Shibuda kufukuzwa CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa kitaunda kamati maalum ya kushughulikia tuhuma dhidi ya Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda (CHADEMA), ambapo akipatikana na hatia atakabiliwa na adhabu nzito ikiwemo kuvuliwa uanachama.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho na kuthibitishwa na mmoja wa maafisa wake waandamizi, zimesema kuwa kamati hiyo inayotarajiwa kukutana wakati wowote kuanzia sasa inaongozwa na mjumbe wa Kamati Kuu, Prof. Abadallah Safari.

Imedaiwa kuwa kamati hiyo maalumu itamhoji Shibuda kabla ya kutoa mapendekezo yake katika kikao cha baraza kuu ambapo kuna habari kuwa litachukua uamuzi mzito na mgumu dhidi ya mbunge huyo, ingawa imedaiwa kuwa naye atakuwa na haki ya kukata rufaa.

Hii itakuwa mara ya pili kwa kamati hiyo kumjadili Shibuda kutokana na kupingana mara kadhaa na msimamo wa CHADEMA katika masuala ya msingi ya sera na itikadi, likiwemo suala la nidhamu.

Hivi karibuni, akiwa mjini Dodoma, Shibuda alikiuka utaratibu wa chama chake na kukidhalilisha hadharani mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM waliokuwa katika semina, akidai kuwa hajaona chama kinachoweza kuongoza nchi zaidi ya chama tawala.

Akizungumza na Tanzania Daima, mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu, Samson Mwigamba, alisema kuwa kitendo alichokifanya Shibuda hakikubaliki kwa mujibu wa katiba yao, ingawa anaweza kudai ni haki yake ya Kikatiba.

Mwigamba alisema katiba inamtaka kila mwanachama wao kukipigania, kukitetea na kukieneza chama chao kwa lengo la kushika dola.

Hivyo kitendo cha Shibuda kudai kwamba mpaka sasa hajaona chama kinachoweza kushika dola, ni kukiuka katiba jambo ambalo linaweza kumfukuzisha moja kwa moja uanachama.

Source: Tanzania Daima
 
Sasa kama aliona CCM ifaa kwanini aliondoka,walimtosa kwa ajili ya mambo yake ya ukinyonga na tamaa ya madaraka,tafadhali fukuzeni huyo mtu haraka sana ili arudi CCM anakoona kufaa na wakimtosa huko basi 2015 awe mgombea binafsi wa uraisi
 
Chezea Shibuda Wewe,huyu Gamba Katumwa Kuja Kukivuruga CDM,so CDM wasipo kuwa makini inakula kwao
 
Huyu jamaa Kero. Hawezi kuita vyama vya siasa 'plate-number' eti yeye anabadilisha tu. Lakini gari lileile.
 
Hii kadhia ya Shibuda ni rahisi sana kumalizwa na wala hahitaji uongozi wa juu wa CHADEMA kunyanyua mkono. BAVICHA wamtangaze SHIBUDA kuwa ni enemy of the M4C. Basi. Kila mahali akienda watu wamwambie wewe ni enemy.
 
Mimi mpaka leo najiuliza juu ya akili ya huyu mtu anitwa John Shibuda je iko sawa?kwani
haiwezekani mtu wa jinsi hii asiyeweza kusoma alama za nyakati,wala kujali hisia za watanzania
walio wengi na anafurahia kuwaumiza kwa maneno yake yaliyo kwa maslahi yake binfsi.Naomba uongozi
wa Chadema kuweni makini na watu wa jinsi hii.Jamani watanzania tumeshaumizwa sana na magamba
na matumaini ya wengi tumeyaelekeza kwa Chadema,anapotokea mtu wa aina hii na kutoa maneno ya jinsi
hii ya kuumiza na kuvunja mioyo ya Watanzania anatakiwa kuchuliwa hatua kali za kutufanyaWatanzania tumsahau kabisa
kuwa alikuwepo kwenye siasa mtu mbinafsi wa aina hii.
 
Huyu dawa yake piga chini mjinga kweli huyu jamaa kama aliona ccm inafaa kwa nini aliondoka kuja upinzani? Hakuna haja ya kumjadili ni kumtimua tu yeye c bora kuliko chama!
 
Heri kupoteza jimbo kuliko kuwa na kamanda msaliti,anayeomba kiberiti kwa adui yake ili awashe sigara yake iliyogaramiwa na jeshi lake linaolompa mafunzo.
 
Hii kadhia ya Shibuda ni rahisi sana kumalizwa na wala hahitaji uongozi wa juu wa CHADEMA kunyanyua mkono. BAVICHA wamtangaze SHIBUDA kuwa ni enemy of the M4C. Basi. Kila mahali akienda watu wamwambie wewe ni enemy.

umenena vema mkuu!!!
itangazwe hadharani kuwa shibuda ni adui ndani yetu, apuuzwe, asipewe jukumu lolote la kukisemea chama.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hizi zote ni njama za ccm, nina uhakika ccm will do all they can kuhakikisha cdm inafurukuta... hawa jamaa hawatondoka kilaini...ccm ina hela itaanza kuwalipa wanachama wa cdm waanze kupigana wao kwa wao..
 
Chezea Shibuda Wewe,huyu Gamba Katumwa Kuja Kukivuruga CDM,so CDM wasipo kuwa makini inakula kwao

Sioni sababu ya CDM kulumbana na huyu jamaa because he is politically dead. Hana influence yeyote kwenye jamii hata katika jimbo lake la Maswa. Wamwache tu abwabwaje, baadae wanaMaswa watamwonyesha njia ya kutokea 2015. Endapo CDM wakianzisha malumbano yeyote na Shibuda kwa sasa, sanasana watampaisha katika vyombo vya habari, na anaweza kujenga influence. Wamwache tu maana hata CCM wanajua yule kwa ni insane...
 
Hana alicholeta CDM na hana ananachoifanyia CDM. Piga buti huyo akasukume mkokoteni Maswa, nyamb*f*!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom