Kikwete watumishi wa Mungu hawezi kutofautisha siasa na dini kwa sababu siasa ni dini na dini ni siasa

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Dec 24, 2014
609
1,007
Watanganyika wenzangu someni andiko hili mtapata faida na maana kubwa acheni kuhadaiwa na viongozi wa kisiasa wanataka kuigeuza nchi yetu shamba la Bibi.🩸🩸🩸

Kwanza kabisa napenda niwashukuru Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuuelewesha Umma. Kanisa Katoliki ni kanisa lenye sifa na heshima Duniani kwa kuwa na Uongozi uliokomaa na kusimikwa kuanzia ngazi ya familia Duniani.

📌 Mheshimiwa Kikwete kama hujui acha tukujuze yafuatayo:

🔹 Dini hizi zote ni Imani tulizoletewa na wakoloni kwa kuwa Babu na Bibi zetu walikuwa na Imani zao ambazo walikuwa wanaamini kabla ya kuja ukoloni.

🔹Historia inaonyesha Dini zimeanza kuingia Barani Afrika miaka ya 1600 - 1700.

🔹 Dini na siasa haviwezi kutenganishwa kwa sababu Dini ni serikali na serikali ni Dini.

Ndio maana jifunze kabla ya kusema kwa muono uliouleta leo hii ili tukujuze.

🩸 Roman Catholic ni kanisa Mama Duniani ambapo kanisa hili makao makuu ya kanisa yako Vatican city na Mkuu wa Kanisa ni Papa ambaye hata wewe unamuheshimu na kumtukuza kama Mkuu wa Kanisa na Mkuu wa serikali ya Vatican city kama nchi.

🩸 Makao makuu ya kanisa la Anglican yako Uingereza ambapo Mkuu wa kanisa hilo ni Malkia au Mfalme wa Uingereza na Uingereza ni nchi.

🩸 Makao makuu ya kanisa la Rutheran yako Ujerumani na mkuu wa kanisa hilo ni Rais wa Ujerumani na Chancellor wa Ujerumani.

🩸 Makao makuu ya makanisa ya Pentecostal yako Marekani na hii ni baada ya Vita kuu ya kwanza ya Dunia Marekani walikuja kustuka ya kuwa ili upate uungwaji mkono wa mtu mweusi ni lazima uwapelekee Imani na Dini ili wapate kuamini hivyo wakaweka mkakati wa kuanzisha Imani na Dini katika Afrika.

🩸Imani zipo nyingi sana kwani historia zinaonyesha katika Imani hizo zipo nyingine zilianza hata BC na kusimamia imara mfano Krishna n.k.

🩸Uislamu ni Imani na Dini iliyoletwa kwetu na Waajemi na Historia inaonyesha waliingia nchini miaka ya 1700 kwa kisingizio cha wafanyabiashara wa pembe za ndovu na mazao ya kilimo, lakini baadaye wakawa wafanya biashara wa kuwauza watumwa kwa Wazungu.

🩸Uisalma makao makuu yao yapo Saudia na katika Uislamu kumegawanyika katika makundi 73 kwa mujibu wa Quran. Na hapa naweza kukutajia machache tu ingawa wote wanaamini katika Muhimili mmoja wa Mtume Mohamed:

Shia
Sun
Bohora
Ahamaddiya

Haya ni baadhi ya madhehebu ya Kiislamu ingawa yapo mengi sana na haya ni mfano wapo tu.
🩸 Hapo unawezaje kutofautisha Dini Imani na serikali ikiwa wakuu wa Imani na Dini ndio hao hao wakuu wa serikali hizo zinazotawala Nchi na Dunia?


MADA KUU.

Mheshimiwa Rais mstaafu wa awamu ya nne, kwanza katika hutoba yako tumesikia ukieleza namna ulivyotatua mgogoro wa kiimani Zanzibar. Ngoja tukueleze na kukukumbusha.

🔹Mgogoro wa kiimani Zanzibar ulisababalishwa na Viongozi wa kisiasa ambao walianza kutamka wazi wazi nchi ya Zanzibar ni nchi ya Kiislamu na kupelekea wananchi wa Zanzibar kutengeneza chuki kwa wakristo na kuamua kuchoma makanisa Tukasahau hakuna Zanzibar nchi bila Tanganyika na sheria inasema Taifa letu halina Dini bali watu wake ndio wenye Dini.

🔹Tunatambua wazi asilimia kubwa ya wananchi wa Zanzibar ni waislamu ingawa wakristo wapo pia. Zanzibar haijawahi tawaliwa Rais mkristo tokea mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. Vivyo hivyo Tanganyika Bara Kuna idadi kubwa ya Wakristo mara 2 au zaidi ya waislamu ingawa Tanganyika kumetawaliwa na Wakristo na Waislamu.

🔹Maasi hayo na mgogoro huo kipindi yanatokea wewe ulikuwa Rais wa Tanzania mwenye Imani ya Uislamu na wakristo hawakurejesha kisasi wakiamini katika akupigaye shavu la kushoto mgeuzie la kulia. Je unawezaje kujisifia kwa jambo kama hilo?

🔹 Tanzania kiujumla, Ukristo umegawanyika katika madhebu tofauti tofauti lakini Imani yao wote ni wakristo wanaamini katika Kristo.

🔹Kiimani na kielimu wakristo wamejikita katika Elimu Dunia na Elimu Akhera na ndio maana karibia Mapadree wote ni PhD holders na hata wachungaji na Maaskofu. Kwani katika msingi wa Imani ya Ukristo elimu zote zinaendana.🔰🔰🔰🔰

🔹 Katika nchi yetu ya Tanzania kwa bahati mbaya sana Tanganyika haina serikali tumesimama na kuishia kusema sisi ni Watanganyika na tukajiweka ndani ya koti la Utanzania.

🔹Hivyo tukakubali kutawaliwa au kuongozwa na Wazanzibar na Watanganyika wenzetu kitu ambacho tuliamini katika Umoja.

🔹Katika Uongozi, sisi tuko tayari kuongozwa na Wanzibar kwa kuanzia na viongozi wa ngazi ya mtaa, kata, wilaya, Mkoa na hata Taifa. Je Zanzibar kuna Mtanganyika ambaye ni kiongozi au anaruhusiwa kumiliki ardhi?

SISI WACHUNGAJI NA BARAZA LA MAASKOFU TURUDI KWENYE HOJA KUU NA MSINGI JUU YA IMANI ZETU, TUSICHANGANYE DINI NA SERIKALI.

Mheshimiwa Rais mstaafu hongera kwa kutoka hadharani na kutueleza hayo lakini tunakuomba upate kutoa ufafanuzi juu ya maswala yetu ambayo tunahitaji majibu juu ufisadi na upendeleo wa haya yanayoendelea nchini juu ya mkataba wa DP WORLD.

📌Baada ya Mkataba wa DP WORLD tumeshuhudia yafuatayo yakiendelea katika nchi yetu na upendeleo wa makundi na hata kutugawa.

❇️ Je uliwahi kutoka na kueleza kama Rais mstaafu mpaka uone BARAZA LA MAASKOFU likitoa msimamo wake nawe ndio utoke na kusema?

❇️ Waislamu na Mashekhe walisimama na kumuunga mkono Mhe Rais Samia juu ya uwekezaji wa Bandari uliwahi kujitokeza na kusema wasichanganye Dini na serikali?
❇️ CCM walitembea nchi nzima wakiusifia Mkataba na kutoa elimu ya uwekezaji wa Bandari, Uliwahi kutoka na kusema wasichanganye siasa na uongozi wa serikali?

❇️ Machawa waliandamana nchi nzima wakiunga mkono uwekezaji wa DP WORLD uliwahi kujitokeza na kusema wasichanganye mahaba na utendaji wa serikali?

❇️ Serikali imewabambikia kesi za uhaini watu wasio kuwa na uhusiano wa Majeshi je wewe kama Rais mstaafu uliwahi kujitokeza na kuwatetea kwa kuuelezea umma madhara ya kesi za namna hiyo?

🩸🩸 Iweje leo Baraza la Maaskofu, watetezi wa mali za nchi, Mawakili wanaotaka kutetea rasilimali za nchi pamoja na watu wanaotaka haki na sheria vizingatiwe wawe wahujumu uchumi au waonekane wanakuwa wachochezi au wanachanganya Imani na serikali?

UFISADI UMEKITHIRI.

Mheshimiwa Kikwete nchi yetu kwa sasa haiko salama wala hakuna amani ni kutokana na uongozi wa Chama cha mapinduzi kutokuangalia umuhimu wa usawa na haki kwa Taifa.

🇹🇿 Kinachozungumzwa na Baraza la Maaskofu Tanzania sio kukataa Mkataba bali taratibu sheria na kanuni zifuatwe katika kutoa hiyo tenda kwa DP WORLD na sio vinginevyo.

🇹🇿 Sheria za ugawaji tenda zitangazwe mashirika yashindanishwe na atakaye shinda tenda birds apewe kulingana na makubaliano serikali itakayoingia na kuwa na mkataba makini na wenye tija kwa pande zote mbili.

🇹🇿 Nchi hii ni mali yetu sote kuwepo na haki katika pande zote yaani kwa wanahoji wapewe majibu na wanaotetea walete majibu.

🇹🇿 Bunge lisitumie nguvu kubwa katika kuunga mkono hoja za uuzwaji wa Bandari kwa kulazimiashia kuwa sehemu ya wananchi kwa uroho wa fedha na kupoteza utu wao.

🇹🇿 Bunge kwenda kupitisha sheria ya umiliki wa ardhi kwa wageni ni kosa kubwa sana bila muswada huo kupitia kwa wananchi ambapo tumeshatambua mchezo mchafu unaofanywa na kikundi cha watu wachache kuonekana wametoa maoni kwa niaba ya wananchi.

🔑 Mheshimiwa Rais mstaafu wewe na kikundi cha baadhi ya familia za watu wachache katika nchi hii sio wasafi na tunajua unatoka hadharani kutetea ugali wako tunaomba uwe muwazi na mkweli.

🔑 Takwimu zinaonyesha wewe ni sehemu ya mnufaika wa baadhi ya Ghati pale Bandarini ambapo ulikuwa ukivuna mapesa mengi kupitia TICTS na hata hapa unatetea ugali baada ya kuona mambo magumu na ikiwa kanisa litasimamia msimamo wake nawe utakosa.

🔑 Katika uongozi wako ufisadi mwingi umetokea ukiwemo wa RICHMOND na Escrow je uliwahi kusema au kuomba radhi kwa wananchi.

Wewe sio msafi hata kidogo katika jambo hilo na huwezi kuwa msafi kwa kauli hii uliyoinena Leo.

Wewe ndio mchonganishi na mwenye kuingiza au kutaka kujimilikisha siasa na uongozi na kutugawa sisi kama wananchi.

Sisi kama viongozi wa Dini jukumu letu ni kusimamia amani na mshikamano kama vitabu vyetu vinavyotuongoza.

Mkataba wa DP WORLD hauna viashiria vya amani wala umoja kwa Taifa letu. Ikiwa Rais ni Mzanzibar, Waziri aliyeingia Mkataba ni Mzanzibar na Katibu mkuu wa wizara husika ni Mzanzibar.

Inaonyesha katika utendaji kazi wako unatuheshimu nasi tutakuheshimu kuwa mkweli na muwazi kwetu usiwe na kauli mbili.

Katika mambo ya Muungano Bandari sio jambo la Muungano iweje haya yatokee nankutendeka?

Nakushauri kuwa mshauri mwema na sio mtu wa mihemko na tamaa za mwili na akili kwa kutaka kuuza Tanganyika na mali zake. Mshauri Mama Samia vyema juu ya mkataba wa Bandari haufai hatuko tayari kuona tunakuja kuingiza kizazi chetu machafukoni na kwenye ulipaji wa madeni kwa DP WORLD.

Mbona ni mengi yametokea, Loliondo, KIA na hatujasikia umetoka kukemea au kuwakemea wahusika why hili?

Sisi tutasimama imara na tutasema kwa sababu kazi za kichungaji ni kutunza amani na kueleimisha jamii kimaadili.

Asante
Tuipende nchi yetu kama Taifa teule la Mungu🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🔑🔑🔑🔑🔑
🔰🔰🔰🔰🔰🔰🔰🔰🔰🔰
 
Dini kwenye elimu sawa,ndio maans wanajenga shule.Dini kwenye afya za wananchi sawa, ndio maana wanajenga hospital.

Dini kwenye siasa eti no no no no no kwanini? Ili uhubiriwe uelewe, inabidi uwe na uelewa mzuri( elimu) na afya njema. Lakini pia lazima iwepo amani.

Amani inatokana na siasa safi. Hapo dini utaitengaje na siasa.Mbona bungeni kuna maaskofu na wachungaji?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom