Serikali Kutoa kauli Kuhusu Mgomo wa Madaktari kesho

ndugu zanguni

hakuna aneunga mkono kupigwa na kuteswa kwa Dr ulimboka! lkn aliefanya hivyo hajulikani. suala la madaktari limekua la kisiasa. siasa ni mchezo mchafu


NIMEJIFUNZA JAMBO MOJA

Nimejifunza kuwa DAKTARI HARUHUSIWI KUGOMA KUTOKANA NA KAZI YAKE INAYOHUSU UHAI. mbona huyu dr ulimboka amekimbizwa mhimbili!!! kwa nini? jibu ni rahisi, KUOKOA MAISHA YAKE. sasa kwa nini wanagoma!? ina maana wantaka watanzania wafe? mboa serikali imetatua maombi yao kwa 70% bado TC SCan pekee na mambo madogo madogo. WANATAKA NIN HAWA MADAKTARI? WANATUMWA NA IFRITI (JINI) YUPI? waziri mkuu amesema bungeni kuwa serikali kesho itatoa msimamo wake.


USHAURI WANGU
Nashauri waziri wa utumishi awafukuze wote ambao HAWATARIPOTI KESHO ASUBUHI KAZINI. tuache kuvuruga nchi yetu yenye amani kwa MAMBO YA UCHU WA MADARAKA
 
Usiseme watanzania tuko nyuma yake. Sema wewe Arnold uko nyuma yake. hatuwezi kuendelea kuiunga mkono serikali hata kama inafanya ushenzi. Ingeboresha mahitaji yao wangegoma? Au unasema hivyo kwa kuwa wewe si daktari ungejua ugumu wa kazi hiyo nawe ungegoma. mimi niko nyuma ya madaktari
Ukishapeleka mgojwa wako Kwa daktari halafu akakuambia kagoma halafu ukarudi nyumbani unamfagilia daktari kwa sababu yeyote ile huo utakuwa uendawazimu! Pinda kesho toa tamko ambalo serikali imechelea siku nyingi watz tupo nyuma yako
 
Ni kweli madaktari wanahaki ya kudai maslahi yao!!! hiyo ni haki yao kwani siku hizi hata kazi za kanisa watu hulipwa. ila inapofika hatua ya kuibana serikali kwa staili ya kumdhuru mwananchi wa kawaida tena ambaye hata hiyo PANADOL kuipata kwake ni ishu nadhani hiyo si sawa!

Serikali yetu nafikiri kuna maeneo inabidi ilaumiwe ila kwa hili tuitetee, sioni sababu ya msingi ya maana ambayo inaweza kunifanya nishawishike kuwa serikali haijafanya kitu kabisa kwenye hili la madaktari. Nafikiri imejitahidi, kuwasomesha bure tu madaktari tena kwa kodi za wananchi hilo si dogo, nafikiri sasa serikali itathmini sheria zake, hii dekezadekeza hii ndiyo inaleta matatizo haya mambo ya upole huu itaifikisha nchi pabaya sasa nidhamu irudi.

Kesho nitashangaa kama nitasikia kauli za chondechonde! Liwalo na liwe. CHONDECHONDE basi, hii chekecheka hii kwa nchi maskini kama hii haitatufikisha popote. Upole na Hekima za Rais wetu kunawatu wanataka waipandie kichwani.! wakati shuleni watoto wa wakulima wanakalia mawe kunamtu anataka atimiziwe na serkali haki zake kwa asilimia 100%

Ninaandika maneno haya maana ninamgonjwa (nadiklea intrest)

I say No! liwalo na liwe! uwepo wa mabingwa hauzuii kifo!!!
 
nchi nyingine zimeweka sheria inayozuia madaktari kugoma. wamesomeshwa na serikali. dktr bingwa mshahara wake na marupurup kwa ss unafikia milioni 8. WANATAKA NINI HAWA WATU!? WALIMU WASEMEJE NA MSHAHARI WA LAKI 3?

huyu bwana amekaidi amri ya mahakama. wanatufundisha kuwa kuanzia leo watanzania tuanze kudharau mahakama zetue?

acheni kauli ya kuwa kikwete ni dhaifu. atakuonesheni kuwa siyo dhaifu. chezea serikali wewe? (huu ni utani)
 
umetumwa na pinda nashangaa raia wengine hapo wa kumbana ni serikali na sio madaktari maana wakienda kazini kwa shingo upande na hizo panadol ndo mtakufa kama mbu wakipuliziwa dawa.
 
nchi nyingine zimeweka sheria inayozuia madaktari kugoma. wamesomeshwa na serikali. dktr bingwa mshahara wake na marupurup kwa ss unafikia milioni 8. WANATAKA NINI HAWA WATU!? WALIMU WASEMEJE NA MSHAHARI WA LAKI 3?

huyu bwana amekaidi amri ya mahakama. wanatufundisha kuwa kuanzia leo watanzania tuanze kudharau mahakama zetue?

acheni kauli ya kuwa kikwete ni dhaifu. atakuonesheni kuwa siyo dhaifu. chezea serikali wewe? (huu ni utani)
 
Kauli aliyoitoa bungeni leo asbuhi waziri mkuu pamoja naklukamatwa kupigwa kiongozi wa jumuiya ya madaktari Dr. Steven Ulimboka vinanifanya kutambua kwamba serikali yetu nzima haina mpango wowote na kujali maisha/uhai wa watanzania hata tone;
Nawasihi madaktari wote nasi tuseme liwalo na liwe haturudi kazini

View attachment 57574
Dr Ulimmboka kama alivyokutwa leo asubuhi akiwa amejeruhiwa vibaya sana, please pray for our colleague to get well soon! Ni vigumu hata kumtambua.

Siamini kama haya mambo yanatokea ndani ya Tanzania.
This is very serious. Tunataka Wabunge wa Upinzani watoe tamko kulaani huu ushenzi. Hii ni kutaka kuunyamazisha umma kwa nguvu kwa madai ambayo ni ya msingi.
 
Sasa nimegundua,kumbe Pinda akipata kauli inayomsikitisha huwa analia (Unafiki) lakini linapotekea suala zito lenye kuwagusa wananchi masikini anasema liwalo na liwe.Ndiyo maadili ya wadhaifu!
 
Ndivyo alivyo huyu "mwana wa mkulima" daima huongea bila kufikiri. Bahati mbaya kashindwa hata kutumia usemi wa bosi wakealiosema, "akili ya mbayuwayu ongeza na za kwako". Sisemi hivi kwa kumdhalilisha Pinda; ila kama mtu anamfuatilia huyu jamaa utaweza kumuweka katika ngazi mbili. 1. Huambiwa/ huandikiwa cha kusema na hawezi kusoma wala kufatakari alichoandikiwa. 2. Ni mropokaji, hatafakari athari za kauli zake kwa umma ukizingatia nafasi yake ya uwaziri mkuu.
Hii hapa mifano ya tabia na kauli za Pinda:
1. Akiwa mkoa mmojawapo magharibi mwa nchi wakati tatizo la mauaji ya albino likiendelea aliropoka, "wauaji wakikamatwa wauwawe". Pamoja na uchungu wa mauaji hayo, Waziri mkuu ni wa kwanza kuhimiza wananchi kufuata misingi ya sheria na kutochukua sheria mkononi. Kauli hii ilimcost kulia mbele ya umma wa waTz!

2. Alitishia kuwafukuza kazi madkari wote waligoma; lakini hata mgomo ulipoendelea hakuweza kuwafukuza kazi. Kwa nini? Pinda hakukaa chini na kutafakari kuwa uko utaratibu wa kumuondoa mtumishi katika ajira na pia mchakato wa kusomesha daktari mmoja una gharama kiasi gani. Kibaya zaidi alifikiri hawa madaktari ni kama shamba boy wake. Hakutaka kuangalia nini chanzo cha mgomo huu na kwa kiasi gani yeye na Serikali yake waliwafikisha madaktari mahali pa kugoma.

3. Alisema Dr. Ulimboka si daktari maana hakuna taarifa/ rekodi kuwa alimaliza mafunzo yake baada ya kufukuzwa chuo. Alimuita Dr Ulimboka mhuni; ajabu mgomo ulipopamba moto Mh. Pinda alikaa meza moja na Mhuni huyu (Dr.Ulimboka); wala hakuhoji huyu katokea wapi?

4. Alisema nitamshauri Rais kuwafuta kazi Mh.Mponda, Nkya; lakini hakufanya hivyo hadi Rais alifanya mabadiliko ya baraza kwa shinikizo la wabunge.

Ya Mh. Pinda ni mengi mno. Nadhani hata kauli hii ya "liwalo na liwe" karopoka tu; ila ajue itamgharimu!


EJL
 
Mie nadhani wote hawatutendei haki walipa kodi na wapiga kura wa nchi hii,kumbuka madktari wengi wamesomeshwa kwa kodi zetu cc wanaotusaliti leo hii na pia serikali kutolitazama tatizo hili kwa jicho la 3 na kutoa majibu dhahifu.je kunatofauti gani Kati ya boko haramu na madoktari wakibongo??

Yani watu wanatetea haki zao unawafananisha na BOKO HALAM unanitafutia bani MBWA MWITU wewe...mood nimekuwa provoked na huyu FISI MAJI.
 
Kauli aliyoitoa bungeni leo asbuhi waziri mkuu pamoja naklukamatwa kupigwa kiongozi wa jumuiya ya madaktari Dr. Steven Ulimboka vinanifanya kutambua kwamba serikali yetu nzima haina mpango wowote na kujali maisha/uhai wa watanzania hata tone;
Nawasihi madaktari wote nasi tuseme liwalo na liwe haturudi kazini

View attachment 57574
Dr Ulimmboka kama alivyokutwa leo asubuhi akiwa amejeruhiwa vibaya sana, please pray for our colleague to get well soon! Ni vigumu hata kumtambua.

Napata shida kidogo kwamba nikupe pole wewe au wale wagonjwa ambao kwa lengo lenu la kugoma na kuiwajibisha serikali wengi wanateseka,wengine wanakufa,mama zetu wanajifungua kwa uchungu bila ya kua na msaada wowote,haya ni mateso makubwa,
Hemu tujiulize vipi kama ulimboka na yeye kama akitelekezwa aachwe bila ya huduma yoyote?
ni vyema madaktari watafute njia tofauti yakuibana serikali kwani watanzania wasio na hatia wanakufa kwa kosa la serikali
 
umetumwa na pinda nashangaa raia wengine hapo wa kumbana ni serikali na sio madaktari maana wakienda kazini kwa shingo upande na hizo panadol ndo mtakufa kama mbu wakipuliziwa dawa.

Ukiwa na mgojwa utajua ninacho kisema! sasa subiri kesho ndiyo utajua kama serikali ni kitu gani?
 
Bravo Madaktari!, Tatizo la kuchangua kiongozi Dhaifu, na kuwa naselekari dhaifu.

Hakuna cha mtoto wa mkulima hapo tena, wamesha m-contaminate,
 
Ni kauli ya mtu aliyekata tamaa ambaye hana uwezo wa kupata ufumbuzi wa tatizo. Ni uthibitisho kwanini awamu hii imekwama. Ni udhaifu mkubwa. Sijui kwanini asijiuzulu akawapisha wenye uwezo.
Liwalo na liwe" viongozi dhaifu, serikali dhaifu
 
Kwa hili lililotokea la Dr. Ulimboka ambalo limehusishwa sana na kauli
yako ya LIWALO NA LIWE ni busara kwako ukiamua kujiuzulu.
Bila shaka umenielewa kwani nina wasiwasi wa kuhusishwa na mengine
makubwa zaidi ambayo pengine utakuwa huhusiki nayo.
Jiuzulu Mheshimiwa ili kulinda Imani ya wapiga kura wako wa Rukwa.
 
Back
Top Bottom