Bull Bucka
Member
- Oct 5, 2023
- 34
- 46
JamiiForums, Jukwaa la Katiba (JUKATA), Tanganyika Law Society (TLS), Twaweza East Africa, Centre for Strategic Litigation (CSL) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwa pamoja tunawasilisha maoni kwenye miswada minne: Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani; Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa na Gharama za Uchaguzi; na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi.
Serikali iliwasilisha miswada hii Bungeni na ilisomwa kwa mara ya kwanza tarehe 10 November, 2023. Kisha Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba imealika wadau kutoa maoni kwenye miswada hiyo kuanzia Januari 6-10, 2024.
Hii ni fursa muhimu sana katika ujenzi wa demokrasia nchini kwetu na kulinda haki muhimu za raia. Tunatambua pia awamu hii miswada hii haikuwasilishwa Bungeni kwa hati ya dharura na hivyo imeongeza muda kwa wadau kuweza kuichambua na kuwasilisha maoni. Kamati ya Bunge imefanya vyema pia kupokea maoni kwa siku kadhaa na kwa njia mbalimbali ili kuwezesha wadau wengi zaidi kuwasilisha maoni yao.
Kwa kuitikia wito huu na katika kutekeleza wajibu wetu wa kikatiba, tunafarijika kuwasilisha maoni yetu ili kuchangia katika kuboresha muktadha wa kisheria utakaowezesha kuimarisha demokrasia nchini kwetu Tanzania. Tunaamini haki na demokrasia ni misingi muhimu sana ya kuwezesha ushiriki wa watanzania wote katika kufikia malengo ya maendeleo.
Katika kila muswada, tunawasilisha maoni ya jumla na maoni mahsusi kifungu kwa kifungu. Maoni ya jumla yanatoa muhtasari wa mambo ya msingi katika kila muswada na maoni mahsusi yanatoa ufafanuzi wa kina wa mapungufu na maboresho katika vifungu vingi.
Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unafanya jambo zuri la kuunganisha sheria mbili za awali na kutengeneza sheria mama ya maswala ya uchaguzi. Hili ni jambo zuri ili kurahisisha rejea ya kisheria. Maoni yetu yamelenga kuboresha utaratibu mzima wa uchaguzi ili kuhakikisha chaguzi zetu ni huru, za haki na za uadilifu. Tunapokuwa na chaguzi huru na za haki inaepusha uvunjifu wa amani na hivyo kuimarisha demokrasia yetu.
Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa unapendekeza mabadiliko kadhaa kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2019. Pamoja na mambo chanya kadhaa ikiwemo kutoa ufafanuzi wa kuboresha maswala ya ujumuishi wa makundi maalum ndani ya vyama, muswada huu hauna mabadiliko makubwa sana katika sheria iliyopo. Na baadhi ya vifungu pendekezwa vinahitaji maboresho kama ambavyo tumebainisha katika uchambuzi wetu ili kuviwezesha vyama vya siasa kutekeleza majukumu yao ya kisiasa bila kukiuka katiba ya nchi yetu na sheria nyinginezo. .
Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi unalenga kuhamasisha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika maswala ya fedha kwa wadau wote wa uchaguzi. Hili ni jambo zuri katika kujenga demokrasia imara yenye uwazi na uwajibikaji wa wadau wote.
Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi unapendekeza kuanzishwa kwa sheria inayojitegemea kuhusu Tume ya Uchaguzi. Sheria hii itatoa ufafanuzi wa kina kuhusu Tume ya Uchaguzi tofauti na ilivyo sasa ambapo Tume imetajwa kikatiba lakinin maelezo yake yamekuwa sehemu tu ya Sheria za Uchaguzi. Maoni yetu yamekusudia kuboresha muundo wa Tume na kuifanya iwe tume huru isiyoingiliwa na mamlaka yoyote katika utekelezaji wa shughuli zake.
Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani
Muswada huu unaunganisha sheria mbili za uachaguzi. Muswada hauna tofauti sana kimaudhui na sheria zilizokuwepo awali isipokuwa baadhi ya mambo mapya yamependekezwa ikiwemo kuiwezesha Tume ya Uchaguzi kukataa jina la mgombea wa chama kwa nafasi tajwa kwa kutumia sababu ambazo zimebainishwa katika muswada huu (Vifungu 36-37).
Uchambuzi wetu umezingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, mapendekezo ya ripoti mbalimbali hasa ripoti za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, maamuzi ya mahakama za ndani na za kikanda pamoja na uzoefu na mifano kutoka nchi nyingine.
Kiujumla, muswada huu unamambo mbalimbali mazuri ikiwemo kuunganisha sheria mbili ambazo ni Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, 1979 kuwa sheria moja.
Maoni ya Jumla
Tunapendekeza…
1. Jina la sheria ijulikane kama Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ambayo itasimamia chaguzi zote na mambo yote yanayohusu uchaguzi nchini.[Kifungu cha 1]
2. Tunapendekeza vifaa vya uchaguzi na miundombinu vizingatie mahitaji ya watu wenye ulemavu.[Kifungu kipya]
3. Tume ibanishe siku mahususi ya uchaguzi “election day” mathalani Jumatano ya Mwisho ya mwezi Oktoba kuwa siku ya uchaguzi.[Kifungu cha 41]
4. Tume iwe na mamlaka ya kuajiri watumishi wake kwenye ngazi zote.[Kifungu kipya]
5. Watu waruhusiwe kupiga kura kwa vitambulisho mbadala vinavyotambulika kisheria. [Kifungu cha 14]
6. Matumizi ya teknolojia yatumike kufanya utambuzi wa wapiga kura kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia “fingerprint.” [Kifungu 166]
7. Fomu ya uteuzi wa mgombea wa ubunge na udiwani umezingatia mahitaji maalum tofauti na fomu ya uteuzi wa mgombea wa nafasi ya urais ambayo haijaweka sharti la fomu hiyo kuzingatia mahitaji maalum. [Kifungu cha 34]
8. Popote kwenye neno “chini ya sheria hii” pafutwe na pasomeke “kwa mujibu wa sheria hii”.
9. Popote kwenye neno “tarehe iliyochaguliwa” pafutwe na pasomeke “tarehe iliyopangwa”.
10. Endapo mpaka siku ya mwisho ya uteuzi hapatakuwa na mgombea au mgombea kajitoa ndani ya saa 24 baada ya muda wa uteuzi kuisha, chama husika kipewe nafasi ya kuteua mgombea mwingine. [Kifungu cha 70 (3)]
11. Kuweka kifungu kitakachoweka wajibu kwa vyombo vya habari vya umma kutokuwa na upendeleo kwa kuwapa fursa sawa wagombea kujinadi. Aidha vyombo vya habari binafsi kuweka muda maalum kwa ajili ya wagombea wote wakati wa kampeni. [Kifungu cha 74]
12. Usikilizwaji wa mashauri ya uchaguzi ukamilike ndani ya siku 90 badala ya miezi 12 kama inavyopendekezwa katika mswada huu. [Kifungu 144 (2)] Na rufaa zikamilike ndani ya siku 60 badala ya miezi 12 kama inavyopendekezwa kwenye muswada huu.
13. Kuwekwa takwa la lazima la uwepo wa midahalo kwa ngazi ya urais mdahalo urushwe mubashara kwenye vyombo vya habari na kwa ngazi ya ubunge na kata midahalo ifanyike katika ngazi husika. [Kifungu kipya]
14. Uwepo wa kifungu kinachoainisha ukomo wa muda wa kutangaza matokeo ya urais, ubunge na madiwani.[Kifungu cha 45, 105, 106]
15. Mtiririko wa vifungu vya muswada huu ufuate mzunguko wa kiuchaguzi “Election Cycle” ili kuleta mantiki na kurahisisha usomaji, yaani uandikishaji, elimu ya mpiga kura, uteuzi wa wagombea, kampeni, upigaji kura, matokeo na mashauri ya uchaguzi.
16. Kuondoa kifungu kanachoweka takwa la kutaifisha dhamana ya mgombea ikiwa hatopata moja ya kumi ya kura zote zilizohesabiwa.[Kifungu cha 51(1)]
17. Mshindi wa nafasi ya urais, ubunge na madiwani wapatikane kwa kura nyingi zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.
18. Kuwe na sura maalum kuhusu “Elimu ya Mpiga Kura na Watazamaji wa Uchaguzi”.
19. Uwasilishwaji wa fomu za uteuzi wa wagombea katika ngazi zote ziwasilishwe kwa njia ya nakala ngumu au tepe. [Kifungu cha 34(2),50(7), 62(7)]
20. Kuondoa kifungu cha 107 (3) kinachopendekeza kuteketeza nyaraka za uchaguzi ndani ya miezi 6 inakinzana na muda wa mashauri ya uchaguzi na Kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Taifa ya Utunzaji wa Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Namba 3, 3002 (The Records and Archives Management Act No.2 of 2002) ambayo inaweka takwa la nyaraka za Taifa kutunzwa ndani ya miaka 30.
21. Nyaraka za uchaguzi zitunzwe kielektroniki.
22. Kurekebisha Kifungu cha 102(1)(e) kirekebishwe kuondoa maneno “iwapo fomu za taarifa za matokeo zipo za kutosha”.
Pia soma: Maoni ya Wadau Kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Muswada wa Vyama vya Siasa - Sehemu 2