Rufaa ya Godbless Lema

​vipi lusinde na mwigulu ni waadilifu sana ndani ya chama chenu du mna kazi
 
Kweli huu ni mwezi wa haki, Janualy mpaka December watu tungeishi hivi basi ingekuwa raha mustarehe bila kujali suluba za maisha haya mabovu tunayoishi.
 
Katika watu ambao tunamfunda Lema ni Ritz na Mkuu Ngongo baadhi ya Pro-Chadema JF wanaona kama tuna uadui na Lema hapana..

Chadema wakijipanga vizuri kwenye rufaa yao na jopo lao la wanasheria wanaweza kumrudisha Lema bungeni...Lema anatakiwa kubadilika angalie kauli zake mambo ya kukakaa juu ya bonet la gari huku gari linakwenda mwendo kasi ni uhuni...

Mkuu ni Ngongo mara nyingi nimemsoma yupo objective, lakini huyo kwenye red mmhhhh!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Sidhani KAMA TAARIFA hizi ni za kweli!
Nikiwa kunako ofisi yangu muda wa saa 3.00 asubuhi nimekutana na Lema, Ole Milya, na Mawazo wakielekea Airport ambako wanatumia helikopta ya Ndesapesa tayari kwa kwenda Simanjiro, raia wa huko wamewaita wanataka kuhamia Airtel, sorry, CDM!
And so by default value Lema asingeacha rufaa yake inasomwa akaondoka kwenda kupiga M4C!

nimeipenda hii
 
Sheikh Ubwabwa,

Mkuu wangu taarifa nilizonazo ni kwamba kesi yake imekidhi matakwa ya kusikilizwa na mahakama ya rufaa kinachofuata ni kusubiri kupangiwa majaji watatu kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za wakili wa Bwana Lema na mapitio ya hukumu yenyewe.Ni wazi hiyo ni hatua kubwa sana wadau wa washeria wanajua hilo na wanaweza kuja hapa kutoa darsa.

Ingawa mimi si mwanasheria lakini knowledge ndogo niliyoipata wakati nasoma [Business law] inatosha kubashiri matokeo ya hukumu ya mahakama ya rufaa itakavyokuwa.

[1] Bwana Lema kafungiwa kutogombea.

Maoni yangu kifungu kilichotumika kumnyima fursa ya kugombea hakina uhusiano na makosa ya Bwana Lema kwa mujibu wa hukumu yenyewe.Bwana Lema hakukutwa na makosa ya kutoa rushwa kwa maana hiyo basi nategemea mahakama ya rufaa itatupilia mbali hoja ya kumfungia.

[2] Ushindi wa walalamikaji [Makada wa CCM

Hoja za makada wa CCM ni kukashifiwa kwa mgombea wao Dr Batilda Buriani hali iliyosababisha mgombea wa chama chao kushindwa.
Maoni yangu ni kama ifuatavyo.
[a] Muathirika mkubwa katika kesi hii ni Dr Batilda Buriani inashangaza sana kama siyo kidogo muathirika mkuu hakutokea mahakamani kuthibitisha,kuonyesha mahakama jinsi alivyozalilishwa na hatimaye kupelekea kushindwa.Natarajia Mahakama ya rufaa itazingatia suala hili na pengine kutupilia mbali ushindi wa makada wa CCM.

Natarajia wakili wa makada wa CCM atakumbana na wakati mgumu wa kuwashawishi majaji wa mahakama ya rufaa ni kwanini shahidi muhimu hakufika mahakamani.Pengine majaji wa mahakama ya rufaa watahoji ni kwanini Dr Batilda mwenyewe hakumshitaki Bwana Lema na badala yake wanajitokeza watu wengine ambao hawakukashifiwa kwa namna yoyote ndiyo wabebe dhamana ya kufungua mashtaka ?.

Ukitazama kwa makini mazingira ya kesi hii utabaini viongozi wa CCM hawakujipanga kisawasawa kushinda kesi hii pasipo kutumia udhaifu wa mahakama au jaji ukipenda.

NB:Mtazamo wangu kuhusiana na Bwana Lema haujabadilika hata kidogo lakini hiyo hainifanyi niache kusema ukweli.

Good analysis at last! Tutashinda kesi na Lema atarudi bungeni!
 
Vyovyote iwavyo ni faida kwa CDM, akishinda ni vizuri hasiposhinda kitu ya M4C itaendelea kwa kasi zaidi.
 
Ngongo pamoja na kutofautiana na lema leo umenionyesha ukomavu wa siasa na sheria.
Hongera kwa hilo na je unafikiri ikulu iliingilia kesi ya lema kama alivyodai.
 
Mkuu Tukundane au ukipenda tupendane mahakama ya rufaa hakuna nafasi ya kupindisha mambo mara nyingi wanakaa majaji watatu kesi ikivurugwa na mahakama za chini ikifika stage hii tegemea haki kuchukua mkondo wake.

Ukisoma hukumu ya mahakama kuu utagundua Lema hakuwa guiltlessness isipokuwa plaintiff hawakujipanga pengine walitegemea zaidi udhaifu wa jaji....

Hawakujua Defendant alikuwa na option nyingine ya kukata rufaa au waliridhika na mafanikio ya muda mfupi na pengine mashinikizo toka muhili mwingine.

Nimekusoma mkuu.
 
LAKINI NI LINI ITASIKILIZWA?
:yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield::yield:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom