Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,017
- 144,373
Siku chache zilizopita, nilileta mada hapa niki-suggest Mbowe aacha kujitetea mbele ya hizi mahakama zetu kutokana na mwenendo mzima wa hii kesi. Leo hii kupitia You tube, nimemsikia Godbless Lema akimshauri Mbowe aondoe mawakili na akae kimya mahakamani ili wafanye kile wanachokita. Lema pia kaongea na katibu mkuu wa chama na anapanga kuongea na makamu mwenyekiti wa chama kuhusu jambo hili. Isitoshe, Lema kakumbusha uamuzi wa mke wake kutoa mawakili wakati ule wa kesi ya yake alipokuwa ananyimwa dhamana.
Katika kufafanua, Lema kataja mapungufu kadhaa yanayoonekana katika hii kesi na mfano mmojawapo ni Jaji kutumia mawazo yake(opinion) kufanya maamuzi badala ya kutumia vifungu vya sheria katika kuamua mapingamizi. Mbali na kutaja mapungufu yanayojitokeza, Lema anahoji kama katika hatua hizi za mwanzo taratibu zinakikuwa, tunatarajia kweli hukumu itakuwa fair?(swali la msingi sana hili).
Binafsi naungana na Lema kuwa kuna umuhimu wa kuondoa mawakili na Mbowe akae kimya mahakamani tuwaache wafanye wanalotaka kufanya. Hapa tunarudia kosa lilelile la kuwa wagumu kufanya maamuzi kama tulivyofanya kwenye kususia chaguzi zinazoendeshwa na hii tume ya uchaguzi isiokuwa huru. Na hapa niwaambie tu, wakifanikiwa kumfunga Mbowe halafu tukalalamika kuwa taratibu zilikiukwa, majibu yao(MATAGA) yatakuwa mawili: (1) kwanini hamkujitoa (2)Mkakate rufaa kama hamridhiki na maamuzi ya mahakama.
Kuhusu hili la kusubiri kwenda Mahakama ya Rufaa kupinga kitachoamuliwa, naungana pia na Lema kupinga hoja hii kwani hata hao Majaji wa Mahakama ya Rufaa upatikanaji wao ni ule ule wa kuteuliwa na Raisi,hivyo bado lolote linaweza kutokea. Kwahiyo, nashauri viongozi wa CHADEMA na wana familia ya Mbowe watafakari upya kama ni sahihi kuendelea kuweka mawakili mahakamani au Mbowe akae kimya na awaache waamue wanavyoona inafaa.