Wabunge wa CUF walipofukuzwa uanachama walipoteza ubunge rufaa walikata wakiwa sio wabunge

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,040
Hukumu iliyokuwa inasubiriwa hatimae leo imetoka.Katika hukumu hiyo Jaji amekiri kuwa Halima na Wenzake walikwishafukuzwa uanachama na Kamati kuu hivyo sio Wanachama wa Chadema.

Kwa kuishia hapo na kwa Mujibu wa KATIBA ya Nchi Ubunge unakoma pale Mbunge anapofukuzwa uanachama na chama chake.

Kukata Rufaa Baraza Kuu ni hatua inayofuata baada ya kufukuzwa Ubunge na Rufaa anaikata akiwa sio Mbunge .

Hili limewahi kutokea kwa Wabunge wa CUF walifukuzwa Uanachama wakafukuzwa Bungeni ndio wakakata Rufaa Kinachoshangaza ni kuona HALIMA na Wenzake licha ya kufukuzwa Uanachama na Kamati Kuu lakini Spika hataki kuwafukuza Bunge akisubiri mpaka Wakate Rufaa Baraza Kuu ikiwa huo ni ukiukwaji wa Katiba na kuendelea kuwalipa Mishahara Wabunge waliopoteza Sifa kwa kufukuzwa Uanachama.
 
Hatari ukivuta bangi na mbegu unaweza kujikuta upo dunia ya peke na ukadhani mambo yatokeayo unayajua peke yako!
 
Back
Top Bottom