Rufaa ya Godbless Lema

Ni jambo jema kama kashinda rufaa yake hongera sana Kamanda Lema...jipange kurudi bungeni.

Ingalikuwa hivyo usingalioneka hapa, mbona kwenye ile hoja ya ccm yadoda Kigoma jana hujatoa maoni! Au unaogopa picha ya Wasira?
 
Asante PJ kwa hii taarifa tuondokane na uzushi.

Kweli na mimi nilikutana naye asubuhi akipandisha mjini kutokea njiro akiwa kafunga bendera kwenye gari nikafikiri anaelekea mahakamani. Asante kwa kutujuza hata hivyo nilimpigia simu mara mbili ili kupata uhakika akiwa bise.
 
Ni jambo jema kama kashinda rufaa yake hongera sana Kamanda Lema...jipange kurudi bungeni.

Hahaaaaa!!!!! Mkuu Ritz Lema akirudi bungeni yule mamako atakuwa na maumivu ya kichwa kila mara!
Lema akirudi bungeni mamako lazima aone period tena!
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: SMU
Sheikh Ubwabwa,

Mkuu wangu taarifa nilizonazo ni kwamba kesi yake imekidhi matakwa ya kusikilizwa na mahakama ya rufaa kinachofuata ni kusubiri kupangiwa majaji watatu kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za wakili wa Bwana Lema na mapitio ya hukumu yenyewe.Ni wazi hiyo ni hatua kubwa sana wadau wa washeria wanajua hilo na wanaweza kuja hapa kutoa darsa.

Ingawa mimi si mwanasheria lakini knowledge ndogo niliyoipata wakati nasoma [Business law] inatosha kubashiri matokeo ya hukumu ya mahakama ya rufaa itakavyokuwa.

[1] Bwana Lema kafungiwa kutogombea.

Maoni yangu kifungu kilichotumika kumnyima fursa ya kugombea hakina uhusiano na makosa ya Bwana Lema kwa mujibu wa hukumu yenyewe.Bwana Lema hakukutwa na makosa ya kutoa rushwa kwa maana hiyo basi nategemea mahakama ya rufaa itatupilia mbali hoja ya kumfungia.

[2] Ushindi wa walalamikaji [Makada wa CCM

Hoja za makada wa CCM ni kukashifiwa kwa mgombea wao Dr Batilda Buriani hali iliyosababisha mgombea wa chama chao kushindwa.
Maoni yangu ni kama ifuatavyo.
[a] Muathirika mkubwa katika kesi hii ni Dr Batilda Buriani inashangaza sana kama siyo kidogo muathirika mkuu hakutokea mahakamani kuthibitisha,kuonyesha mahakama jinsi alivyozalilishwa na hatimaye kupelekea kushindwa.Natarajia Mahakama ya rufaa itazingatia suala hili na pengine kutupilia mbali ushindi wa makada wa CCM.

Natarajia wakili wa makada wa CCM atakumbana na wakati mgumu wa kuwashawishi majaji wa mahakama ya rufaa ni kwanini shahidi muhimu hakufika mahakamani.Pengine majaji wa mahakama ya rufaa watahoji ni kwanini Dr Batilda mwenyewe hakumshitaki Bwana Lema na badala yake wanajitokeza watu wengine ambao hawakukashifiwa kwa namna yoyote ndiyo wabebe dhamana ya kufungua mashtaka ?.

Ukitazama kwa makini mazingira ya kesi hii utabaini viongozi wa CCM hawakujipanga kisawasawa kushinda kesi hii pasipo kutumia udhaifu wa mahakama au jaji ukipenda.

NB:Mtazamo wangu kuhusiana na Bwana Lema haujabadilika hata kidogo lakini hiyo hainifanyi niache kusema ukweli.
 
Ngongo you Nailed it. kama Watanzania wengi bila kujali itikadi za vyama wala tofauti yako na kiongozi fulani tungekuwa tubase kwenye fact kama ulivyodadavuwa basi nchi yetu ingekuwa imepiga hatuwa kubwa sana. binafsi nimekuelewa vizuri sana na ni sawa na mimi msimamo wangu hautobadilika kuhusu Afande Sele kwamba kamwe hafai kuwa Mbunge kupitia chama chochote kile.
 
Last edited by a moderator:

Ukitazama kwa makini mazingira ya kesi hii utabaini viongozi wa CCM hawakujipanga kisawasawa kushinda kesi hii pasipo kutumia udhaifu wa mahakama au jaji ukipenda.

Ujaji wake si ule aliousemea Tundu bungeni!
 
Sheikh Ubwabwa,

Mkuu wangu taarifa nilizonazo ni kwamba kesi yake imekidhi matakwa ya kusikilizwa na mahakama ya rufaa kinachofuata ni kusubiri kupangiwa majaji watatu kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za wakili wa Bwana Lema na mapitio ya hukumu yenyewe.Ni wazi hiyo ni hatua kubwa sana wadau wa washeria wanajua hilo na wanaweza kuja hapa kutoa darsa.

Ingawa mimi si mwanasheria lakini knowledge ndogo niliyoipata wakati nasoma [Business law] inatosha kubashiri matokeo ya hukumu ya mahakama ya rufaa itakavyokuwa.

[1] Bwana Lema kafungiwa kutogombea.

Maoni yangu kifungu kilichotumika kumnyima fursa ya kugombea hakina uhusiano na makosa ya Bwana Lema kwa mujibu wa hukumu yenyewe.Bwana Lema hakukutwa na makosa ya kutoa rushwa kwa maana hiyo basi nategemea mahakama ya rufaa itatupilia mbali hoja ya kumfungia.

[2] Ushindi wa walalamikaji [Makada wa CCM

Hoja za makada wa CCM ni kukashifiwa kwa mgombea wao Dr Batilda Buriani hali iliyosababisha mgombea wa chama chao kushindwa.
Maoni yangu ni kama ifuatavyo.
[a] Muathirika mkubwa katika kesi hii ni Dr Batilda Buriani inashangaza sana kama siyo kidogo muathirika mkuu hakutokea mahakamani kuthibitisha,kuonyesha mahakama jinsi alivyozalilishwa na hatimaye kupelekea kushindwa.Natarajia Mahakama ya rufaa itazingatia suala hili na pengine kutupilia mbali ushindi wa makada wa CCM.

Natarajia wakili wa makada wa CCM atakumbana na wakati mgumu wa kuwashawishi majaji wa mahakama ya rufaa ni kwanini shahidi muhimu hakufika mahakamani.Pengine majaji wa mahakama ya rufaa watahoji ni kwanini Dr Batilda mwenyewe hakumshitaki Bwana Lema na badala yake wanajitokeza watu wengine ambao hawakukashifiwa kwa namna yoyote ndiyo wabebe dhamana ya kufungua mashtaka ?.

Ukitazama kwa makini mazingira ya kesi hii utabaini viongozi wa CCM hawakujipanga kisawasawa kushinda kesi hii pasipo kutumia udhaifu wa mahakama au jaji ukipenda.

NB:Mtazamo wangu kuhusiana na Bwana Lema haujabadilika hata kidogo lakini hiyo hainifanyi niache kusema ukweli.
Leo unazi umeuweka pembeni...Hongera sana bado tutaunganisha nguvu zetu kwenye swala la pensheni zetu.
 
Mkuu Crashwise

Hakika mimi si miongoni mwa wanazi wa chama chochote mara nyingi nasimamia ukweli na si vinginevyo.

Leo unazi umeuweka pembeni...Hongera sana bado tutaunganisha nguvu zetu kwenye swala la pensheni zetu.
 
Last edited by a moderator:
Taarifa nilizonazo ni kwamba rufaa ya Lema imekubaliwa kusikilizwa, sasa ndiyo itapangiwa majaji na tarehe ya kusikiliza.
*Habari ya kushinda kesi ni imagination Sheikh Ubwabwa.

stand to be corrected!*

Kama ni kweli basi wameamua kutoa taarifa hizi basi ni muendelezo uleule wa kuziba midomo. Rufaa inapopelekwa mahakamani ni lazima isikilizwe, si suala la choice unless kuwe kuna technicalities. Hawa watu kusema imekubalika na itapangiwa majaji ni kutaka kumfanya Lema aache kumshambulia yule bwana aliye toa amri kwa Lwakibarila kutokea magogoni kuwa Lema awekwe pembeni kwa vyovyote ili kumkomoa hata kama utetezi wake una nguvu.

Kwa kuwa Lema amekuwa akipita kueleza umma ukweli juu ya yeye kung'olewa ubunge kwa zengwe lwa JK majukwaani, taarifa hii ina lengo la kumfanya asiendelee kuongelea suala lililo mahakamani mpaka August 2015 watakapotoa hukumu.
 
Mkuu Tukundane au ukipenda tupendane mahakama ya rufaa hakuna nafasi ya kupindisha mambo mara nyingi wanakaa majaji watatu kesi ikivurugwa na mahakama za chini ikifika stage hii tegemea haki kuchukua mkondo wake.

Ukisoma hukumu ya mahakama kuu utagundua Lema hakuwa guiltlessness isipokuwa plaintiff hawakujipanga pengine walitegemea zaidi udhaifu wa jaji....

Hawakujua Defendant alikuwa na option nyingine ya kukata rufaa au waliridhika na mafanikio ya muda mfupi na pengine mashinikizo toka muhili mwingine.

Naona unamtabilia ushindi na atashinda kweli safi sana.
 
Lema hawezi kushinda kesi hii. Sanasana atafungiwa kugombea cheo chochote katika siasa za Tanzania.
 
Katika watu ambao tunamfunda Lema ni Ritz na Mkuu Ngongo baadhi ya Pro-Chadema JF wanaona kama tuna uadui na Lema hapana..

Chadema wakijipanga vizuri kwenye rufaa yao na jopo lao la wanasheria wanaweza kumrudisha Lema bungeni...Lema anatakiwa kubadilika angalie kauli zake mambo ya kukakaa juu ya bonet la gari huku gari linakwenda mwendo kasi ni uhuni...
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom