| ||
|
Sema yote kuhusu Shibuda lakini usimnyang'anye haki yake ya kuwa na influence hko kwao. CDM imebebwa na Shibuda huko Shinyanga na wasipo tumia busara safari ya kuelekea kwa NCCR ya kina Mrema na Marando.
Kwa mawazo haya...wewe unatofauti gani na Shibuda? Naweza sema heri ya Shibuda kuliko wewe.Mfukuzeni muone! anamaono ya mbali sana. Hawezi kufungwa na minyororo ya ukabila. Nyinyi watu (hasa vijana) wa Mwanza, Shinyanga, Tabora, Mara na Rukwa, hebu jaribuni kuwa neutral (mawazo huru) mchambue hivi kweli cdm ni chama cha wanyonge wa nchi hii au mnatumiwa na hao wanaotaka kujitenga na kutangaza jamhuri yao. Ole wao wavivu wa kufikiri, watapiginia hata kitakachowaangamiza.
Kama kuna kosa kubwa na la kiufundi CDM wanaweza kufanya ni kumfukuza Shibuda. Huwezi kuwa na wanachama wote wenye mawazo sawa kwenye chama chochote kile cha siasa duniani. Hata USA Republicans yupo Senetor wa Maine Susan Collins na mwenzake Olympia Snowe wanajulikana kama the most liberals in the party. Wamekuwa kikwazo kikubwa kwa chama chao kila inapofikia wakati wa kupiga kura za kuzuia fillibusters. Wameisaidia sana Democrats kwenye hizo kura. Lakini hata siku moja hawajatishiwa kufukuzwa chama.
Kama CDM wanataka kila mwanachama na kiongozi asiwe na mawazo tofauti, hata kama yanaonekana ni ya ukichaa, basi hilo ni tatizo kubwa kidemokrasia. Si busara kuwaandama kina Zitto na sasa Shibuda kwa kutofautiana na viongozi wao.
Shibuda simuungi mkono hata kidogo, lakini ni muhimu ashughulikiwe kwa hoja tu na sio vitisho vya kufukuzwa chama. Na hata kama ikibidi kumuondoa basi democrasia ichukue mkondo wake. Wasubiri harakati zijazo za kugombea ubunge wampambanishe na mwanachama mwingine wawapigie kura na atakayeshindwa ampishe mwenzake. Ndio machungu ya democrasia hayo.
CDM inatakiwa kuwa kinara wa demokrasia TZ na kuonyesha wana CCM kwamba CDM ina uwezo zaidi yao katika kuenzi na ku-practice democracy. Otherwise naanza kuogopa! Seriously!
US Mbunge ni mali ya constintuent. Unaweza hama chama na ubunge wako. au ukaamua kutokuwa mwanachama wa chama chochote.
Sijasema kufukuzwa ubunge. Nimesema kufukuzwa chama!
Hapana hili lingekuwa sahihi endapo CDM ingeweza kufahamu kama itafika naye salama hiyo 2015. Anavyoelekea anazidi kuwa tatizo kwa CDM. Ninahakika hana nafasi kubwa ya kufahamu mambo ya ndani ya CDM, je akifahamu mikakati yote na wakati ambapo ni sensitive, anaweza sababisha matatizo makubwa. Huyu ni kupe, huwezi kaa na kupe mwilini ukingoja afe adondoke. Atakutia kichaaa!Sioni sababu ya CDM kulumbana na huyu jamaa because he is politically dead. Hana influence yeyote kwenye jamii hata katika jimbo lake la Maswa. Wamwache tu abwabwaje, baadae wanaMaswa watamwonyesha njia ya kutokea 2015. Endapo CDM wakianzisha malumbano yeyote na Shibuda kwa sasa, sanasana watampaisha katika vyombo vya habari, na anaweza kujenga influence. Wamwache tu maana hata CCM wanajua yule kwa ni insane...