwa na MCT bila kujua ni lini hilo litafanyika, Ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari anapata mapumziko baada ya kutoka katika Matibabu nchini Afrika Kusini, lakini ni katika kipindi hiki ambacho mpaka sasa hakuna hata hoja moja ya Madaktari imefanyiwa kazi na Serikali.
Tunapenda ieleweke kuwa suala la madai ya Madaktari si tukio, ni mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ndio maana tumeshuhudia migomo hii katika nyakati tofauti pamoja na kujitokeza kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini na maslai ya watumishi kwa ujumla.
Kuhusu suala la interns, Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 10, Julai 2012, Baraza la Madaktari Nchini lilitoa taarifa kwa umma kuwa imesitisha leseni za muda kwa Madaktari waliochini ya mafunzo kwa vitendo, pia waliahidi kuwaita kwa nia ya kuwahoji mmoja mmoja pindi wakatapokamilisha uchunguzi wao, cha kushangaza ni kwamba miezi 2 sasa imepita bila hilo kufanyika.
Katika vikao mbalimbali ambavyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, na Kaimu Katibu Mkuu wameshiriki, wamekuwa wakisisitiza kuwa hili lipo kisheria na interns wasuburi kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa. Hivyo tunapenda kutumia nafasi hii kuitaka MCT itekeleze kwa haraka majukumu yake kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa haki.
Hivyo basi Kamati ya Jumuiya ya Madaktari imejiandaa vya kutosha na taratibu za kisheria na itahakikisha inaweka wakili pale interns watakapoanza kuhojiwa kwa kuwa sheria inayounda MCT inatoa hiyo nafasi.
Mwisho kabisa tunapenda kutoa wito kwa interns kutumia hekima na busara katika kipindi hiki kigumu, waepuke kutumiwa na kikundi cha watu ambao wanatumika au wanajitumia kwa maslai ya kustarehesha watawala.


IMETOLEWA NA; KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA-BARA.
 
Mkuu bagwell,hii si bi taarifa ya jana, then ukweli huo uko wapi,yaani (content ya thread yako ambayo itaendana na thread title)?
 
Back
Top Bottom