Mkereketwa
JF-Expert Member
- May 19, 2007
- 202
- 25
Hicho nacho ni kipaumbele cha maendeleo ya nchi "Kugawana Samaki"
Hivi mbona sikuwai kuwasikia toka siku wamekamatwa samaki hawa? iweje leo? ama kweli mchuzi mtamu jaman teh, teh, teh
bila shaka wako tayari kulipia na gharama za utunzaji kwa 40%, au sio ndugu zetu?
Hicho ndio kinachotakiwa, sio kama Zenji wanataka hao samaki waliotoka kwenye mafriza.Huu Muungano una kero kweli kweli, ningekuwa na uwezo ningeuvunjilia mbali ili nchi ile cha kwao.
Wazanzibari bwana, chao kinakuwa chao wenyewe wala hawatushirikishi, lakini chetu wanataka asilimia 40? Zanzibar kuna watu wasiozidi milioni moja, bara tuna watu milioni 40 halafu watake asilimia 40? Hivi hawa siyo wachawi kweli?
Ninachojua mimi ni kwamba watanzania wote walitangaziwa kuomba hao samaki iwapo wanawahitaji, sasa wenyewe hawakuomba, wanataka wapelekewe? Wao ni akina nani hadi tuwabembeleze hivyo? Sometimes huu muungano ni kero tupu. Uvunjike tu wala hautusaidii. Nichagueni mimi niwe Rais ili niuvunjilie mbali huo muungano.
Vipi wasiombe kulipia 40% ya storage charges!? Wazanzibari bwana!
Hawa jamaa wala siwaelewi....... yaani wao kulalama tuuu....... hiyo storage charge hawaizungumzii kabisaaaa.....!!!!! Mafuta wanataka 100%
Hawa wamezungukwa na maji kila upande, na chakula chao cha kila siku ni samaki, lakini hawaridhiki hadi wawapate hao wa makufuli...huu ni utoto dizaini...huh!
Au watu wa pwani nielezeni, jodari ni mtamu kuliko CHANGU?
Omba Mungu Muungano udumumu ili muendelee kunufaika na vya Bahari Kuu lakini ukivunjika leo tunarudisha mipaka-Please ielewe mipaka ya Tanganyika yako katika Bahari ya Hindi!!!!! Watu wanachojivunia ni Tanzania na siyo Tanganyika na Tanzania haiwezi kuwepo bila nchi Zanzibar. Hivi hujafahamu tu wale wa Maandalizi (Nursery)wanafahamu hivyo.
naomba kufahamu,
Eneo la bahari ambalo ni sehemu ya Zanzibar linafikia asilimia 40?
Una mawazo mgando, kwani hao watu/taasisi waliogawiwa samaki si ni sehemu ya Muungano?Kumbe mna mawazo mgando? Kwani pesa iliyotumika si ya Muungano?
mimi nashauri wapewe samaki woote meli nzima kama watahitaji!binafsi wazenji nimeanza kuwachoka,because THEY ARE TOO DEMANDING
Walianza kumalizana na kushikana uchawi wenyewe kwa wenyewe sasa wameshaeneza sumu mpaka bara.
Nilishasema kuwa ktk kipindi hiki kuna jambo tena la siri linaendelea kupangwa huko zenji kama tusipokuwa makini na hawa wazee wa chaza watakuja na kitu ghafla na tutashindwa pa kutokea.
Muungano kwao si mali kitu tena kwani nje ya muungano wanaweza kutengeneza usultani wa kutawala milele visiwani. hawapendi kupokezana madaraka hawa.
Yangu macho
UNAWEZA KUTUSAIDIA KITU KIMOJA KAKA...!tunaomba wewe au INVISIBLE mui-upload sheria ya muungano hapa!...tunaweza jadili kwa hoja za msingi
Hivi mbona sikuwai kuwasikia toka siku wamekamatwa samaki hawa? iweje leo? ama kweli mchuzi mtamu jaman teh, teh, teh
bila shaka wako tayari kulipia na gharama za utunzaji kwa 40%, au sio ndugu zetu?
waziri Hamza wa zanzibar leo kwenye Tv anasema zanzibar inastahili ipewe share ya 40% kwa sababu sheria inasema hivyo.
jee huu ni mgogoro mwengine ktk muungano?
jamaa anasema waziri magufuli alikuwa anatakiwakae na mwenziwe kabla ya kuamua lkn katumia ubabe kwa hio wao watakaa na waangalie cha kufanya
Halafu Magufuli alisema samaki wataliwa na watanzania sio kuuzwa ila ni zile taasisi zilizopendekezwa yaani magereza, shule, mahospitali n.k au wao Zanzibar sio Watanzaniia mbona hawakupeleka hayo maombi yao basi? Au ndio hivyo kutafuta choko kila kukicha kwa kisingizio cha Muungano?
Walipokamatwa hawakusema, waliposemekana watauzwa hawakusema, kesi iko mahakamani wachangii hata mawazo hata kutoa sifa kwa Magufuli kwa kazi kubwa aliyofanya ya kukamatwa kwa hizo samaki, Taasisi zinazotaka samaki wa bure leteni maombi na muda maalumu umetolewa hatujasikia taasisi za Zanzibar zimepeleka maombi ndio kwanza nasikia wanataka mgao wa 40% kama nani? Zanzibar au Taasisi iliyopo Zanzibar au watanzania wa visiwani au tena ni masuala ya Muungano. Mmh mimi sielewi.
Huu Muungano una kero kweli kweli, ningekuwa na uwezo ningeuvunjilia mbali ili nchi ile cha kwao. Naanza kuona kama vile Mtikila alikuwa sahihi kudai kuwepo kwa taifa la Tanganyika ambayo ingekuwa ni njia nzuri ya kuelekea kuvunja muungano huu.
Baadaye hata Tabora nao watasema ilikuwaje samaki hao waishie Dar tu wakati Tabora nayo ni saehemu ya Tanzania? Hili dai la kutaka mtu atoke Zanzibar aje Dar kujadili swala la matumizi ya samaki wale, kitu ambacho kinaweza kutolewa maamuzi na mtu mmoja kama ilivyotokea ni kuonyesha jinsi gani tunavyopenda kutumia muda na raslimali za serikali vibaya.