macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 21,770
- 39,556
Bwana Joseph Kulangwa, watanzania mamia kwa mamia wanakufa kila siku kwa ajili ya uzembe na mizaha ya wanasiasa kama hii. Kina Shibuda, John Cheyo n.k hawa ni sawa na mashetani kwani kila jambo kwao ni mzaha na utani wakati watu wanakufa. Hutawasikia hata siku moja wakiukemea uovu unaoangamiza wananchi kikweli kweli bali kwao kila jambo ni mzaha na utani. Demokrasia sio uhuru wa kufanya mizaha na utani. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo kila kukicha watu wanakimbilia kutangaza tamaa zao za kuwa marais huku wananchi wanakufa kwa vifo vinavyoweza kuzuilika. Halafu huo uongo wako unaotaka kuwalisha watu ''eti watu wakijitokeza mapema kutangaza nia ya kugombea uongozi ndio tunapata nafasi ya kuwapima vizuri'' mimi naukataa. Kwani wakitangaza nia kipindi cha uchaguzi watu watashindwa kurudisha kumbukumbu nyuma na kupima waliyokwisha fanya?