Well said mkuu nami naunga mkono hoja though tunarudi kule kwenye msimamo wangu na wajibu wa rais.... hapo kwenye red....Kama wateule hao wa rais hawafanyi kazi zao ipasavyo..je rais anajua?? kama anajua basi hilo ni tatizo kwasababu anaacha watu wasiofaa, wasiojua wajibu wao na ambao hawamsaidii rais.
Kama hajuibasi hilo ni tatizo kubwa zaidi....
Upo Sahihi Mkuu wangu, na ndio maana kwenye post yangu # 15, nilisema hivi: ".....Kilichobaki, na ama kilichokosekana toka kwake yeye binafsi (Rais) na watendaji wengine ni kuchukua hatua stahiki kutokana na reform husika!" Mwisho wa nukuu.
Hivyo basi, hatua stahiki kwa Rais ni hizo ulizotaja wewe! Alitakiwa kujiuliza, kama kila ripoti inaonesha madudu, je TAKUKURU hadi sasa wamechunguza tuhuma ngapi na nini matokeo ya uchunguzi huo. Je, DCI amepiga hatua zipi katika hilo! DPP nae amepeleka kesi ngapi mahakamani hadi ripoti nyingine inatoka! Hapa bila shaka panahitaji sheria iliyopitishwa na bunge kwamba kabla ya ripoti ya pili ya CAG kusomwa, TAKUKURU, DCI na DPP watoe kwanza ripoti ya uchunguzi wao wa ripoti ya nyuma(ya CAG).