Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 887
- 2,201
Mwanasiasa mkongwe nchini na M/kiti mstaafu wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Magale Shibuda amesema yuko njiani kutosha Shinyanga kwenda Dar es salaam kuyaunga mkono maandamano ya Chadema ya 24/1/2024 na kutoa sababu za kufanya hivyo.
Shibuda ambaye amewahi kuwa kada wa Chadema na Mbunge wa chama hicho amekatiriwa na Mwandishi akisema:
"Niko njiani kuja Dar es kuyaunga mkono maandamano ya Chadema si kwa sababu yoyote Bali ni kwa sababu CCM imempiga kisogo Hayati Mwl. Nyerere alichowaambia kupitia kitabu chake TUJISAHIHISHE."
Ameongeza CCM haitaki kujisahihisha kwa kusikiliza maoni ya watu wanaowaongoza. Kimebaki kuwa gulio la kupata utajiri wakilinda kwa silaha nzito za moto"
Sabubu nyingine Shibuda amesema, "CCM inajipinga yenyewe kuhusu 4R za Rais Samia Suluhu Hassan kiasi kwamba Sasa hujui nani aeleweke maana kijana wao Chalamila (Albert) ametangazia Dunia kuwa atatumia wanajeshi wa JWTZ kuwatawanya waandamanaji. Jambo hili tayari limeleta impact mbaya sana huko duniani"
Shibuda amehoji na kueleza, "maandamano ni wananchi kutoa hisia zao za maumivu yao na namna wanavyotaka waongozwe wao. Tumefanya hivyo siku za uhuru na hakukutokea haya ya majeshi barabarani. Na ijulukane maandamano si lazima kuwaona watu barabarani wanaweza kutumia picha tu za mabango kila Kona ya nchi na Dunia ikajua. Nina mashaka sana na washauri wa Rais Samia inawezekana wanampotosha ili wao wachote rasilimali fedha kwa kumdanganya".
My take: Namuunga mkono Shibuda kwa hoja ya CCM kupinga 4R za za Rais Samia Suluhu Hassan. Lakini pia Chadema watambue haya maandamano ni fursa nyingine ya kuleta Mapinduzi (mabadiliko) ambayo mkiacha kuyatumia umma hautowaamini tena maana nafasi kama hizi mlizichezea 2016, 2019, 2020 na Sasa 2024.