Samaki wa Magufuli wafufua mgogoro wa muungano?

,,,,Kama serikali kamilifu,basi ni wajibu wa SMZ kuchukua jukumu lake hilo la kulipia pia GHARAMA za kuwatunza hao samaki kwa mgawano huohuo wa 40%, tatizo hata wakipewa percent hiyo ambayo inatambuliwa kisheria katika jumla ya tani 260 huko za hao samaki,ni mgao mkubwa kwelikweli,hivi na tatizo hili la umeme tutawatunza vipi hao,huyo waziri aache kutuhamishia "goal posts" sasa,tuna tatizo la msingi la umeme zanzibar,Serikali ya SMZ inatusaidia vipi kutoka hapa???

Inaonyesha hujuwi kuwa matumizi ya pesa hata kama kwa Tanganyika basi ni matumizi ya Muungano na hivyo hivyo malipo ya samaki yalifanywa na Muungano. Mpaka pale jeshi, magereza na mahospitali ya Bara yatakapolazimishwa kulipia basi nayo Zanzibar ionaweza ikatakiwa ilipie.
 
Huyu naye kituko tu! Sasa kwani kama aliliona hilo kwa nini asingemwambia kabla ya kutoa maamuzi! Au alikuwa anamtegea akishasema tu na yeye aranduke na maneno yake ili watu wamuone na yeye yupo Khaaaaa aende zake bana

Yanini kumuamsha alielala? Kama waziri haelewi kuweko kwa sehemu mbili za Muungano? Naam ilibidi hivyo ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Huu Muungano una kero kweli kweli, ningekuwa na uwezo ningeuvunjilia mbali ili nchi ile cha kwao. Naanza kuona kama vile Mtikila alikuwa sahihi kudai kuwepo kwa taifa la Tanganyika ambayo ingekuwa ni njia nzuri ya kuelekea kuvunja muungano huu.

Baadaye hata Tabora nao watasema ilikuwaje samaki hao waishie Dar tu wakati Tabora nayo ni saehemu ya Tanzania? Hili dai la kutaka mtu atoke Zanzibar aje Dar kujadili swala la matumizi ya samaki wale, kitu ambacho kinaweza kutolewa maamuzi na mtu mmoja kama ilivyotokea ni kuonyesha jinsi gani tunavyopenda kutumia muda na raslimali za serikali vibaya.

kwani hilo hulijuwi Mkuu ?mtu hatupi Jongo na ujiti wake.
 
hii ya kusema zanzibar haichangii kwenye mambo ya muungano mie haijanikaa vizuri kwa kweli. Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania(Zanzibar na Tanganyika) kwa hio by default Zanzibar inachangia kwenye muungano tokea rasilimali watu kama Dr shein na mawaziri wengine pamoja na watendaji wengine wa serikali na mashirika. Pia inachangia rasilimali nyengine au ghafi sasa tunachangia ila zanzibar haichangiwi na Tanganyika sasa Zanzibar anachanga kwa Tanganyika, zanzibar na muungano
 
..Zanzibar walipewa tani 80 kati ya tani 296 zilizokamatwa. sasa wakadai hiyo siyo asilimia 40 wanayopaswa kugawiwa kama ilivyoelekezwa ktk makubaliano ya muungano.

..sasa hivi serikali ya Muungano imeelekeza kwamba Zanzibar watapewa tani 120 kama walivyodai. hatua za kutekeleza uamuzi huo zimeanza.

..pamoja na kudai hiyo asilimia 40, Zanzibar pia wameomba MSAADA wa kuhifadhi samaki hao kwasababu hawana UMEME.

NB:

..naona huu Muungano uvunjwe tu, na mashirikiano ya Zenj na Tanganyika yawe kupitia jumuiya ya Afrika Mashariki.

..Tanganyika inabeba mizigo na lawama isizostahili.

..hebu tujiulize gharama za kuhifadhi samaki hao, Zenj imechangia kiasi gani?
 
Ukivunjwa mie mmoja wa wazanzibari ambae nitapiga bonge la party kusherehekea!

Kumbukeni Tanganyika kuwa wazanzibari hawakutaka muungano from the first place!Ni nyie na Nyerere wenu ndio mulilazimisha na munaoendeleza kutukumbatia, jiulize ni mara ngapi Zanzibar imeshafanya majaribio ya kutaka kujitoa na muungano huu?

Ukizijua ni mara ngapi then utaweza kusema kama Tanganyika inabeba mzigo au Zenji ndio inabeba mizigo...
 
Froasty said:

Mr.Froasty,

..walioushabikia Muungano ni Nyerere na Karume kwasababu ambazo zilikuwa relevant zama hizo. leo hii hakuna sababu zozote zile za msingi za Muungano huu kuendelea kuwepo.

..kwa upande mwingine Wazenj mnatunyonya Watanganyika. hebu chukulia hili suala la hawa samaki. waliokamata hao samaki ni Watanganyika. waliowahifadhi kwa gharama kubwa tu ni Watanganyika. wanaohangaika na kesi mahakamani ni Watanganyika. nyinyi Wazenj mnatokea siku ya mgao tu. tena hata hao samaki wa mgao mnaodai, mnaomba msaidiwe kuwahifadhi.

..hakuna juhudi zozote zilizofanywa na Wazenj kuvunja muungano. sana sana kinachofanyika ni juhudi za kutaka kutunyonya zaidi Watanganyika. juhudi ninazoziona mimi ni za Wazenj ni kupata share kubwa zaidi ktk mambo yetu Watanganyika.

..hata mapato ya dhahabu iliyopatikana Tanganyika mnataka mgaiwe!! lini mmesikia Watanganyika tukiwadai mabungo, mihogo,na karafuu, iliyoko Zenj??
 
Hata mafuta yetu pia hamuyataki, hii sasa kali.Iko wazi bro Zanzibar hatutaki muungano, mie maishani mwangu sijawahi kuulizwa utaifa wangu nikasema mtanzania.Always nasema natoka Zanzibar, na hiyo ni natural kabisa sijaona cha kujivunia Tanzania na wala damu yangu hainipelekei kusema mtanzania.

Kwa hiyo hoja ya muungano kama huutaki, we are on the same boat!

Kusema Zenji inainyonya Tanganyika, hapo naona kama haingii akilini.Japo suali hili la samaki hata mie sasa hivi naona kama ni vyema mukaachiwa hao samaki.Hapo ni kutokana na sababu za kibinadaamu, lakini huu na uwe mfano kwenu na JK wa kuteletea mjadala na utafiti mzima wa kuangalia mfumo wa muungano na faida zake.

Kwa upande wangu kama mzanzibari sina faida hata moja ya muungano ambayo naweza kuinyooshea vidole, natamani kama leo Zanzibar itoke nje ya muungano.Sasa kama na Tanganyika inaona haina faida inayopata, basi uvunjwe tuu.

Nyie ndio wenyewe jeshi na asilimia kubwa ya Tanzania, mukitaka hata na jina la Tanzania pia tutakuachieni!
 
Mr.Froasty,

..kuna eneo la bahari ambalo rasilimali zake zinapaswa kugawanywa kwa Zenj na Tanganyika. ukipitia sheria za kimataifa za bahari unaweza kupata ufafanuzi mzuri. kama mafuta, gesi,..yakipatikana ktk eneo hilo basi kuna ulazima wa kugawana.

..kwa upande mwingine, kama mafuta au gesi yakipatikana Kigoma au Mwanza sioni ulazima wa kugawana mafuta hayo baina ya Zenj na Tanganyika. ni kama vile ambavyo karafuu inapatikana Pemba na hakuna Mtanganyika mwenye haki nayo.

..ukweli kwamba hakuna Mzenj anayependa au kuona fahari ya kuwa Mtanzania ni moja ya sababu zinazonisukuma mimi kuamini ni bora Muungano huu uvunjwe. I understand that majority of Zanzibaris would rather be associated with the Arabs. nimeshuhudia kwa macho yangu, Mzenj mweusi kama Jaluo, lakini anausema vibaya Uafrika na Waafrika, na wakati huohuo akiutukuza Uarabu!!

..kuhusu kubakia na jina Tanzania hilo pia siyo wazo baya. Watanganyika kutokana na ukarimu wetu tumewekeza sana ktk jina hili Tanzania. tumemwaga damu chini ya bendera ya Tanzania.

NB:

..hakuna haja ya Jeshi kuhusika ktk kuuvunja Muungano huu. kwa mtizamo wangu Bunge na Baraza la Wawakilishi ndiyo vyombo muafaka vya kushughulikia tatizo hili.
 
Mie sio mwana sheria siwezi kujua mipaka ya Zanzibar na Tanganyika.Lakini hisia zangu zinaniambia kuna ujanja mwingi Tanganyika inafanya katika muungano huu na kujinufaisha.Na tokea asubuhi nilipozaliwa nina hisia za kuwa Zanzibar iko katika nafasi nzuri kusonga mbele kimaendeleo na kujinasua na umasikini ikiwa nje ya muungano kuliko ikiwa ndani ya Tanzania.

Kwa hiyo ngumu kunifahamisha nikakuelewa kama Tanganyika ina haki yoyote ya mafuta yatakayopatikana katika eneo la Zanzibar, wakati mafuta yatakayopatikana Mwanza yasifaidishe Zenji.

..ukweli kwamba hakuna Mzenj anayependa au kuona fahari ya kuwa Mtanzania ni moja ya sababu zinazonisukuma mimi kuamini ni bora Muungano huu uvunjwe. I understand that majority of Zanzibaris would rather be associated with the Arabs. nimeshuhudia kwa macho yangu, Mzenj mweusi kama Jaluo, lakini anausema vibaya Uafrika na Waafrika, na wakati huohuo akiutukuza Uarabu!!

Kuhusiana na uarabu, sioni kama mtu mmoja alie mweusi au mweupe kupenda waarabu ikawa ndio sababu ya kugeneralize watu wote wa Zanzibar kuwa ni waarabu.

Mie ni mzanzibari na ofcourse nina jamaa wa kiarabu, lakini sina interests zozote za kujisifia kama nina asili ya kiarabu au bibi yangu alikuwa anatoka Oman.

Wala sichukii muarabu, mzungu, muafrika nimeshakuwa na marafiki wengi tuu kutoka sehemu mbali mbali za dunia Vietnam, Spain, Rusia, Cameroon, Nigeria,Tanganyika etc.Makabila hayo yote nimeishi nayo vizuri tuu, na wala sijawahi kustereo type nchi nzima kwa kuwa mmoja ya watu hao alikuwa na tabia fulani.

All in all huo ndio ukweli wazanzibari wanapenda kutumia utaifa wao kama ni wazanzibari, kama Tanganyika imewekeza kwenye jina la Tanzania hakuna tatizo lolote kama mimi ningelikuwa kiongozi munaweza kuchukua hilo jina na mukatuachia Zanzibar yetu.

Zanzibar jina lake liko tokea enzi na jina ambalo ukimtajia tuu mtu anakuwa interested bila ya hata kujua nchi hiyo iko wapi!

Cheers.
 
Mr.Froasty,

..kuna kipengele hiki hapa cha sheria za kimataifa za bahari na rasilimali zake zinatoa mwanga kidogo kuhusu haki na umiliki wa mafuta ikiwa yatapatikana ktk eneo la mwambao wa Tanganyika na Zanzibar.

Law of the Sea said:
In 1982 a United Nations treaty known as "The Law of the Sea" was presented. It addressed navigational rights, territorial waters limits, exclusive economic zones, fishing, pollution, drilling, mining, conservation and many other aspects of maritime activity. With over 150 nations participating it was the first attempt by the international community to establish a formal agreement on how the seas can be used. It also proposes a logical allocation of ocean resources.

Under the Law of the Sea, each country receives exclusive economic rights to any natural resource that is present on or beneath the sea floor out to a distance of 200 nautical miles (230 miles / 371 kilometers) beyond their natural shorelines.

..hapa chini utaona Raisi Museveni anazungumzia huu muungano wa Tanganyika na Zanzibar. sasa utaona anabainisha kwamba kati ya Zenj na Tanganyika hakuna anayeweza ku-claim hizo 200 nautical miles[230 miles / 371 kilometers] za Exclusive Economic Zone.

..sasa katika mazingira kama hayo mgawanyo wa rasilimali za baharini ktk mwambao wa Zenj na Tanganyika unapaswa kuwa vipi?

..msome Raisi Museveni hapa chini...

Yoweri Museveni said:
Mwalimu Nyerere and late Mzee Karume, together with the Tanganyika National Union (TANU) and Afro-Shirazi Party (ASP), created Tanzania in 1964. Both of them are now dead. Who is benefiting from the union? It is the Tanzanians of this generation. If Tanganyika and Zanzibar had remained separate, there would be a lot of complications which sometimes we do not think about. Take the example of the exclusive economic zones in the ocean according to the Law of the Sea which is supposed to be 200 Nautical miles. How would Tanganyika and Zanzibar handle that as separate states being so entertwined? The Union of Tanganyika and Zanzibar in 1964 obviated those problems.

..nime-google na nimekutana na data zinazosema kwamba umbali kati ya Dar na Zenj ni 44.23 miles [sina uhakika na data hizo.] kama unataka kuamua kuhusu suala la mafuta ktk mwambao wetu basi unapaswa kuanzia hapo na kuzingatia sheria za bahari za kimataifa.

..pia nimetembelea wikipedia na wanaelezea vizuri masuala kama TERRITORIAL WATERS[12 nautical miles], CONTIGUOUS ZONE[territorial + 12 nautical miles], na EXCLUSIVE ECONOMIC ZONE[200 nautical miles].
 
Wapewe hiyo 40%, nafikiri haki ya mtu kuila ni haramu..kama sheria za muungano zinasema mgawabyo wa aina hiyo waziri alitakiwa awe anafahamu hivyo..

Miaka ya zamani ya ku take for granted vitu kama hivi imekwisha, wazanzibar wanajua haki zao, wana haki ya kusema..dai waziri wala usikate tamaa
 
..Zanzibar walipewa tani 80 kati ya tani 296 zilizokamatwa. sasa wakadai hiyo siyo asilimia 40 wanayopaswa kugawiwa kama ilivyoelekezwa ktk makubaliano ya muungano.

..sasa hivi serikali ya Muungano imeelekeza kwamba Zanzibar watapewa tani 120 kama walivyodai. hatua za kutekeleza uamuzi huo zimeanza.

..pamoja na kudai hiyo asilimia 40, Zanzibar pia wameomba MSAADA wa kuhifadhi samaki hao kwasababu hawana UMEME.

NB:

..naona huu Muungano uvunjwe tu, na mashirikiano ya Zenj na Tanganyika yawe kupitia jumuiya ya Afrika Mashariki.

..Tanganyika inabeba mizigo na lawama isizostahili.

..hebu tujiulize gharama za kuhifadhi samaki hao, Zenj imechangia kiasi gani?

Kwani huu Muungano wenu ni wa nani na nani mbona mnajifanya hamuwelewi? Huu Muungano na muundo wake si mmeuweka nyie Tanganyika (kwani hakuna hata saini za Zanzibar kwenye documents za huo Muungano)? Sasa mliweka wapi mpaka katika Matumizi kati ya Serikali ya Muungano na ile ya kwenu ya Tanganyika? Mlivyojipangia chenu ni cha Tangavyika na cha Muungano ni cha Tanganyika, mgaliweka mipaka basi tungejuwa Zanzibar ina kiasi gani katika matumizi na Tanganyika ina kiasi gani.

Mkorogano huu wa mapato na matumizi unawanufaisha nyinyi kwani mkitaka kujenga Mwanza mnachukua fedha za Muungano, mkitaka kujenga barabara Kigoma pesa ni za Muungano lakini Zanzibar wakitaka umeme wa Muungano mnatowautaratibu mwengine ionekane kuwa Zanzibar hawahusiki na umeme na sasa samaki wa Muungano mmetumia zaidi ya bilioni za Muungano kuwahifadhi na baadae mnataka Zanzibar eti wachangie.
 
..Zanzibar walipewa tani 80 kati ya tani 296 zilizokamatwa. sasa wakadai hiyo siyo asilimia 40 wanayopaswa kugawiwa kama ilivyoelekezwa ktk makubaliano ya muungano.

..sasa hivi serikali ya Muungano imeelekeza kwamba Zanzibar watapewa tani 120 kama walivyodai. hatua za kutekeleza uamuzi huo zimeanza.

..pamoja na kudai hiyo asilimia 40, Zanzibar pia wameomba MSAADA wa kuhifadhi samaki hao kwasababu hawana UMEME.

NB:

..naona huu Muungano uvunjwe tu, na mashirikiano ya Zenj na Tanganyika yawe kupitia jumuiya ya Afrika Mashariki.

..Tanganyika inabeba mizigo na lawama isizostahili.

..hebu tujiulize gharama za kuhifadhi samaki hao, Zenj imechangia kiasi gani?

Pathetic. Pamoja na kuwahifadhia bure, gharama za kuendesha kesi hawatachangia, na kama tukishindwa kwenye kulipa damages wataturuka kimanga! Halafu wakitubeza kuwa tunajipendekeza tunakasirikia nini?

Amandla.........
 
Mr.Froasty,

..walioushabikia Muungano ni Nyerere na Karume kwasababu ambazo zilikuwa relevant zama hizo. leo hii hakuna sababu zozote zile za msingi za Muungano huu kuendelea kuwepo.

..kwa upande mwingine Wazenj mnatunyonya Watanganyika. hebu chukulia hili suala la hawa samaki. waliokamata hao samaki ni Watanganyika. waliowahifadhi kwa gharama kubwa tu ni Watanganyika. wanaohangaika na kesi mahakamani ni Watanganyika. nyinyi Wazenj mnatokea siku ya mgao tu. tena hata hao samaki wa mgao mnaodai, mnaomba msaidiwe kuwahifadhi.

..hakuna juhudi zozote zilizofanywa na Wazenj kuvunja muungano. sana sana kinachofanyika ni juhudi za kutaka kutunyonya zaidi Watanganyika. juhudi ninazoziona mimi ni za Wazenj ni kupata share kubwa zaidi ktk mambo yetu Watanganyika.

..hata mapato ya dhahabu iliyopatikana Tanganyika mnataka mgaiwe!! lini mmesikia Watanganyika tukiwadai mabungo, mihogo,na karafuu, iliyoko Zenj??

Sir Joka Kuu msingi wa ulioleta malalamiko yote hayo ni kuwa hao samaki nim wa Zanzibar na fahamu kuwa Zanzibar imekuwa nanguvu kwa sababu ya hao samaki kuwa ni wao.

Si unaelew mlivyo, chenu ni chenu tu unafikiri mgekubali vipi kugawana na Zanzibar kama sio mnakabiliwa na ukweli?
Kuhusu hili la kudai dhahabu si kweli kuwa Zanzibar ina haja na dhahabu yenu bali hiyo ni element ya ushahidi wa kukufanyeni nyie muone vibaya kuwa kwa karibu miaka44 nyuma mmekuwa mkikumbatia raslimali yenu na hata pale wenzenu wanapopata ya kwao kiroho kinawauma na kutaka iwe bia.
 
Mr.Froasty,

..kuna eneo la bahari ambalo rasilimali zake zinapaswa kugawanywa kwa Zenj na Tanganyika. ukipitia sheria za kimataifa za bahari unaweza kupata ufafanuzi mzuri. kama mafuta, gesi,..yakipatikana ktk eneo hilo basi kuna ulazima wa kugawana.

..kwa upande mwingine, kama mafuta au gesi yakipatikana Kigoma au Mwanza sioni ulazima wa kugawana mafuta hayo baina ya Zenj na Tanganyika. ni kama vile ambavyo karafuu inapatikana Pemba na hakuna Mtanganyika mwenye haki nayo.

..ukweli kwamba hakuna Mzenj anayependa au kuona fahari ya kuwa Mtanzania ni moja ya sababu zinazonisukuma mimi kuamini ni bora Muungano huu uvunjwe. I understand that majority of Zanzibaris would rather be associated with the Arabs. nimeshuhudia kwa macho yangu, Mzenj mweusi kama Jaluo, lakini anausema vibaya Uafrika na Waafrika, na wakati huohuo akiutukuza Uarabu!!

..kuhusu kubakia na jina Tanzania hilo pia siyo wazo baya. Watanganyika kutokana na ukarimu wetu tumewekeza sana ktk jina hili Tanzania. tumemwaga damu chini ya bendera ya Tanzania.

NB:

..hakuna haja ya Jeshi kuhusika ktk kuuvunja Muungano huu. kwa mtizamo wangu Bunge na Baraza la Wawakilishi ndiyo vyombo muafaka vya kushughulikia tatizo hili.

Sir Joka Kuu,
Bora uwe na msimamo! Hakuna pahala hata pamoja pataposababisha nchi mbili zigawane rasilimali na badala yake upande mmojawapo utakuwa na haki yake peke yake. Tukija kwenye suwala la mafuta ya pwani ya Zanzibar ni wazi kuwa mafuta hayo ni ya Zanzibar na ndio maana kukawa na mvutano wa kuwa ni mali ya Muungano au la. Mvutano hapa haupo kuwa ni mali ya Tanganyika au Zanzibar. Mafuta yanayogombewa ni ya Zanzibar nanyi mnataka eti tugawane wakati yalioko Mtwara Zanzibar hawana haja nayo kwa vile wanawajuwa nyie kuwa wachoyo wa vyenu.
 
Back
Top Bottom