Quote From: The President Dr. Jakaya M. Kikwete!

Ni kweli yameanza wakati wa KIKWETE ila nafikiri kwa asilimia kubwa sana hili litakuwa limechangiwa na UMATONYA wetu/wake huko anakopita kutembeza bakuli, wanamuwekea masharti.

Kama hizi kamati za Bunge kuwa chini ya upinzani, ni hao Wafadhili waliweka hilo. Kama Tanganyika ingelikuwa na Mafuta kama Angola, sidhani kama haya tungeyaona maana wangelikuwa wakali wakijringia hela za mafuta. Ila kwa sababu sasa tumeshikwa pabaya, ngoja tuadhirike tu na Kikwete apewe HONGERA kwa KUTIMIZA masharti ya Wafadhili na sisi hapa nyumbani tubaki kumsifia kwa kubadili utaratibu.

HONGERA Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (Wafu?)..................
- Mnyonge mnyongeni baba, one step kwanza mimi nilidhani hawa CAG wameanza kwenye Awamu yake tu, kumbe mnasema walikuwepo siku zote, duh!

- Mkuu Rome haikujengwa siku moja!

William.
 
Yaani badala ya kuchukua hatua stahiki Jk anasema amefurahishwa na sisi tunashangilia?kama amefurahi so what?,kwa rais mwenye madaraka makubwa kama Rais wa Tanzania,hili sio swala la yeye Rais kufurahishwa bali ni swala la kuchukua hatua,yaani mabilioni ya fedha yanatafunwa kifisadi,rais anakuja na sentensi ya ajabu kama hii....
Alichonichekesha ni kusema anashughulikia mfumuko wa bei. Miezi michachje ilokiwa 19 per cent, sasa zaidi ya 24 per cent! Is he really serious? Anafanya nini practically kuupungiza? Sioni na sielewi!
 
Mkuu NasDaz umenifurahisha sana na hayo maono yako. Naisupport sana hiyo ADG. Kwa nchi zetu hizo hiyo aina ya utawala ni nziri hadi ambapo wananchi tutakapobadilika na kuwa waungwana. Lakini katika jamii yetu hii iliyoporomoka kimaadili ambapo kila kijana akimaliza chuo anagikiria kuajiriwa mmserikalini ili awe fisadi, utawala bora si mahala pake. Miaka ya 90 vijana walipokuwa wakimaliza vyuoni walikuwa wakitaka waajiriwe kwenye sekta binafsi ili wapate mshahara mzuri kulinganisha na serikali. Lakini siku hizi kila kijana anataka aingie serikali si kwa sababu ya mshahara bali fursa za kufisidi.
Kwenye good governance and rule of law ni tabu kwelikweli kumtia mtu hayiani kwa wizi kwa kuwa watu huwa wajanja ukiwapeleka mahakamani unakosa shahidi jamaa anatoka huku unajua kabisa kwamba ana mali za wizi.

Africa tulikimbilia demokrasia kabla ya kupita hatua ya udikteta kama wa Italy, Urusi, Germany, nk.
 
Last edited by a moderator:
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,

- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita! Na mfano mdogo ni hii CAG, mnasema imekuwepo toka Awamu ya kwanza, mna maana toka enzi zile tunanunua Mandege mabovu ya ATC, Gapex, BOT, mnasema CAG walikuwepo?

William.[/QUO

mwaka jana mlitoa kauli gani juu ya matukio hayo yote ? Mliyaita kuwa ni mafanikio ya Uongozi chini ya CCM. Leo mnaanza kuwalaumu wengine. Lakini haina maana kwani kwa wenzake hapakuwa na wizi wa kiasi hiki.

Kaka kumbuka ripoti ya CAG iliyomuhusu jairo
 
Mkuu ni JK anatisha sana, majambazi na wezi wanamuogopa sana.

Ila naona tatizo anafight alone maana huku kwenye maidara kuna mchwa

Walau unakaribia kuelewa chanzo cha tatizo ....... naunga mkono hoja......swali la nyongeza...
Kwakuwa huu ni mwaka wa 7 akiwa madarakani kama rais wa JMT..je,.. amefanya nini kudhibiti hao mchwa??
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,

- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita!

unataka ubunge bwelele?
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,

- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita! Na mfano mdogo ni hii CAG, mnasema imekuwepo toka Awamu ya kwanza, mna maana toka enzi zile tunanunua Mandege mabovu ya ATC, Gapex, BOT, mnasema CAG walikuwepo?

William.

Sina shaka hata kidogo katika hilo....ukweli ndio huo hata kama kuna wengine watapinga! Ni bahati mbaya sana, pale penye ukweli panapofushwa na itikadi kisiasa, lakini mbaya zaidi wengine wanaleta hadi itikadi za dini! Any, But hii ndio JF banaa!
 
Nakubaliana na wewe maana quote yake inaonesha kuwa hakuwa na uwezo wa kuwajibisha wabadhilifu mpaka wabunge watokwe mapovu bungeni?

Hujamsikiliza aliyoyasema, amesema kinaga ubaga, kaletewa ripoti akasema ipelekwe bungeni ikajadiliwe na kila Mtanzania aelewe kinachotendeka na CAG asimuonee mtu haya (I am not quoting word to word, the concept).
 
Wiliam
Unajifariji na maneno matupu?kwa hali ya nchi,na jinsi watanzania masikini tena walipa kodi wanavyokufa kwa kukosa dawa,hospitalini,kwa kuwa tu kuna wachache wamefisadi hizo huduma,alafu eti tunafurahia na kupongeza kufurahishwa kwa Rais na ripoti ya CAG...
Ripoti ya CAG si ya kufurahisha hata kidogo,huwezi soma ile ripoti ukafurahi,badala yake ni kuchukua hatua..
CAG yupo miaka yote,na ni mteule wa Rais,akishamaliza ukaguzi anawasilisha ripoti kwa Rais,hivyo JK amekalia ripoti za CAG sita sasa,eti hii ya sita ambayo ni chafu kuliko zote imemfurahisha,.....Tafakari
- Mnyonge mnyongeni baba, one step kwanza mimi nilidhani hawa CAG wameanza kwenye Awamu yake tu, kumbe mnasema walikuwepo siku zote, duh!

- Mkuu Rome haikujengwa siku moja!

William.
 
Kwa Institutional Reforms, JK amefanya vya kutosha hata kama watu wataendelea kupinga! Kilichobaki, na ama kilichokosekana toka kwake yeye binafsi na watendaji wengine ni kuchukua hatua stahiki kutokana na reform husika!

Ndani ya jamii isiyo na mapungufu ya maadili, reform iliyofanywa na JK ilitosha kabisa kusafisha nchi yetu! Kwa bahati mbaya sana, kuna mmomonyoko mkubwa sana wa maadili, toka kwa vingozi, watendaji wakuu hadi wananchi wa kawaida! Mmomonyoko huu katu hauwezi kutibika ndani ya wha's so called GOOD GOVERNANCE! Good Governance/Utawala Bora unafanya vizuri ndani ya jamii iliyesheheni maadili. Lakini jamii kama yetu, inahitaji Approved Dictatorship Governance (ADG)....yaani Utawala wa Kidikteta Ulioidhinishwa!
Ripoti ya CAG imetaja ufisadi mkubwa kwenye wizara na taasisi mbalimbali....under Good Governance, hatuna chochote cha kuwafanya wahusika! Sana sana, ni kuwaachisha kazi....kazi ni ya nini basi ikiwa tayari mtu ameshapata ukwasi wa kutosha!!! Haina haja! Na kama tumejitahidi sana, labda tutawapeleka mahakamani....huko, kesi itaunguruma miaka kadhaa....at the end of the game, hapatakuwa na ushahidi usio na shaka yoyote kuthibitisha tuhuma ama za wizi au ubadhirifu! Labda, tunaweza ku-force na kubambika kesi ya matumizi mabaya ya ofisi; Amatus Lyumba, alifungwa miaka 2; What da Hell! That's why I Hate Good Governance kwenye nchi yenye mmomonyoko wa maadili kama yetu!
Under ADG, kama kweli mtu kama Ngeleja amenunua nyumba ya mamilioni ya fedha, wala tusingekuwa na sababu ya upande wa mashitaka uthibitishe kwamba nyumba hiyo ameinunua kwa vyanzo ambavyo si halali, bali ni yeye; within a day, athibitishe beyond reasonable doubt, kwamba ameinunua kwa mapato halali! Na akishindwa kufanya hivyo, JELA!

Well said,

Kama nimekuelewa vyema tuna matatizo makubwa kwenye sheria zetu, na hapo ndio wafujaji wanapozichakachua kwa

kujua weakness zake.

Well said my brother
 
Walau unakaribia kuelewa chanzo cha tatizo ....... naunga mkono hoja......swali la nyongeza...
Kwakuwa huu ni mwaka wa 7 akiwa madarakani kama rais wa JMT..je,.. amefanya nini kudhibiti hao mchwa??

Unafikiri hicho kinachoongelewa sasa ni kitu kidogo? hilo ni kubwa sana katika kudhibiti haya madudu, ngoja uone ripoti ya mwaka 2012-2013 ya CAG, utaona madudu yalivyopunguwa.
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,

- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita!

unataka ubunge bwelele?

- ha! ha! ha! ha! ha! ha!

Le Mutuz Big Shooow!
 
Vipi ile taarifa ya CAG (Mhilu) ya mwaka 2009 kabla ya hajawa rais. Je, wahusika wa wizara ya ya Mambo ya nje ambayo ni kati ya wizara zilizoongoza kwa kutafuna. alikasirika.

Hueleweki Mkuu, 2009 nani hajawa Rais?
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,

- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita! Na mfano mdogo ni hii CAG, mnasema imekuwepo toka Awamu ya kwanza, mna maana toka enzi zile tunanunua Mandege mabovu ya ATC, Gapex, BOT, mnasema CAG walikuwepo?

William.[/QUO

mwaka jana mlitoa kauli gani juu ya matukio hayo yote ? Mliyaita kuwa ni mafanikio ya Uongozi chini ya CCM. Leo mnaanza kuwalaumu wengine. Lakini haina maana kwani kwa wenzake hapakuwa na wizi wa kiasi hiki.

Kaka kumbuka ripoti ya CAG iliyomuhusu jairo

- Kumbe CAG ilimnyofoa na Jairo, tena kwenye awamu hii hii ya nne, kweli Mnyonge mnyongeni!

William.
 
Walau unakaribia kuelewa chanzo cha tatizo ....... naunga mkono hoja......swali la nyongeza...
Kwakuwa huu ni mwaka wa 7 akiwa madarakani kama rais wa JMT..je,.. amefanya nini kudhibiti hao mchwa??

Mkuu, ufisadi au uovu wowote haudhibitiwi na mtu bali unadhibitiwa na mfumo wa kitaasisi! Mathalani, Rais unaweza kuwa mkali kweli kweli kwenye masuala ya rushwa, lakini mfumo wa kitaasisi sio mzuri! What next, ina maana ukishaondoka madarakani basi kila kitu kitakuwa shaghalabaghala! Inasemekana Nyerere alikuwa anachukia sana ufisadi, lakini alipoondoka tu, ufisadi ukaota mizizi...why? Coz' hakuacha mfumo unaopiga vita ufisadi! Ufisadi ulikuwa unachukiwa na yeye binafsi na sio taasisi...hayo ni mapungufu makubwa! Anachofanya JK, ni kujenga mfumo utakaokuwa against na ufisadi! Mfano mzuri, ni hili la CAG! Ni utawala wa JK ndio uliamua kumu-attach DCI na TAKUKURU ili pale mapungufu as a result of CAG Report yakionekana, basi kama kuna dalili za rushwa basi hapo moja kwa moja TAKUKURU wanaingia na kama kuna dalili za wizi, moja kwa moja DCI anaingia!

Nilishapata kusema hapo kabla.....tatizo lililopo, TAKUKURU, DCI na DPP hawafanyi kazi zao inavyopaswa!! Inasemekana, hawa watu hawana meno, jambo ambalo si kweli hata kidogo! Madai kwamba wanashindwa kufanya kazi kwavile nafasi zao ni za kuteuliwa na Rais, nayo ni madai mfu!!
 
Mnyonge wa kunyongwa au kupewa haki hapa ni le Baharia au le Dr. Dr. Dr. Kikwete?

Nilimaanisha Kikwete na mleta mada anastahili sifa kwa kuwa mkweli na muwazi.

Cha kushangaza nilileta mada ya kuisifia hii hotuba ya JMK leo, lakini imefutwa na kuunganishwa na nyingine.

Kuna moderator anafanya kila njia kupunguza makali ya hii, nimefi=urahi kwa kuwa nasikia huyu kijana ni mfadhili wa JF kwa hiyo kaileta na hakuna anayeweza kuthubutu kuihamisha au kuifuta. Kwa hilo nampa hongera.
 
Kwa hili la uwazi, Kikwete tutamkumbuka. Maana kabla yake repoti ya CAG huwa inabaki ikulu na haipelekwi kwa wananchi. Kwa hili Bravo Kikwete.

Ikiletwa kwetu ndo wezi Katka wizara na halmashauri watafunguliwa mashtaka? watanzania tujifunze kufkiria kwa umakini vinginevyo tutaendelea kuibiwa.
Kwa kifupi ni kuwa hakuna jipya kwenye hotuba ya Jk bali ni muendelezo wa maneno yale yale kama ilivokuwa kwenye issue ya DOWANS.
 
Ok Willy,
But unachukuliaje suala la kuomba kwanza ushauri kwenye CC ya chama juu ya kuwashughulikia wabadhirifu serikalini?
Huoni kama inaleta picha kua anawaogopa so anatafuta cha kujitetea kua ni CC ndo imewafukuza na sie yeye??
 
Unafikiri hicho kinachoongelewa sasa ni kitu kidogo? hilo ni kubwa sana katika kudhibiti haya madudu, ngoja uone ripoti ya mwaka 2012-2013 ya CAG, utaona madudu yalivyopunguwa.

Mkuu Ribosome inatakiwa tuwe makini sana na hizi report. Unaweza ukaona rrport nzuri ama hati safi lakini ikawa nayo ometolewa kifisadi! Jamii yetu imebobea kwenye ufisadi kila ukigusa mahala ni ufisadi tu kuanzia serikalini hadi kwenye vyama vya siasa. Hivyo mkuu kwa kuwa kuna ufisadi usije ukashangaa wakaguliwa wanajipanga upya dhidi ya CAG na watu wake na matokeo yake ikawa ni kuonekana kupungua kwa madudu kama unavyosema.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom