Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 987
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Baraza la Madaktari Tanzania (MCT) ambalo kimsingi ndilo lenye mamlaka ya kisheria katika kusimamia taaluma ya Utabibu nchini linalalamikiwa na Wanataaluma wa tiba hasa madaktari tarajali kwa kukiuka makubaliono yaliyotokana na majadiliano ya kikao kati ya wataalam hao tarajali pamoja na Naibu waziri wa Afya Dr Godwin Moleli akimwakilisha Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu aliyefunga mjadala kwa kuunda tume ya kiuchunguzi juu ya malalamiko yao.
Wanauliza ni kwanini MCT wametangaza tarehe ya kufanya mtihani wa Pre-Internships mwaka huu wakati kamati ya Mhe Waziri bado haijatoa ripoti yake? Mwenye uhakika na usalama wa huo mtihani ni nani haliyakua watuhumiwa wanachunguzwa? Siyo ukaidi ni nini?
Ni takribani zaidi ya Mwezi mmoja kupita baada ya Mhe Waziri kutoa taarifa kuundwa kwa tume ya kitaalam itakayochunguza ni kwanini Wataalam hao wamekua wakifeli mitihani zaidi ya nusu ya watahiniwa wote? Hata kabla Kamati au Tume ya Mhe Waziri haijatoa Ripoti yake imekuaje MCT wanatangaza mtihani? Yaani wanachunguzwa halafu wanaendelea kufanya kile kile nicholalamikiwa, hii ni sawa?
OMBI/USHAURI KWA MHE WAZIRI
MCT wasitishe kwanza kusajili watahiniwa kwa ajili ya mtihani ambao watungaji wake wametiliwa mashaka.
Kitu kiingine ni kwamba. Hakuna mantiki au hoja yenye mashiko kwenye kufanya mtihani wa Preinternship wakati kuna mtihani wa Postinternship, kwenye preinternship wanapima kitu gani hasa wakati wanafunzi hawa wamekaa darasani miaka 5 na wakafaulu katika vyuo walikotoka? Kama vyuo vingekuwa na walakini TCU wana kazi gani?
Mhe Waziri ulisema kwamba watakaofanya mitihani ya Preintetnships wataendelea na kazi mahospitalini haijalishi wamefeli au wamefaulu, hii maana yake nini? Nini mantiki,tija na umuhimu wa Preinternship zaidi ya siasa na kikundi cha watu wachache kujitengenezea posho kutoka pesa za umma ambazo zingefanya mambo mengine?
Hivyo basi, Mhe Waziri kwa niaba ya Watoa elimu ya utabibu nchini nikiwa kama mwalimu wa vijana hawa, sioni kama Baraza likiwatendea haki, tutapoteza wataalam wengi bila sababu za msingi. Tuige mifano toka kwenye mataifa ya wenzetu.
MCT wasitishe mara moja usajili wa watahiniwa wa mtihani wa preinternship mpaka tume yako itakapokuja na majibu Mhe Waziri.
KAZI IENDELEE!
===================================
PIA SOMA:
UPDATE: Wizara ya Afya yaunda Kamati kuchunguza Malalamiko ya Madaktari Watarajali
Madaktari watarajali wamekuwa ombaomba Mtaani kisa leseni, wamuangukia Waziri Ummy Mwalimu na Rais Samia
Sina imani na Kamati Huru iliyoundwa na Ummy Mwalimu kufuatilia sakata la Madaktari Watarajali