Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,413
- 31,403
Sehemu ya I
Bandiko Duru: Hatima ya Muungano na dalili za kuvunjika mapema tulisema bila kura ya maoni na Katiba ,tuna ahirisha tatizo la Muungano kwa muda.
Kuna 'utatu' wa ''Katiba, Muungano na Kura ya maoni'' . Madai ya katiba ni katika eneo la madaraka ya Rais, kuimarisha taasisi na kuzifanya huru, utaguzi wa madaraka na suala la Muungano.
Ukweli, Muungano ni sehemu muhimu ya uandikaji wa katiba, suala lilodumu takribani miaka 60.
Muundo wa Muungano unaacha maswali yasiyo na majibu '' Loose ends'', kuanzia kwa Karume, Aboud Jumbe, G55, Jaji Nyalali, Jaji Kisanga, na kamati zingine ikiwemo maarufu ya Jaji Warioba.
Zaidi ya 75% ya Watanzania walizaliwa baada ya Muungano. Ni kizazi kinachohoji na kina weledi kuliko cha wakati wa Muungano ambacho kilikubali Muungano bila kuhoji ''conventional'
Usahidi wa hoja hii unatolewa na maneno ya Mzee WArioba akisema '' kulikuwa na makundi yaliyotaka muundo wa Muungano wa Serikali 1, Serikali 2, Serikali 3 na Hata kuvunja Muungano'.
Katika makundi aliyotaja Mzee Warioba, ni kundi moja tu lina msimamo wa uhakika, lile la Kuvunja Muungano.
Makundi ya Serikali (S1,S2,S3) yanaonyesha kutaka Muungano yakiwa na misimamo tofauti na hati hati.
Makundi tajwa hapo juu yanatupa swali muhimu lisilotakiwa kuulizwa.
Kizazi cha Muungano Wazee '' conventional'' hakitaki kueleza , kudadisiwa au kuhojiwa.
Ni kizazi kilichokubali Muungano kwa majibu rahisi ' Ni tunu, tuliachiwa na Wazeu, ni Muungano wa kipekee etc''
Linapoulizwa swali la maudhi kilakaulizwa '' Kwanini kusiwepo kura ya Maoni'' kwa Zanzibar kuamua iwapo inataka Muungano au la, kizazi cha Wazee kinaliona swali hilo ni la kihuni, kihaini na kihalifu.
Kizazi cha Wazee kinaamini Muungano usihojiwe na utakuwepo tu ukubalike ''conventinally'.
Ni kizazi kisichoangaalia mabadiliko ya nyakati , watu na mazingira. Hakitaki kusikia kura ya maoni! hivyo tu!!
Kura ya Maoni ni suala linalokamilisha 'utatu' wa Katiba na Muungano.
Mambo hayo 3 huwezi kuyatenga ikiwa nchi inataka suluhu ya kudumu ya aina yoyote ile itakayokubaliwa.
Kuandika katiba inakubaliwa na kila mmoja wetu wakiwemo wahafidhina wa CCM.
Kwa pamoja, watu wanakubaliana katiba iandikwe upya, iwe shirikishi kulingana na matakwa ya nyakati
Kura ya maoni inaepukwa tu kwa hofu ingawa linajulikana ni suala muhimu sana kabla ya kuandika katiba kwani italeta muafaka kwamba nchi mbili zinakubaliana au hazikubaliani.
Katika kukwepa kura ya maoni kuna maswali yanaulizwa, na hakika yanafikirisha.
1. Kwanini iwe Zanzibar?
Ni muda mrefu Zanzibar ikiwa nchi ndogo inalalamika kuonewa na Tanganyika.
Kanuni za asili zinaipa Zanzibar haki ya kura ya maoni ili kutendewa haki.
Ikiwa Tanganyika itashiriki na kuamua uwepo wa Muungano, itathibitisha madai ya Zanzibar kwamba inafanywa koloni kwa ubabe tu.
Si mara ya kwanza kutokea duniani, kanuni zinapipa Zanzibar haki ya kura ya maoni kama ilivyokuwa kule East Timor mwaka 1999 ilipoamua kujitoa Indonesia, au Eritrea 1993 kujitoa Ethiopia, au Quebec Canada 1980 na 1995 kutoka Shirikisho la Canada, na pia Scotland kutoka UK. kwa uchache wa kutaja.
2. Je katiba yetu inaruhusu Kura ya maoni?
Jibu lni rahisi, je mchakato wa kuandika katiba kuanzia Mzee Warioba na kamati ya Mkandala ulifuata sheria au katiba ya sasa? Ni mambo mangapi yanakiukwa katika katiba hii inayolindwa dhidi ya kura ya maoni?
Katiba JMT inapokiukwa na Katiba ya Zanzibar ni sheria gani inafuatwa ?
Je, mgogoro wa Jaji Mkuu kuteuliwa au kuondolewa CAG vilifuata sheria za nchi?
Hoja hii haina maana ya kuhalalisha haramu, ina maana moja kwamba nafasi ya kuanzisha mchakato wa kura ya maoni ipo tena kwa kufuata sheria kama utashi wa kisiasa upo, utashi ule ule unakiuka katiba ya leo
Hoja ya Mwisho ni ya Muungano , suala linalochelewesha katiba, ni mwiba kwasababu watawala hawataki kusikia tofauti na wanavyotaka.
Ni suala lililoua Bunge la Katiba na historia yake si nzuri. Kila jitihada zinafanywa kuliepuka kwa udi na uvumba.
Je, suala la Muungano liangaliwe kwa kutumia darubini gani? Mchakato wa Rasimu ya Warioba?
Rasimu ya CCM ya katiba pendekezwa? au Kamati ya Prof Mkandala?
Waziri husika anasema mchakato wa kuandika katiba utaanza mwezi wa Septemba.
Hakuna anayejua mchato utaanza alipoishia Mzee Warioba au kuna namna tofauti.
Maoni ya Mzee Warioba ndiyo maoni ya Wananchi.
Hakuna chombo au tume nyingine yoyote iliyokuja na maoni shirikishi zaidi ya Tume ya Mzee Warioba.
Kuna hoja potofu eti maoni ya Tume ya Mzee Warioba yamepitwa na wakati.
Ni hoja za kipuuzi sana kwasababu endapo tungekuwa na katiba baada ya Bunge la Katiba, leo tusingeifuta kwa hoja kwamba maudhui yake yamepitwa na wakati.
Jitihada za kuua maoni ya Tume ya Mzee Warioba zinafanywa kwa kutumia chombo mbdala '' Kamati ya Prof Mkandala' iliyoundwa kumshauri Mh Rais lakini si shirikishi wala si ya kikatiba.
Kamati ya Prof Mkandala na uwepo wa Tume ya Haki jinai chini ya Jaji Chande na kutangazwa na Msajili wa vyama mchakato wa Tume huru ya uchaguzi kunaeleza kitu komoja, suala la kuandika katiba halipo.
Kilichopo ni kuweka viraka katiba ya 1977 kwa kisingizio kwamba mambo muhimu yameshughulikiwa na Tume husika hakuna haja ya kufumua katiba iliyopo. Yote yanAtokea kwasababu tu ya kukwepa suala la Muungano.
Itaendelea