Tulia Ackson: Naagiza Serikali ifanye utafiti wa Mapungufu ya Sheria ya Ushoga na Usagaji ili iendane na uhalisia wa sasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 6 leo Aprili 13, 2023 jijini Dodoma.



SERIKALI YAAGIZA NHIF ITOE KIBALI MATUMIZI YA CT SCAN HOSPITALI YA IRINGA
Agizo hilo limetolewa baada Mbunge Jesca Msambatavangu kuhoji Bungeni sababu za wagonjwa wanaotumia Bima ya NHIF katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kutopewa kibali kutumia kadi zao kupata huduma ya CT Scan.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema “Namuagiza DG wa Bima kwamba mpaka kesho saa mbili asubuhi (Aprili 14, 2023) watu wanaostahili na waliotimiza vigezo waanze kupata huduma hiyo.”

MWONGOZO KUHUSU MASUALA YA USHOGA NA USAGAJI NCHINI
Akitumia kanuni ya 76, Mbunge Noah Saputu ameomba mwongozo unaotaka Bunge litoe msimamo wake kuhusu suala la ushoga kwa kuwa Mamlaka zote za Nchi ikiwemo Rais Samia, viongozi wa dini pamoja na taasisi zingine kubwa zimetoa msimamo wa kutokuafikiana na jambo hilo.

Ameomba Muswada utakaoleta Sheria kali uletwe Bungeni haraka ili Bunge liupitishe.

Akijibu hoja hiyo, Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson amesema hoja hiyo imeibuka baada ya hotuba ya Waziri Mkuu kutolewa Bungeni. Amekiri kuwa viongozi wa sekta zote wamelizungumzia na Serikali imeelewa inapaswa kufanya nini.

Amesema wakati mwingine kuyazungumza sana mambo haya inaweza kuwa sababu ya kuyasambaza na kuongeza uharibifu zaidi. Kwa kuwa Tanzania inafuata utawala wa Sheria, Spika Tulia amesisitiza kuwa Tanzania tayari ina Sheria ya Makosa ya Kujamiiana pamoja na Sheria ya Makosa ya Jinai ambazo zote zina vipengele vinavyozungumzia jambo hilo.

Ameiagiza Serikali kufanya utafiti kupitia tume ya kurekebisha sheria ya mambo yapi yaongezeke kwenye Sheria ya kuzuia Ushoga na Usagaji ili kuziba mianya iliyopo sasa. Sheria hiyo inapaswa kutungwa kwa uhalisia pasipo kufuata mihemko baada ya kufanya utafiti wa kutosha.

RIPOTI YA CAG KUFANYIWA KAZI MWEZI NOVEMBA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson amesema Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka 2021/22 itafikishwa Bungeni baada ya Kamati zinazosimamia masuala ya Fedha kuipitia na kuwahoi watuhumiwa kisha majibu yatatolewa Novemba 2023.

Amesema kwa sasa hoja zinazoibuliwa na Wabunge hazitapatiwa majibu ikiwemo wahusika kuchukuliwa hatua yoyote hadi pale ambapo wahusika watahojiwa na Kamati za Chombo hicho kwa kuwa Serikali inazingatia haki za msingi za binadamu zinazojumlisha “Haki ya kusikilizwa kwa watuhumiwa”

Amebainisha kuwa kikao cha mwezi novemba kitatoa maazimio ya pamoja kwa Serikali ambayo yataonesha sura ya jumla ya mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwa wahusika.

Mbunge Asia Abdulkarim Halanga ashauri wasanii wa kiume kuacha kuvaa uhusika wa kike

Mbunge Asia Abdulkarim Halamga ameshauri Wasanii wa Kiume Nchini kuacha kutumia Mavazi ya kike wakati wanapoigiza badala yake watafute njia nyingine ya kufikisha ujumbe kwa kuwa tabia hiyo inachangia kuhamasisha Mapenzi ya Jinsia moja

 
Ameiagiza Serikali kufanya utafiti kupitia tume ya kurekebisha sheria ya mambo yapi yaongezeke kwenye Sheria ya kuzuia Ushoga na Usagaji ili kuziba mianya iliyopo sasa. Sheria hiyo inapaswa kutungwa kwa uhalisia pasipo kufuata mihemko baada ya kufanya utafiti wa kutosha.
safi, sheria itute meno tuhangaike na haya ma bwabwa mitaani, msako utakuwa nyumba kwa nyuma tunaanzia mikoa vinara Dar es salaam, Tanga, Zanzibar mabwabwa yote kaeni mkao wa kula tunakuja.
 
Sheria iseme wazi kuwa kufanya kitendo chochote kinachoashiria ushoga na usagaji ni kosa na kifungo ni miaka 30! Kwa mfano wanawake kupigana busu au mwanamume kumshika kiunoni au matakoni mwanamume mwenzake! au wanaume kupigana busu!!
 
Back
Top Bottom