Mapungufu 21 katika Miswada Sheria ya Taifa ya Tume ya uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Tayari Bungeni limesoma miswada hii kwa mara ya kwanza Novemba hii ,hivyo kutoa fursa kwa wananchi,vyama vya siasa,wadau na wana demokrasia kuchambua ,kujadili na kubainisha maeneo yenye upungufu kabla ya Januari/ Februari 2024 ambapo itasomwa kwa mara ya pili.

Ni muhimu sana Wananchi wote ,wadau , vyama vya siasa kutumia muda wetu kubainisha mapungufu katika miswada hii kuliko kuishia kulalamika tuu kwamba hakuna kilichofanyika ,ni fursa yetu kutumia muda huu kuonesha mapungufu na tupaze sauti Bunge lisikie na Serikali isikie mapungufu yaliyopo ili yapatiwe marekebisho kabla miswada hii kupitishwa.

Nimejiaribu kupitia maeneo kadhaa machache yenye upungufu katika miswada miwili ,Muswada wa Sheria ya Tume ya uchaguzi na muswada wa Sheria ya uchaguzi.

A. Muswada wa Sheria ya Tume ya uchaguzi

Muswada wa Sheria ya Tume ya uchaguzi imetungwa kwa mujibu wa katiba ya 1977 ibara ya 74(1) inayozungumzia uwepo wa Tume ya uchaguzi. Sheria hii ina mapungufu kadhaa.

1. Kifungu cha 7(1) cha Muswada wa Tume ya uchaguzi
Kifungu hiki kimetaja sifa ya Mwenyekiti wa Tume na Makamu Mwenyekiti (awe Jaji wa Mahakama kuu au Mahakama ya Rufani /Wakili miaka 10. Kifungu cha 7(2) kimetaja sifa za wajumbe wa Tume .

Upungufu.

Kifungu hakija taja sifa ya kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa au kiongozi wa chama cha siasa . Sheria ilipaswa iguse na kuweka Sharti hili kama ilivyoainishwa kwenye katiba ibara ya 74(3)d. Tumekuwa na majaji wengi ambao ni makada wa chama. Kutokuweka kifungu hiki ni kutengeneza mwanya,haitoshi kusema Mjumbe wa Tume awe Raia muaminifu bila kuweka Sharti la kutokuwa mwanachama au kujihusisha na chama cha siasa.Ni kama kuruhusu wajumbe wa Tume wakatumikie vyama vyao na kutii maagizo ya vyama vyao.

2. Kifungu cha 9(3) cha Muswada wa Tume ya uchaguzi. , Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu wa Kamati ya Usaili ,Kamati yenye jukumu la kufanya Usahili wa wajumbe wa Tume ya uchaguzi na kupendekeza kwa Rais majina .
Ukisoma tena kifungu cha 18(1) kinasema,kutakuwa na Mkurugenzi wa uchaguzi atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya uchaguzi.

Mapungufu

Kipi kinaanza ?, sababu Tume ya uchaguzi inayompendekeza Mkurugenzi wa uchaguzi kwa Rais upatikanaji wa Tume hiyo unatokana na Kamati ya Usaili ambaye Mkurugenzi wa uchaguzi ni katibu wa Kamati hiyo ya Usahili . Kipi kinaanza ? . Mkurugenzi wa uchaguzi katokea wapi kuwa Katibu wa Kamati ya Usahili kabla ya Tume ya uchaguzi kupatikana na kumpendekeza kwa Rais kwa uteuzi? . (Swali hili ni sawa na swali la Yai na Kuku kipi kilianza?. ).

Ushauri
Nakubaliana na mapendekezo ya Mwanaharakati wa Demokrasia,katiba na Haki za Binadamu ndugu. Deus Kibamba anaposema kuna paswa kuwe na chemba mbili ndani ya Tume ya uchaguzi yaani Bodi na Menejimenti. Mwenyekiti wa Bodi awe Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ambapo Bodi ndio itapaswa kufanya mchakato wa kuajiri Mkurugenzi wa Tume kwa mchakato wa wazi ,watu kuomba na sio lazima Mkurugenzi wa uchaguzi atokane na watumishi wa umma kama ilivyoainishwa kwenye Muswada wa Sheria ya uchaguzi kifungu cha 8(1)(2).

Huyu Mkurugenzi ndio atakuwa Mtendaji Mkuu na ataongoza Menejimenti katika utendaji wa kila siku .Kwa sababu Mkurugenzi wa uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 20(1)(3) muswada wa Tume ya uchaguzi ndio mtendaji Mkuu wa Tume na msimamizi Mkuu ,na anaweza kukasimishwa majukumu na Tume kwa mujibu wa kifungu cha 11(2) cha muswada wa Tume ya uchaguzi.

Hivyo Bodi ya Tume ya uchaguzi ndio inapaswa kumsimamia Mkurugenzi na Menejimenti yake (Dhana ya Principal- Agency Model au Principal -Agent Model). Kifungu cha 9(3) cha Muswada wa Tume ya uchaguzi kifutwe , Mkurugenzi hapaswi kuwa Katibu wa Kamati ya Usaili , kufanya hivyo ni vigumu Tume itakayopatikana kumsimamia.

3.Kifungu cha 21(1) Muswada wa Tume ya uchaguzi

Mtumishi aliyeteuliwa ,aliyeazimwa na Tume katika kipindi cha kutekeleza majukumu yake atachukuliwa kama Mtumishi wa Tume.

Mapungufu.

Ni jambo la kushangaza Tume ya uchaguzi kuendelea kuazima watumishi. Na hili limejidhihirisha wazi kwenye muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi Kifungu cha 6 (1) kinachotaja Wakurugenzi wa Jiji,Manispaa,Miji , Halmshauri atakuwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo na kata . Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu imeshatoa hukumu Mwezi Juni 2023 katika kesi iliyofunguliwa na Mwanaharakati Babu Chacha Wangwe kuzuia Wakurugenzi wa Halmshauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi na Mahakama ilitoa miezi 12(Mwaka mmoja ) kwa serikali kufanya Marekebisho ya sheria ya uchaguzi.

Hawa Wakurugenzi ni makada wa CCM ,hawana uhalali wa kusimamia chaguzi zetu . Ni hoja dhaifu na isiyo na mashiko kusema uwanachama wao unaondoka kupitia Muswada wa Sheria ya Uchaguzi Kifungu cha 6(6) kwamba atajivua uwanachama wake kwa kula kiapo mbele ya hakimu. Miaka yote hawa wamekuwa wakila viapo ila wamekuwa wakisaidia chama chao na Mwenyekiti wa chama chao ambaye ndio mteule wao.

Wakurugenzi wa Halmshauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi itafanya uchaguzi kuvurugika ,sababu Tume yenyewe haiwezi kumuwajibisha Mkurugenzi wa Halmshauri ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi kwa sababu , Mamlaka ya uteuzi na nidhamu ni Rais wa JMT ambaye ni Mwenyekiti wa chama chake ,hivyo MaDED hawawezi tenda haki na usawa. kifungu hiki kurekebishwe.

Ushauri
Tume ya uchaguzi iajiri watumishi wake ngazi ya kila Wilaya kwa ajira za muda na kudumu ,ajira zitangazwe watu waombe kwa Uwazi ,Usahili ufanyike na iachane kutumia Wakurugenzi wa Halmshauri.Pia Tume ya uchaguzi iwe na Ofisi zake kila Mkoa na Wilaya.

4. Kifungu cha 22 cha muswada wa sheria ya Tume ya uchaguzi, kinazungumzia Fedha za uendeshaji wa shughuli za Tume zitatoka katika bajeti ya Serikali yaani chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Ndio wapange waipe shilingi ngapi Tume na lini waiombee fedha Tume kutoka Mfuko wa hazina. Hii haifai na inadhoofisha uhuru wa Tume ya uchaguzi katika kutekeleza majukumu yake.

Ushauri

Fedha ya kuendesha shughuli za Tume zitoke kwenye Mfuko Mkuu wa serikali (Consolidated Fund) ,ambapo ni fedha zenye uhakika,zenye taratibu nzuri na ambazo haziguswi zikiingizwa huko . Kuliko sasa Tume ya uchaguzi kupewa fedha kama hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

5.Kifungu cha 23, Muswada wa Sheria ya Tume ,kinasema Tume itashauriana Waziri wa masuala ya Utumishi ,kuandaa muundo wa Utumishi wa Sekretariati ya Tume ,kifungu hiki wazi wazi kinaonesha Tume kuendelea kupokea maagizo na kuingiliwa na idara zingine za serikali. Uhuru huo upo wapi?. Hii ni kinyume na kifungu cha 6(1) cha muswada wa Tume ya uchaguzi.

6.Kifungu cha 8(2)(i)( ii) na (3),Muswada wa Tume ya uchaguzi kinatoa mamlaka ya Rais kumuondoa Mjumbe wa Tume ya uchaguzi baada ya kushauriwa na Kamati ya uchunguzi. Mapungufu yapo kwenye sababu za kumuondoa huyo Mjumbe, imetaja kutokuwa na uwezo kutekeleza majukumu yake sababu ya maradhi au Sababu nyingine yeyote Sababu nyingine yeyote ndio sababu gani? , imetaja tena tabia mbaya ,tabia mbaya nini ?. Tafsiri ya tabia mbaya anatoa nani? Sababu ni neno ambalo ni Subjective, kila mtu ana tafsiri yake . Mjumbe anaweza kuwa na misimamo dhidi ya wengine katika kutenda haki na usawa akaambiwa ana tabia mbaya.Hivyo uhuru wa wajumbe ukitikisika tafsiri yake Tume haiwezi kuwa huru,ulinzi kwa watumishi wa Tume (Security of Tenure) ni muhimu sana.

B.Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya uchaguzi..

1.Sheria hii inakuja kufuta sheria ya uchaguzi wa udiwani Sura 292 na Sheria ya uchaguzi sura 343 .(Sheria ya uchaguzi ya Mwaka 1985 na sheria ya uchaguzi serikali ya mtaa No.4 ya 1979).

Mapungufu

Sheria hii ilipaswa iingize pia uchaguzi wa serikali ya mtaa ,yaani kuwe na sheria moja ya Uchaguzi wa Urais , Ubunge , Udiwani na Serikali ya mitaa.

Kwasababu uchaguzi wa serikali ya mtaa(Neighborhood Election), hauna sheria bali kanuni ambazo Waziri wa TAMISEMI amepewa mamlaka kuzitunga chini ya Sheria ya Serikali ya Mtaa (Mamlaka ya Miji) sura 288 na Sheria ya Serikali ya mitaa (Mamlaka ya Wilaya ) sura 287 (R.E 2019),kanuni hizo za uchaguzi serikali ya mtaa zinatungwa na Waziri wa TAMISEMI bila ulazima wa kuchukua maoni ya wadau wa vyama vya siasa au kushirikisha.

Ushauri.

Kulipaswa kuwe na sheria moja ya Uchaguzi,Urais, Ubunge, Udiwani na Serikali ya Mtaa chaguzi zote zisimamiwe na Tume ya uchaguzi na sio TAMISEMI (Uchaguzi Serikali ya mtaa).

2.Kama nilivyogusia juu, kifungu cha 6(1) cha muswada wa sheria hii ya uchaguzi, bado sheria na Tume ya uchaguzi inaendelea kuwatambua Wakurugenzi wa Halmshauri kusimamia chaguzi.

Ushauri

Hawafai kusimamia chaguzi,ni makada wa CCM , Hawawezi kuwajibishwa na Tume wakifanya makosa,sababu mamlaka ya uteuzi na nidhamu hayapo kwa Tume ya uchaguzi bali kwa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM .

3. Sheria hii imeendelea kuweka Zuio kwa asiyeridhika na Maamuzi ya Tume kutokwenda Mahakamani. (Finality Clauses , Exclusionary Clauses ,Ouster Clauses). Kwamba maamuzi ya Tume ndio ya Mwisho . Hii ipo kwenye uteuzi wa Mgombea wa Urais. Kifungu cha 37(6) cha muswada wa sheria ya uchaguzi. Ikiwa Tume ikikataa uteuzi wa Mgombea wa Urais , maamuzi ya Tume ndio ya Mwisho hakuna rufaa . Pia kifungu cha 137 ya muswada huu wa sheria ya uchaguzi ,kifungu hiki kinakataza Matokeo ya Urais kupingwa Mahakamani isipokuwa Ubunge tuu.

Vifungu hivi juu vya muswada wa sheria hii ya uchaguzi , msingi wake upo kwenye katiba ya 1977 ibara ya 74(12) na 41(7) ibara hizi zinapinga Matokeo ya Urais kuhojiwa Mahakamani na Tume kutoshtakiwa Mahakamani .

Uhuru wa Tume ya uchaguzi msingi wake ni uwajibikaji, kuzuia Matokeo kupingwa Mahakamani au Tume kushtakiwa tafsiri yake Uwajibikaji hauwezi kuwepo.Watumishi wa Tume wanaweza kutenda makosa kwa uzembe au makusudi wakiamini hawawezi kuwajibishwa kwa uzembe na makosa yao

Lakini pia ,ni kinyume pia na Katiba ya 1977 ibara ya 107 (A) inasema Mahakama ndio chombo cha maamuzi ya mwisho katika utoaji haki ndani ya JMT. Pia ibara ya 13(6a) ya katiba inatoa fursa kwa mtu ambaye hajaridhika na maamuzi kutafuta haki yake Mahakamani.

Huyu Rai anayetafuta haki yake kwa amani kwa njia ya Mahakama anazuiwa kwenda Mahakamani, watawala wanataka haki yake akaitafute Msituni ? . Huu ndio mwanzo wa machafuko. Haki na mifumo imara ya Demokrasia hudumisha amani.Francis Fukuyama katika kitabu chake " End Of History and Last Man (1992)" anasema nchi yenye misingi imara ya Demokrasia haingii katika machafuko, Pia Emmanuel Kant anathibitisha hili kupitia dhana yake ya Democratic Peace Theory -Perpetual Peace.(1795).

Ndio maana madai ya chama chetu ,TCD ,wadau na Wananchi wengi tunasema ni muda muafaka sasa kufanyia marekebisho madogo katiba ya JMT 1977 (Minimum Reforms). Katika ibara zinazohusu chaguzi hasa ibara ya 74(12) na 41(7) huku mchakato wa Katiba Mpya ukipaswa kuanza sasa. Bila marekebisho haya , hakuna Tume huru wala uchaguzi huru utakaotokea.

4.Tume ya uchaguzi haiwezi kuwa huru kama itaendelea kuazima azima watumishi wa Umma,katika muswada huu wa sheria ya uchaguzi kuna vifungu vingi kama 6(2),6(4) vimeipa mamlaka Tume ya uchaguzi kuteua watumishi wa Umma kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kiuchaguzi. Swali la kujiuliza sifa za watumishi hao ni zipi , uadilifu wao ni upi?. Watu waombe ,wateuliwe kwa sifa kuliko kutumia watumishi wa umma.

5.Kifungu cha 14 (1) na 85(1) cha muswada huu wa sheria ya uchaguzi, kinazuia mtu kupiga kura katika eneo ambalo hakuandikishwa . Kuna haja ya nchi yetu kwenda na kasi ya teknolojia ,mtu aruhusiwe kupiga kura popote. Hii ndio inachangia idadi ndogo ya watu kupiga kura (low voter turnout).

6.Mtu kukosa sifa ya kuandikishwa kupiga kura . Kifungu cha 10(1)C cha muswada wa sheria ya uchaguzi kifungu Kinazuia mtu aliyetiwa hatiani kwa kifungo kinachozidi miezi 6 na kifungu cha maisha kupiga kura . Hii ni kinyume kabisa na ibara ya 5(1) na 21 ya Katiba 1977 ya JMT ,ibara hii inatoa fursa kwa mtu aliyefikisha umri wa miaka 18 kupiga kura. Lakini pia kuna kesi no. 3 ya 2022 iliyofunguliwa na Mwanaharakati Ndug.Tito Magoti chini ya Jaji Elinaza Luvanda kupinga kifungu cha sheria ya uchaguzi kinachozuia wafungwa kupiga kura na hukumu ya kesi hii imetoka , Kifungu cha sheria ya uchaguzi kinachozuia wafungwa au mahabusu zaidi ya miezi 6 kuandikishwa kupiga kura kimebatilishwa na Mahakama. Hivyo wafungwa na mahabusu ruhusa kupiga kura.Sababu hata huko Gerezani walipo wanaathirika na siasa na maamuzi ya viongozi huku nje,hivyo ni lazima washiriki kuchagua viongozi wanaona wanafaa.

Sasa kwanini serikali imeendelea kuweka kifungu hiki katika muswada huu wa sheria ya uchaguzi badala ya kutii hukumu ya Mahakama?.

7. Muswada wa sheria ya uchaguzi hii kifungu cha 45(10 ) kinasema mshindi katika uchaguzi wa Urais , Ubunge au udiwani ni aliyepata kura halali nyingi kuliko mwingine. (Winner takes all /Plurality/Post-Past the Post .).

Kuna haja muswada huu wa sheria ya uchaguzi na mabadiliko madogo ya katiba kufanyika ili mshindi wa ngazi ya Urais apate 50.1% . (Majoritarian Electoral System). Ili kuongeza uhalali (Legitimacy) ya ushindi wa kiongozi kutoka kwa Wananchi.

8.Kupotea na kuharibika kwa kadi ya kupiga kura ili kupewa kadi nyingine. Kifungu cha 20(1)(2) cha muswada huu wa sheria ya uchaguzi kinasema ikiwa mtu atapoteza kadi au kadi kuharibika,basi ikithibitishwa na mwandikishaji , mtu huyu atapewa kadi Mpya baada ya kulipa Ada.

Mapangufu

Hakuna haja ya malipo ya Ada ili kupata kadi nyingine ya kupiga kura,hiyo inapaswa kuwa huduma ili kufanikisha Mwananchi kutimiza haki yake ya kupiga kura na kuchagua kiongozi kwa mujibu wa Katiba ibara ya 5 (1) na 21. Kifungu hiki ni informal disfranchisement ya kuzuia mtu kuandikishwa kupiga kura hakifai.

9. Mpiga kura kupata kadi Mpya katika eneo jipya la makazi au kituo cha kupigia kura kipya tofauti na cha awali. Kifungu cha 19(1)(a)(b) ,kinasema mpiga kura huyo aliyehamia eneo jipya tofauti na awali atapewa kadi tuu kama atarudisha kadi ya awali , kama atathibitishwa ni mkazi wa eneo hilo .

Mapungufu

Utaratibu uwe wazi , na vigezo vya kuthibitishwa kama ni mkazi mpya wa eneo viwe wazi , sheria itamke kuwe na barua ya Serikali ya Mtaa huo kumtambulisha pamoja na saini za majirani watatu wa eneo hilo ili kudhibiti asiye mkazi wa eneo hilo kupiga kura au mkazi halali kutozuiwa kupiga kura. Lakini kuna haja ya mifumo yetu iwe ya kisasa kutambua kama mtu ni mkazi wa eneo jipya kwa kuangalia histori ya uandikishwaji wake wa awali aliandikishwa wapi na kadi ya awali ifutwa ili iwe kigezo cha mtu huyo kupewa kadi Mpya bila mlolongo mrefu.

10. Fidia ya pingamizi. Kifungu cha 28(1) hadi (5) cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinazungumzia pingamizi. Mtu anaweza kuweka pingamizi kwa afisa muandikishaji dhidi ya mtu ambaye anakisiwa sio mkazi wa eneo hilo ili asiandikishwe . Kifungu cha 28(5) kinasema baada ya uchunguzi kama afisa muandikishaji kwa maoni yake ataona pingamizi halina msingi ,ataagiza kwa maandishi aliyeweka pingamizi kumlipa fidia ya fedha aliyewekewa pingamizi. Hii sio sahihi ,fidia ya fedha kwanini?. Kuna njama ya kuweka hofu ili wasio na sifa kupiga kura eneo fulani waandikishwe bila kuzuiwa na waenyeji

11. Kukata rufaa Mahakamani kwa dhamana ya fedha. Mtu ambaye hakuridhika na maamuzi ya Afisa muandikishaji,anaweza kwenda Mahakama ya Wilaya kukata rufaa kwa mujibu wa muswada wa sheria ya uchaguzi kifungu cha 30(1) baada ya kulipa kiasi cha fedha kama dhamana, na kifungu cha 30(4) kinasema Mahakama ikiona madai hayakuwa na msingi wowote kiasi cha fedha kama dhamana kilichowekwa kitataifishwa kwa serikali. Kwanini iwe lazima kuwe na dhamana ya fedha katika kupata huduma ya haki ya Mahakama ?. Kifungu hiki hakifai ,kinakeuka katiba ibara ya 107 (A) na ibara ya 13(6 a) ,ibara zina toa uhuru wa mtu kwenda Mahakamani asiporidhika na maamuzi sababu Mahakama ndio chombo cha Mwisho cha utoaji haki.

12.Mgombea kuweka dhamana kwa msimamizi wa uchaguzi.Sheria hii kifungu cha 35(1)(2)na 51(1) muswada wa sheria ya uchaguzi, katika uchaguzi wa Urais , Ubunge hata Udiwani inahitaji mgombea kuweka dhamana ya fedha baada ya uteuzi ,na fedha hizo zitataifishwa ikiwa atapata kura 1/10 ya kura zote halali zilizopigwa. Hii ni kinyume na ibara ya 21(1)(2) ya katiba ya JMT inaruhusu mtu yeyote kushiriki katika masuala ya kiuongozi na maamuzi. Hakuna haja ya kuweka dhamana,kama mtu amepitishwa na chama chake huyo anapaswa kuaminika.

13.Kifungu cha 76(a,b,c) cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinatoa fursa kwa msimamizi wa uchaguzi kuandika orodha ya Wasimamizi wa wasaidizi wa vituo , Je, hao wasimamizi wasaidizi wa vituo wanapatikana namna gani ? . Sababu tumeshudia wengi ni watumishi na makada wa CCM. Kuna haja hata upatikanaji wa wasimamizi wasaidizi wa vituo wapatikane kwa mchakato wa wazi wa kuomba.

14.Kifungu cha 85(5) cha muswada wa sheria ya uchaguzi,kinaruhusu msimamizi wa kituo kutoa amri kumuondoa mtu yeyote kutoka kwenye kituo cha kupiga kura kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Utovu upi wa nidhamu? . Hiki kifungu kinaweza tumika vibaya dhidi ya mawakala wa vyama pinzani . Haya yamewahi tokea kwenye uchaguzi wa Marudio wa Mbarali. Kifungu kisitoe nguvu ya namna hii kwa msimamizi wa kituo ,lakini pia kifungu kioneshe njia ya kumpata wakala mwingine mbadala wa chama ikiwa ni wakala wa chama fulani ndio ameondolewa kwenye kituo.

15. Sheria haijaweka utaratibu wa kumuwajibisha, msimamizi wa uchaguzi Wala msimamizi wa kituo ambaye anakeuka taratibu wakati wa uchaguzi. Kifungu cha 114 kimejikita zaidi adhabu kwa mpiga kura.

Abdul Nondo.
 
Nyie ACT ni sikio la kufa, nyie mnatumika kuhalalisha huu uovu, mnashiriki kwenye hizi chaguzi za maigizo kwa sababu gani? CCM ni wajinga waache kuweka makada wao kwenye tume ya uchaguzi tena wao ndiyo wanatunga sheria? dawa ni katiba mpya ambayo itatoa tume huru ya uchaguzi. ma-DEDs ni makada wa CCM wote wameachwa wasimamie uchaguzi na hakuna kilichobadilika hata kimoja zaidi ya maigizo tupu.
 
Ningejua huyu alie weka bandiko hapa ni kada wa ACT nisinge poteza muda kusoma.
ACT Wazalendo mmekuwa wasaliti wa upinzani muda mrefu.
Haya mapendekezo ya sheria ya uchaguzi mmeshiriki kuya andaa.
Yalipo letwa bungeni mtu wa kwanza kuyasifu ni Zitto.
Ina maana ana jua kila mtego ulio wekwa
ACT mmekuwa mna shirikj kila chaguzi ovu zinazo tokea.
Sasa kwenye hili waacbieni wenye nia njema na Taifa letu
Nyie bakini kwenye kuisindikiza Ccm.
 
Abdul Nondo;
Unaonekana kuandika kwa hisia nzito, za kizalendo, lakini zenye upungufu mkubwa.
Unasema, na hapa ninanukuu, "ni fursa yetu kutumia muda huu kuonesha mapungufu na tupaze sauti Bunge lisikie na Serikali isikie mapungufu yaliyopo ili yapatiwe marekebisho kabla miswada hii kupitishwa." (mwisho wa kunukuu)
Hivi kweli Abdul Nondo, unaamini maneno hayo uliyoandika?
Unaamini kuwa sauti zikipazwa, Wabunge hawa wa CCM watasikia na kurekebisha mapungufu?
Unaamini kuwa ukipaza sauti, Serikali itarekebisha mapungufu ili uwanja wa mashindano uwe huru, sawia na wa haki?
Kama unaamini hivyo, basi ni dhahiri huijui CCM, au wewe ni mshirika wa CCM unayeipambania kuipa uhalali.
 
Abdul mdogo wangu ukitaka kujua chama chenu kimekosa uungwaji mkono soma maoni ya wachangiaji

ACT NI MALI YA CCM HATA UWE MA HOJA KIASI GAN UTAONEKANA NI MADENGE TU

NB: Chama chako walau kikupe usafiri uachane na kujibanza kwenye daladala na kuvaa barakoa kama nesi wasikutumie wakakuacha na umasikin wako kijana au urudi kwenu BUKAVU
 
Una hoja nzuri sana zenye mashiko, lakini kumbuka tuna Bunge la chama kimoja (CCM) mule ndani, hivyo ni wazi maoni ya wananchi, kama haya yako, yataishia kuwekwa kapuni.

Umetimiza wajibu wako wa kutoa maoni, ila ni wakati wa ACT kubadilika na kuacha kabisa kushiriki katika hizi chaguzi zinazoendeshwa kwa kutumia sheria hii mbovu kabisa ya uchaguzi.

Talk the talk and walk the walk.
 
Uchambuzi wako ni mzuri. Tatizo lililopo ni unafiki, uchumia tumbo na ukigeugeu unaowatesa nyinyi wanasiasa wetu.

Imagine leo hii umetoa mapungufu yote haya kuhusu huo muswada!! Lakini ukiitishwa uchaguzi na hiyo hiyo serikali ya ccm; wewe, Kiongozi wako mkuu wa maisha wa chama ndugu Zitto na chama chako cha ACT Wazalendo mnashiriki!! Hovyo kabisa.
 
Ningejua huyu ke weka bandiko hapa i kada wa ACT nisingd poteza muda kusoma.
ACT Wazalendo mmekuwa wasaliti wa upinzani muda mdefu.
Haya mapendekezo ya sheria ya uchavuzi mmeshiriki kjya andaa.
Yalkpo lelekwa bunveni mtu wa kwanza kuyasifu ni Zitto.
Ina maana ana jua kila mtevo jlko wekwa.
ACT mmekuwa mna shirikj kila chavhzi ovu zinalo tokea.
Sasa kwenye bili waacbieni wenye nia njema na Taifa bili.
Nyie bakini kwenye kuisindikiza Ccm.
Mkuu jikite kwenye hoja yake, sio utu, haiba, heshima au tajiriba yake na huo ndio ukomavu kiongozi.

Mkuu wewe pinga, jadiliana, tukana au kataa hoja yake uwezavyo kwa kuainisha sababu na mapungufu ya hoja hiyo, hapo itakuwa sawa.
 
Tayari Bungeni limesoma miswada hii kwa mara ya kwanza Novemba hii ,hivyo kutoa fursa kwa wananchi,vyama vya siasa,wadau na wana demokrasia kuchambua ,kujadili na kubainisha maeneo yenye upungufu kabla ya Januari/ Februari 2024 ambapo itasomwa kwa mara ya pili.

Ni muhimu sana Wananchi wote ,wadau , vyama vya siasa kutumia muda wetu kubainisha mapungufu katika miswada hii kuliko kuishia kulalamika tuu kwamba hakuna kilichofanyika ,ni fursa yetu kutumia muda huu kuonesha mapungufu na tupaze sauti Bunge lisikie na Serikali isikie mapungufu yaliyopo ili yapatiwe marekebisho kabla miswada hii kupitishwa.

Nimejiaribu kupitia maeneo kadhaa machache yenye upungufu katika miswada miwili ,Muswada wa Sheria ya Tume ya uchaguzi na muswada wa Sheria ya uchaguzi.

A. Muswada wa Sheria ya Tume ya uchaguzi

Muswada wa Sheria ya Tume ya uchaguzi imetungwa kwa mujibu wa katiba ya 1977 ibara ya 74(1) inayozungumzia uwepo wa Tume ya uchaguzi. Sheria hii ina mapungufu kadhaa.

1. Kifungu cha 7(1) cha Muswada wa Tume ya uchaguzi
Kifungu hiki kimetaja sifa ya Mwenyekiti wa Tume na Makamu Mwenyekiti (awe Jaji wa Mahakama kuu au Mahakama ya Rufani /Wakili miaka 10. Kifungu cha 7(2) kimetaja sifa za wajumbe wa Tume .

Upungufu.

Kifungu hakija taja sifa ya kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa au kiongozi wa chama cha siasa . Sheria ilipaswa iguse na kuweka Sharti hili kama ilivyoainishwa kwenye katiba ibara ya 74(3)d. Tumekuwa na majaji wengi ambao ni makada wa chama. Kutokuweka kifungu hiki ni kutengeneza mwanya,haitoshi kusema Mjumbe wa Tume awe Raia muaminifu bila kuweka Sharti la kutokuwa mwanachama au kujihusisha na chama cha siasa.Ni kama kuruhusu wajumbe wa Tume wakatumikie vyama vyao na kutii maagizo ya vyama vyao.

2. Kifungu cha 9(3) cha Muswada wa Tume ya uchaguzi. , Mkurugenzi wa Uchaguzi atakuwa Katibu wa Kamati ya Usaili ,Kamati yenye jukumu la kufanya Usahili wa wajumbe wa Tume ya uchaguzi na kupendekeza kwa Rais majina .
Ukisoma tena kifungu cha 18(1) kinasema,kutakuwa na Mkurugenzi wa uchaguzi atakayeteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na Tume ya uchaguzi.

Mapungufu

Kipi kinaanza ?, sababu Tume ya uchaguzi inayompendekeza Mkurugenzi wa uchaguzi kwa Rais upatikanaji wa Tume hiyo unatokana na Kamati ya Usaili ambaye Mkurugenzi wa uchaguzi ni katibu wa Kamati hiyo ya Usahili . Kipi kinaanza ? . Mkurugenzi wa uchaguzi katokea wapi kuwa Katibu wa Kamati ya Usahili kabla ya Tume ya uchaguzi kupatikana na kumpendekeza kwa Rais kwa uteuzi? . (Swali hili ni sawa na swali la Yai na Kuku kipi kilianza?. ).

Ushauri
Nakubaliana na mapendekezo ya Mwanaharakati wa Demokrasia,katiba na Haki za Binadamu ndugu. Deus Kibamba anaposema kuna paswa kuwe na chemba mbili ndani ya Tume ya uchaguzi yaani Bodi na Menejimenti. Mwenyekiti wa Bodi awe Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ambapo Bodi ndio itapaswa kufanya mchakato wa kuajiri Mkurugenzi wa Tume kwa mchakato wa wazi ,watu kuomba na sio lazima Mkurugenzi wa uchaguzi atokane na watumishi wa umma kama ilivyoainishwa kwenye Muswada wa Sheria ya uchaguzi kifungu cha 8(1)(2).

Huyu Mkurugenzi ndio atakuwa Mtendaji Mkuu na ataongoza Menejimenti katika utendaji wa kila siku .Kwa sababu Mkurugenzi wa uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 20(1)(3) muswada wa Tume ya uchaguzi ndio mtendaji Mkuu wa Tume na msimamizi Mkuu ,na anaweza kukasimishwa majukumu na Tume kwa mujibu wa kifungu cha 11(2) cha muswada wa Tume ya uchaguzi.

Hivyo Bodi ya Tume ya uchaguzi ndio inapaswa kumsimamia Mkurugenzi na Menejimenti yake (Dhana ya Principal- Agency Model au Principal -Agent Model). Kifungu cha 9(3) cha Muswada wa Tume ya uchaguzi kifutwe , Mkurugenzi hapaswi kuwa Katibu wa Kamati ya Usaili , kufanya hivyo ni vigumu Tume itakayopatikana kumsimamia.

3.Kifungu cha 21(1) Muswada wa Tume ya uchaguzi

Mtumishi aliyeteuliwa ,aliyeazimwa na Tume katika kipindi cha kutekeleza majukumu yake atachukuliwa kama Mtumishi wa Tume.

Mapungufu.

Ni jambo la kushangaza Tume ya uchaguzi kuendelea kuazima watumishi. Na hili limejidhihirisha wazi kwenye muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi Kifungu cha 6 (1) kinachotaja Wakurugenzi wa Jiji,Manispaa,Miji , Halmshauri atakuwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo na kata . Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu imeshatoa hukumu Mwezi Juni 2023 katika kesi iliyofunguliwa na Mwanaharakati Babu Chacha Wangwe kuzuia Wakurugenzi wa Halmshauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi na Mahakama ilitoa miezi 12(Mwaka mmoja ) kwa serikali kufanya Marekebisho ya sheria ya uchaguzi.

Hawa Wakurugenzi ni makada wa CCM ,hawana uhalali wa kusimamia chaguzi zetu . Ni hoja dhaifu na isiyo na mashiko kusema uwanachama wao unaondoka kupitia Muswada wa Sheria ya Uchaguzi Kifungu cha 6(6) kwamba atajivua uwanachama wake kwa kula kiapo mbele ya hakimu. Miaka yote hawa wamekuwa wakila viapo ila wamekuwa wakisaidia chama chao na Mwenyekiti wa chama chao ambaye ndio mteule wao.

Wakurugenzi wa Halmshauri kuwa wasimamizi wa uchaguzi itafanya uchaguzi kuvurugika ,sababu Tume yenyewe haiwezi kumuwajibisha Mkurugenzi wa Halmshauri ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi kwa sababu , Mamlaka ya uteuzi na nidhamu ni Rais wa JMT ambaye ni Mwenyekiti wa chama chake ,hivyo MaDED hawawezi tenda haki na usawa. kifungu hiki kurekebishwe.

Ushauri
Tume ya uchaguzi iajiri watumishi wake ngazi ya kila Wilaya kwa ajira za muda na kudumu ,ajira zitangazwe watu waombe kwa Uwazi ,Usahili ufanyike na iachane kutumia Wakurugenzi wa Halmshauri.Pia Tume ya uchaguzi iwe na Ofisi zake kila Mkoa na Wilaya.

4. Kifungu cha 22 cha muswada wa sheria ya Tume ya uchaguzi, kinazungumzia Fedha za uendeshaji wa shughuli za Tume zitatoka katika bajeti ya Serikali yaani chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Ndio wapange waipe shilingi ngapi Tume na lini waiombee fedha Tume kutoka Mfuko wa hazina. Hii haifai na inadhoofisha uhuru wa Tume ya uchaguzi katika kutekeleza majukumu yake.

Ushauri

Fedha ya kuendesha shughuli za Tume zitoke kwenye Mfuko Mkuu wa serikali (Consolidated Fund) ,ambapo ni fedha zenye uhakika,zenye taratibu nzuri na ambazo haziguswi zikiingizwa huko . Kuliko sasa Tume ya uchaguzi kupewa fedha kama hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

5.Kifungu cha 23, Muswada wa Sheria ya Tume ,kinasema Tume itashauriana Waziri wa masuala ya Utumishi ,kuandaa muundo wa Utumishi wa Sekretariati ya Tume ,kifungu hiki wazi wazi kinaonesha Tume kuendelea kupokea maagizo na kuingiliwa na idara zingine za serikali. Uhuru huo upo wapi?. Hii ni kinyume na kifungu cha 6(1) cha muswada wa Tume ya uchaguzi.

6.Kifungu cha 8(2)(i)( ii) na (3),Muswada wa Tume ya uchaguzi kinatoa mamlaka ya Rais kumuondoa Mjumbe wa Tume ya uchaguzi baada ya kushauriwa na Kamati ya uchunguzi. Mapungufu yapo kwenye sababu za kumuondoa huyo Mjumbe, imetaja kutokuwa na uwezo kutekeleza majukumu yake sababu ya maradhi au Sababu nyingine yeyote Sababu nyingine yeyote ndio sababu gani? , imetaja tena tabia mbaya ,tabia mbaya nini ?. Tafsiri ya tabia mbaya anatoa nani? Sababu ni neno ambalo ni Subjective, kila mtu ana tafsiri yake . Mjumbe anaweza kuwa na misimamo dhidi ya wengine katika kutenda haki na usawa akaambiwa ana tabia mbaya.Hivyo uhuru wa wajumbe ukitikisika tafsiri yake Tume haiwezi kuwa huru,ulinzi kwa watumishi wa Tume (Security of Tenure) ni muhimu sana.

B.Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya uchaguzi..

1.Sheria hii inakuja kufuta sheria ya uchaguzi wa udiwani Sura 292 na Sheria ya uchaguzi sura 343 .(Sheria ya uchaguzi ya Mwaka 1985 na sheria ya uchaguzi serikali ya mtaa No.4 ya 1979).

Mapungufu

Sheria hii ilipaswa iingize pia uchaguzi wa serikali ya mtaa ,yaani kuwe na sheria moja ya Uchaguzi wa Urais , Ubunge , Udiwani na Serikali ya mitaa.

Kwasababu uchaguzi wa serikali ya mtaa(Neighborhood Election), hauna sheria bali kanuni ambazo Waziri wa TAMISEMI amepewa mamlaka kuzitunga chini ya Sheria ya Serikali ya Mtaa (Mamlaka ya Miji) sura 288 na Sheria ya Serikali ya mitaa (Mamlaka ya Wilaya ) sura 287 (R.E 2019),kanuni hizo za uchaguzi serikali ya mtaa zinatungwa na Waziri wa TAMISEMI bila ulazima wa kuchukua maoni ya wadau wa vyama vya siasa au kushirikisha.

Ushauri.

Kulipaswa kuwe na sheria moja ya Uchaguzi,Urais, Ubunge, Udiwani na Serikali ya Mtaa chaguzi zote zisimamiwe na Tume ya uchaguzi na sio TAMISEMI (Uchaguzi Serikali ya mtaa).

2.Kama nilivyogusia juu, kifungu cha 6(1) cha muswada wa sheria hii ya uchaguzi, bado sheria na Tume ya uchaguzi inaendelea kuwatambua Wakurugenzi wa Halmshauri kusimamia chaguzi.

Ushauri

Hawafai kusimamia chaguzi,ni makada wa CCM , Hawawezi kuwajibishwa na Tume wakifanya makosa,sababu mamlaka ya uteuzi na nidhamu hayapo kwa Tume ya uchaguzi bali kwa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM .

3. Sheria hii imeendelea kuweka Zuio kwa asiyeridhika na Maamuzi ya Tume kutokwenda Mahakamani. (Finality Clauses , Exclusionary Clauses ,Ouster Clauses). Kwamba maamuzi ya Tume ndio ya Mwisho . Hii ipo kwenye uteuzi wa Mgombea wa Urais. Kifungu cha 37(6) cha muswada wa sheria ya uchaguzi. Ikiwa Tume ikikataa uteuzi wa Mgombea wa Urais , maamuzi ya Tume ndio ya Mwisho hakuna rufaa . Pia kifungu cha 137 ya muswada huu wa sheria ya uchaguzi ,kifungu hiki kinakataza Matokeo ya Urais kupingwa Mahakamani isipokuwa Ubunge tuu.

Vifungu hivi juu vya muswada wa sheria hii ya uchaguzi , msingi wake upo kwenye katiba ya 1977 ibara ya 74(12) na 41(7) ibara hizi zinapinga Matokeo ya Urais kuhojiwa Mahakamani na Tume kutoshtakiwa Mahakamani .

Uhuru wa Tume ya uchaguzi msingi wake ni uwajibikaji, kuzuia Matokeo kupingwa Mahakamani au Tume kushtakiwa tafsiri yake Uwajibikaji hauwezi kuwepo.Watumishi wa Tume wanaweza kutenda makosa kwa uzembe au makusudi wakiamini hawawezi kuwajibishwa kwa uzembe na makosa yao

Lakini pia ,ni kinyume pia na Katiba ya 1977 ibara ya 107 (A) inasema Mahakama ndio chombo cha maamuzi ya mwisho katika utoaji haki ndani ya JMT. Pia ibara ya 13(6a) ya katiba inatoa fursa kwa mtu ambaye hajaridhika na maamuzi kutafuta haki yake Mahakamani.

Huyu Rai anayetafuta haki yake kwa amani kwa njia ya Mahakama anazuiwa kwenda Mahakamani, watawala wanataka haki yake akaitafute Msituni ? . Huu ndio mwanzo wa machafuko. Haki na mifumo imara ya Demokrasia hudumisha amani.Francis Fukuyama katika kitabu chake " End Of History and Last Man (1992)" anasema nchi yenye misingi imara ya Demokrasia haingii katika machafuko, Pia Emmanuel Kant anathibitisha hili kupitia dhana yake ya Democratic Peace Theory -Perpetual Peace.(1795).

Ndio maana madai ya chama chetu ,TCD ,wadau na Wananchi wengi tunasema ni muda muafaka sasa kufanyia marekebisho madogo katiba ya JMT 1977 (Minimum Reforms). Katika ibara zinazohusu chaguzi hasa ibara ya 74(12) na 41(7) huku mchakato wa Katiba Mpya ukipaswa kuanza sasa. Bila marekebisho haya , hakuna Tume huru wala uchaguzi huru utakaotokea.

4.Tume ya uchaguzi haiwezi kuwa huru kama itaendelea kuazima azima watumishi wa Umma,katika muswada huu wa sheria ya uchaguzi kuna vifungu vingi kama 6(2),6(4) vimeipa mamlaka Tume ya uchaguzi kuteua watumishi wa Umma kwa ajili ya kutekeleza majukumu ya kiuchaguzi. Swali la kujiuliza sifa za watumishi hao ni zipi , uadilifu wao ni upi?. Watu waombe ,wateuliwe kwa sifa kuliko kutumia watumishi wa umma.

5.Kifungu cha 14 (1) na 85(1) cha muswada huu wa sheria ya uchaguzi, kinazuia mtu kupiga kura katika eneo ambalo hakuandikishwa . Kuna haja ya nchi yetu kwenda na kasi ya teknolojia ,mtu aruhusiwe kupiga kura popote. Hii ndio inachangia idadi ndogo ya watu kupiga kura (low voter turnout).

6.Mtu kukosa sifa ya kuandikishwa kupiga kura . Kifungu cha 10(1)C cha muswada wa sheria ya uchaguzi kifungu Kinazuia mtu aliyetiwa hatiani kwa kifungo kinachozidi miezi 6 na kifungu cha maisha kupiga kura . Hii ni kinyume kabisa na ibara ya 5(1) na 21 ya Katiba 1977 ya JMT ,ibara hii inatoa fursa kwa mtu aliyefikisha umri wa miaka 18 kupiga kura. Lakini pia kuna kesi no. 3 ya 2022 iliyofunguliwa na Mwanaharakati Ndug.Tito Magoti chini ya Jaji Elinaza Luvanda kupinga kifungu cha sheria ya uchaguzi kinachozuia wafungwa kupiga kura na hukumu ya kesi hii imetoka , Kifungu cha sheria ya uchaguzi kinachozuia wafungwa au mahabusu zaidi ya miezi 6 kuandikishwa kupiga kura kimebatilishwa na Mahakama. Hivyo wafungwa na mahabusu ruhusa kupiga kura.Sababu hata huko Gerezani walipo wanaathirika na siasa na maamuzi ya viongozi huku nje,hivyo ni lazima washiriki kuchagua viongozi wanaona wanafaa.

Sasa kwanini serikali imeendelea kuweka kifungu hiki katika muswada huu wa sheria ya uchaguzi badala ya kutii hukumu ya Mahakama?.

7. Muswada wa sheria ya uchaguzi hii kifungu cha 45(10 ) kinasema mshindi katika uchaguzi wa Urais , Ubunge au udiwani ni aliyepata kura halali nyingi kuliko mwingine. (Winner takes all /Plurality/Post-Past the Post .).

Kuna haja muswada huu wa sheria ya uchaguzi na mabadiliko madogo ya katiba kufanyika ili mshindi wa ngazi ya Urais apate 50.1% . (Majoritarian Electoral System). Ili kuongeza uhalali (Legitimacy) ya ushindi wa kiongozi kutoka kwa Wananchi.

8.Kupotea na kuharibika kwa kadi ya kupiga kura ili kupewa kadi nyingine. Kifungu cha 20(1)(2) cha muswada huu wa sheria ya uchaguzi kinasema ikiwa mtu atapoteza kadi au kadi kuharibika,basi ikithibitishwa na mwandikishaji , mtu huyu atapewa kadi Mpya baada ya kulipa Ada.

Mapangufu

Hakuna haja ya malipo ya Ada ili kupata kadi nyingine ya kupiga kura,hiyo inapaswa kuwa huduma ili kufanikisha Mwananchi kutimiza haki yake ya kupiga kura na kuchagua kiongozi kwa mujibu wa Katiba ibara ya 5 (1) na 21. Kifungu hiki ni informal disfranchisement ya kuzuia mtu kuandikishwa kupiga kura hakifai.

9. Mpiga kura kupata kadi Mpya katika eneo jipya la makazi au kituo cha kupigia kura kipya tofauti na cha awali. Kifungu cha 19(1)(a)(b) ,kinasema mpiga kura huyo aliyehamia eneo jipya tofauti na awali atapewa kadi tuu kama atarudisha kadi ya awali , kama atathibitishwa ni mkazi wa eneo hilo .

Mapungufu

Utaratibu uwe wazi , na vigezo vya kuthibitishwa kama ni mkazi mpya wa eneo viwe wazi , sheria itamke kuwe na barua ya Serikali ya Mtaa huo kumtambulisha pamoja na saini za majirani watatu wa eneo hilo ili kudhibiti asiye mkazi wa eneo hilo kupiga kura au mkazi halali kutozuiwa kupiga kura. Lakini kuna haja ya mifumo yetu iwe ya kisasa kutambua kama mtu ni mkazi wa eneo jipya kwa kuangalia histori ya uandikishwaji wake wa awali aliandikishwa wapi na kadi ya awali ifutwa ili iwe kigezo cha mtu huyo kupewa kadi Mpya bila mlolongo mrefu.

10. Fidia ya pingamizi. Kifungu cha 28(1) hadi (5) cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinazungumzia pingamizi. Mtu anaweza kuweka pingamizi kwa afisa muandikishaji dhidi ya mtu ambaye anakisiwa sio mkazi wa eneo hilo ili asiandikishwe . Kifungu cha 28(5) kinasema baada ya uchunguzi kama afisa muandikishaji kwa maoni yake ataona pingamizi halina msingi ,ataagiza kwa maandishi aliyeweka pingamizi kumlipa fidia ya fedha aliyewekewa pingamizi. Hii sio sahihi ,fidia ya fedha kwanini?. Kuna njama ya kuweka hofu ili wasio na sifa kupiga kura eneo fulani waandikishwe bila kuzuiwa na waenyeji

11. Kukata rufaa Mahakamani kwa dhamana ya fedha. Mtu ambaye hakuridhika na maamuzi ya Afisa muandikishaji,anaweza kwenda Mahakama ya Wilaya kukata rufaa kwa mujibu wa muswada wa sheria ya uchaguzi kifungu cha 30(1) baada ya kulipa kiasi cha fedha kama dhamana, na kifungu cha 30(4) kinasema Mahakama ikiona madai hayakuwa na msingi wowote kiasi cha fedha kama dhamana kilichowekwa kitataifishwa kwa serikali. Kwanini iwe lazima kuwe na dhamana ya fedha katika kupata huduma ya haki ya Mahakama ?. Kifungu hiki hakifai ,kinakeuka katiba ibara ya 107 (A) na ibara ya 13(6 a) ,ibara zina toa uhuru wa mtu kwenda Mahakamani asiporidhika na maamuzi sababu Mahakama ndio chombo cha Mwisho cha utoaji haki.

12.Mgombea kuweka dhamana kwa msimamizi wa uchaguzi.Sheria hii kifungu cha 35(1)(2)na 51(1) muswada wa sheria ya uchaguzi, katika uchaguzi wa Urais , Ubunge hata Udiwani inahitaji mgombea kuweka dhamana ya fedha baada ya uteuzi ,na fedha hizo zitataifishwa ikiwa atapata kura 1/10 ya kura zote halali zilizopigwa. Hii ni kinyume na ibara ya 21(1)(2) ya katiba ya JMT inaruhusu mtu yeyote kushiriki katika masuala ya kiuongozi na maamuzi. Hakuna haja ya kuweka dhamana,kama mtu amepitishwa na chama chake huyo anapaswa kuaminika.

13.Kifungu cha 76(a,b,c) cha muswada wa sheria ya uchaguzi kinatoa fursa kwa msimamizi wa uchaguzi kuandika orodha ya Wasimamizi wa wasaidizi wa vituo , Je, hao wasimamizi wasaidizi wa vituo wanapatikana namna gani ? . Sababu tumeshudia wengi ni watumishi na makada wa CCM. Kuna haja hata upatikanaji wa wasimamizi wasaidizi wa vituo wapatikane kwa mchakato wa wazi wa kuomba.

14.Kifungu cha 85(5) cha muswada wa sheria ya uchaguzi,kinaruhusu msimamizi wa kituo kutoa amri kumuondoa mtu yeyote kutoka kwenye kituo cha kupiga kura kwa sababu ya utovu wa nidhamu. Utovu upi wa nidhamu? . Hiki kifungu kinaweza tumika vibaya dhidi ya mawakala wa vyama pinzani . Haya yamewahi tokea kwenye uchaguzi wa Marudio wa Mbarali. Kifungu kisitoe nguvu ya namna hii kwa msimamizi wa kituo ,lakini pia kifungu kioneshe njia ya kumpata wakala mwingine mbadala wa chama ikiwa ni wakala wa chama fulani ndio ameondolewa kwenye kituo.

15. Sheria haijaweka utaratibu wa kumuwajibisha, msimamizi wa uchaguzi Wala msimamizi wa kituo ambaye anakeuka taratibu wakati wa uchaguzi. Kifungu cha 114 kimejikita zaidi adhabu kwa mpiga kura.

Abdul Nondo.

Mnafiki tu. Wakati wengine wanasusia hizo chaguzi kwasababu ya sheria za kijinga nyie mnashiriki na kuhalalisha ujinga. Sasa Leo unalalamika Nini?. Very hypocrite
 
ZITTO KABWE dalali alishiriki kwenye ujinga huu ,Yale Yale ya DPWORLD tutaitwa Ikulu kuna ubwabwa halafu mtapitisha tena
 
Back
Top Bottom