Malalamiko ya Madaktari Watarajali (Interns) kuhusu kufeli mitihani ya MCT

helu

Member
Feb 28, 2015
86
124
Malalamiko ya Madaktari Watarajali (Interns) kuhusu kufeli mitihani ya Mct:

Kama Mdau wa Afya, nimeisoma barua ya wazi ya madaktari tarajali (interns) ya tarehe 21 July.

Nimesikializa press ya madaktari hao ya tarehe 04 August.

Lakini pia nimeona taarifa kwa umma ya Wizara ya Afya ya tarehe 14 August.

Kila mmoja kati yao angalau wameeleza lau kwa muhtasari kadhia hii kwa namna tofauti.

Kuna maswali kadhaa yanatafakarisha na Mct, Wizara, na wadau wa Afya, ingefaa watafakari na kujiuliza maswali angalau kwa uchache:

Hoja kuu ambayo kila mtu anapaswa kujiuliza ni kwa vipi utaratibu huu wa "pre and post internship Examinations" umependekezwa mwaka 2017, na kuanza kutekelezwa rasmi mwaka 2000, kati kati ya awamu ya tano, awamu ambayo haikutoa ajira ispokuwa chache sana kwa watoto wa Watafuna nchi. Hapa ndipo chanzo na mzizi wa fitna yote ilipoanzia.

Maprofessa wa Mct, ambao wao wenyewe hawakufanya mitihani hii, hawataki kutafakari hata kwa dakika na kujiuliza kwamfano:

Internship ni nini?

Nini maana yake?

Lengo na madhumuni ya internship hasa ni nini?

Ni kwanini utaratibu huu ambao huendeshwa so unfair and free wa "pre and post internship Examinations" upo Tanzania tu, na haupo mahali pengine?

Kada za afya zipo nyingi sana, mfano nurses, physios, xrays, nk. Ni kwanini kada nyingine za afya hazifanyishwi mitihani hii ispokuwa ni kwa junior doctors tu peke yao?

Ni kwanini madaktari wa Masters of Medicine na PhD hawafanyiwi Pre and post internship Examinations, au ukipenda "pre and post residence Examinations" kwa hoja zile zile za ubora na uwezo kama zilivyoelezwa na Msajilili wa Mct?

Ni kwa nini taaluma nyingine hapa nchini hazifanyiwi mambo haya ya Pre and post internship Examinations?

Itapendeza kama tutaona madaktari wote bila kujali vyeo vyao, na kada zote nyingine wakifanya mtihani. Ukifaulu ulipie leseni na ndipo uweze ku practice. Hii ndio haki, na sio kulenga kundi moja tu linalozuiliwa lisiingie kwenye soko au ajira.

Iwapo daktari tarajali kwa bahati mbaya hakufaulu mitihani hii ya masaa mawili ya Mct, ambayo haiko huru na imekosa haki, Jee hivi vyeti vilivyotolewa kwenye hivyo Vyuo Vikuu, vilivyo kaa na mwanafunzi huyu kwa miaka mitano, hatma yake ni nini? Ni Null and void?

Na hivyo vyuo vilivyotoa hivyo vyeti mna viweka wapi? Walimu waliofundisha na mabingwa walio simamia Internship, wao wapo kwenye nafasi gani?

Mnamueka wapi Mzazi wa kijana huyu, aliyejinyima, akapigana jihadi kwa hali na mali, kwa zaidi ya miaka mitano kuhakikisha anatimiza ndoto ya kijana wake?

Mnampa ujumbe gani kijana ambaye ana ndoto ya kuwa daktari?

Na mzo wa mambo na maswali yenye kuchagiza.

Baada ya tafakuri hii fupi, sasa naomba niwaeleze kuwa mzizi wa fitna wa jambo hili ulianzia katika serikali ya awamu ya tano ya Mwendazake. Serikali hii pamoja na mambo mengine ilikataa, ilishindwa, au tuseme ilikuwa na sera ya kuto kutoa ajira kwa madaktari na vijana wengine walio hitimu vyuoni. Hapa ndipo lilipo tengenezwa bomu ambalo likingoja kuripuka.

Madaktari waliendelea kuzaliswa kila mwaka na mpaka leo wanahitimu kila mwaka, lakini Serikali imeshindwa kutoa ajira.

Matokeo yake madaktari vijana waliendelea kulundikana mtaani na Serikali ikawa haina utatuzi wa mlundikano huu.

Mwisho wa kufikiri kwao wakakubalina kati kati ya mwaka 2017 kuwa, kupambana na wimbi hili la madaktari walio mtaani, mzigo huu wabebeshwe Mct kama mbinu ya "ku shift blame".

Walikubalina kuwa ni afadhali ilaumiwe Mct kuliko serikali.

Na kama tujuavyo udhaifu wa idara zetu, Mct walipo rushiwa ndoo hii ya uchafu na kuidaka, wakaridhia wachafuke bora tu wailinde serikali iliyo kosa mbinu za kutengeneza ajira kwa vijana wake wanaotaka vyuoni. Maprofessa wa Mct nao kwa upande wao wakabuni mbinu ya kupunguza idadi ya kusajili madaktari wanao zalishwa kwa kuanzisha (introduce) pre and post internship Examinations ili lawama zielekezwe kwamba vijana hawana ubora na wanafeli mitihani, (shift of blame).

Na mara tu baada ndoa hii ya Mct na serikali, kuanzia hapo Mct, ikabeba ajenda hiyo ya kukwamisha ndoto za junior doctors kama kwamba wao Mct kazi yao ni kusimamia mitihani tu ya pre and post internship.

Ni kwa nini Mct msianzishe vyuo vyenu mkafundisha nyinyi wenyewe ili mtoe madaktari nyinyi wenyewe kama vyuo vinavyofundisha havitoshi na kama iwapo wanaosimamia internship hawatoshi?

Mitihani ya masaa mawili ya Mct imejichukulia kura ya turufu kuliko assessment za miaka zaidi ya mitano pamoja na internship.

"Doctor per capita" ya nchi, ni idadi ya madaktari kwa kila watu elfu moja kwa mujibu wa WHO.

Mwaka 2022, Cuba iliongoza dunia kwa kuwa na Doctor per capita kubwa ya 84.30 ikifatiwa na Sweden.

Tz ilikuwa na 0.5 ya Doctor per capita, ikiwa ni ya tatu kutoka chini mkiani, ikiwa imezipiku Somalia na South Sudan.

Kamati iliyojaa Maprofessa imechaguliwa na Waziri wa Afya inalichunguza jambo hili ili itoe mapendekezo yake kwa Waziri. Lakini itashangaza iwapo mpiga zumari anaweza kuwa na ubavu wa kuimba wimbo ambao hauku chaguliwa na aliyelipia zumari.

Kamati hii inafanana na tume zetu za uchaguzi.

Tz imejaaliwa kila kitu. Ipo hapa ilipo kutokana na ubinafsi wa viongozi na kukosa maono (vision). Lakini pia aina ya Maprofessa wa nchi hii, wamechangia kuididimiza na kuipeleka shimoni nchi.

Siasa katika nchi hii imeingizwa na imetamalaki katika kila kitu.

Uzoefu umeonyesha kuwa wenye jukumu la kufungua njia na kuleta ustawi wanaishi katika majigambo ya kujivunia enzi na Uwao.

Tanzania inahitaji ukombozi wa kiroho.
 
Acheni Ujinga ,
Fanyeni mitihani mfaulu...

Hili la kitakankujipangia utaratibu wa kufauli limeanza Lawa School sasa na ninyi mnalileta.

Hatutaki watabibu vilaza huku mitaani.
 
Kada zote zinazohitaji leseni ni lazima kufanya mtihani mbona pharmacy wanafanya mtihan mbona medical laboratory wanafanya mtihani nurses walianza pia mitihani wanasheria wanafanya mitihan Wale CPA wanafanya mtihani madakitari tunapendekeza wafanye mitihani tena iwe migumu hasa hatutaki vilaza waje kututibu
 
Muhimu kujua ni je viwango vya kimataifa kwa taaluma husika vinatambua huo utaratibu?, kama jibu ni hapana ndio tujiulize sisi tumeutoa wapi na kwa maslahi gani?.

Short of that, wakuu komaeni na kitabu
 
Íla ni kua makini sana, incompetent doctors wapo wengi sana,nadhani wanapitapita tu,matokeo yake wanakuja kudakwa na MCT.Pigeni kitabu,ili msituue hovyo.
 
Malalamiko ya Madaktari Watarajali (Interns) kuhusu kufeli mitihani ya Mct:

Kama Mdau wa Afya, nimeisoma barua ya wazi ya madaktari tarajali (interns) ya tarehe 21 July.
Nimesikializa press ya madaktari hao ya tarehe 04 August.
Lakini pia nimeona taarifa kwa umma ya Wizara ya Afya ya tarehe 14 August.
Kila mmoja kati yao angalau wameeleza lau kwa muhtasari kadhia hii kwa namna tofauti.

Kuna maswali kadhaa yanatafakarisha na Mct, Wizara, na wadau wa Afya, ingefaa watafakari na kujiuliza maswali angalau kwa uchache:

Hoja kuu ambayo kila mtu anapaswa kujiuliza ni kwa vipi utaratibu huu wa "pre and post internship Examinations" umependekezwa mwaka 2017, na kuanza kutekelezwa rasmi mwaka 2000, kati kati ya awamu ya tano, awamu ambayo haikutoa ajira ispokuwa chache sana kwa watoto wa Watafuna nchi. Hapa ndipo chanzo na mzizi wa fitna yote ilipoanzia.

Maprofessa wa Mct, ambao wao wenyewe hawakufanya mitihani hii, hawataki kutafakari hata kwa dakika na kujiuliza kwamfano:
Internship ni nini?
Nini maana yake?
Lengo na madhumuni ya internship hasa ni nini?

Ni kwanini utaratibu huu ambao huendeshwa so unfair and free wa "pre and post internship Examinations" upo Tanzania tu, na haupo mahali pengine?

Kada za afya zipo nyingi sana, mfano nurses, physios, xrays, nk. Ni kwanini kada nyingine za afya hazifanyishwi mitihani hii ispokuwa ni kwa junior doctors tu peke yao?

Ni kwanini madaktari wa Masters of Medicine na PhD hawafanyiwi Pre and post internship Examinations, au ukipenda "pre and post residence Examinations" kwa hoja zile zile za ubora na uwezo kama zilivyoelezwa na Msajilili wa Mct?

Ni kwa nini taaluma nyingine hapa nchini hazifanyiwi mambo haya ya Pre and post internship Examinations?

Itapendeza kama tutaona madaktari wote bila kujali vyeo vyao, na kada zote nyingine wakifanya mtihani. Ukifaulu ulipie leseni na ndipo uweze ku practice. Hii ndio haki, na sio kulenga kundi moja tu linalozuiliwa lisiingie kwenye soko au ajira.

Iwapo daktari tarajali kwa bahati mbaya hakufaulu mitihani hii ya masaa mawili ya Mct, ambayo haiko huru na imekosa haki, Jee hivi vyeti vilivyotolewa kwenye hivyo Vyuo Vikuu, vilivyo kaa na mwanafunzi huyu kwa miaka mitano, hatma yake ni nini? Ni Null and void?
Na hivyo vyuo vilivyotoa hivyo vyeti mna viweka wapi? Walimu waliofundisha na mabingwa walio simamia Internship, wao wapo kwenye nafasi gani?

Mnamueka wapi Mzazi wa kijana huyu, aliyejinyima, akapigana jihadi kwa hali na mali, kwa zaidi ya miaka mitano kuhakikisha anatimiza ndoto ya kijana wake?
Mnampa ujumbe gani kijana ambaye ana ndoto ya kuwa daktari?
Na mzo wa mambo na maswali yenye kuchagiza.

Baada ya tafakuri hii fupi, sasa naomba niwaeleze kuwa mzizi wa fitna wa jambo hili ulianzia katika serikali ya awamu ya tano ya Mwendazake. Serikali hii pamoja na mambo mengine ilikataa, ilishindwa, au tuseme ilikuwa na sera ya kuto kutoa ajira kwa madaktari na vijana wengine walio hitimu vyuoni. Hapa ndipo lilipo tengenezwa bomu ambalo likingoja kuripuka.

Madaktari waliendelea kuzaliswa kila mwaka na mpaka leo wanahitimu kila mwaka, lakini Serikali imeshindwa kutoa ajira.
Matokeo yake madaktari vijana waliendelea kulundikana mtaani na Serikali ikawa haina utatuzi wa mlundikano huu.

Mwisho wa kufikiri kwao wakakubalina kati kati ya mwaka 2017 kuwa,
kupambana na wimbi hili la madaktari walio mtaani, mzigo huu wabebeshwe Mct kama mbinu ya "ku shift blame".
Walikubalina kuwa ni afadhali ilaumiwe Mct kuliko serikali.

Na kama tujuavyo udhaifu wa idara zetu, Mct walipo rushiwa ndoo hii ya uchafu na kuidaka, wakaridhia wachafuke bora tu wailinde serikali iliyo kosa mbinu za kutengeneza ajira kwa vijana wake wanaotaka vyuoni. Maprofessa wa Mct nao kwa upande wao wakabuni mbinu ya kupunguza idadi ya kusajili madaktari wanao zalishwa kwa kuanzisha (introduce) pre and post internship Examinations ili lawama zielekezwe kwamba vijana hawana ubora na wanafeli mitihani, (shift of blame).

Na mara tu baada ndoa hii ya Mct na serikali, kuanzia hapo Mct, ikabeba ajenda hiyo ya kukwamisha ndoto za junior doctors kama kwamba wao Mct kazi yao ni kusimamia mitihani tu ya pre and post internship.

Ni kwa nini Mct msianzishe vyuo vyenu mkafundisha nyinyi wenyewe ili mtoe madaktari nyinyi wenyewe kama vyuo vinavyofundisha havitoshi na kama iwapo wanaosimamia internship hawatoshi?
Mitihani ya masaa mawili ya Mct imejichukulia kura ya turufu kuliko assessment za miaka zaidi ya mitano pamoja na internship.

"Doctor per capita" ya nchi, ni idadi ya madaktari kwa kila watu elfu moja kwa mujibu wa WHO.
Mwaka 2022, Cuba iliongoza dunia kwa kuwa na Doctor per capita kubwa ya 84.30 ikifatiwa na Sweden.
Tz ilikuwa na 0.5 ya Doctor per capita, ikiwa ni ya tatu kutoka chini mkiani, ikiwa imezipiku Somalia na South Sudan.

Kamati iliyojaa Maprofessa imechaguliwa na Waziri wa Afya inalichunguza jambo hili ili itoe mapendekezo yake kwa Waziri. Lakini itashangaza iwapo mpiga zumari anaweza kuwa na ubavu wa kuimba wimbo ambao hauku chaguliwa na aliyelipia zumari.
Kamati hii inafanana na tume zetu za uchaguzi.

Tz imejaaliwa kila kitu. Ipo hapa ilipo kutokana na ubinafsi wa viongozi na kukosa maono (vision). Lakini pia aina ya Maprofessa wa nchi hii, wamechangia kuididimiza na kuipeleka shimoni nchi.
Siasa katika nchi hii imeingizwa na imetamalaki katika kila kitu.
Uzoefu umeonyesha kuwa wenye jukumu la kufungua njia na kuleta ustawi wanaishi katika majigambo ya kujivunia enzi na Uwao.
Tz inahitaji ukombozi wa kiroho.
Huwa ni mgum sana sifia mkuu, ila kwa andiko lako hili chukua maua yako kaka, wapumbavu hawawezi kukuelewa ila umeongea fact, na kwa hoja ya mwendazake ulivyo iweka nakubali maana ni kipindi ambacho pia vyuo vingi vikiwemo vya afya vilifungwa bila kujua ,waliosoma vyuo hivyo ndo kila siku wanatupima tezi dume, na kutatua changamoto Zetu ,

Wapeni watoto wa wa watu lesen , wajitafutie ridhiki kupitia njia zingine hata kama ni ajira binafsi ,

Mwisho kama kweli aya mamitiani yana impact mbona mbona wale nyuma ya elfu mbili na 17(2017) wapo na wanaendelea na kazi? Umwinyi tu, na uchawi tu ,
 
Back
Top Bottom