Quote From: The President Dr. Jakaya M. Kikwete!

JK Mzee wa OTTU alaah kumbe alimaanisha UTouh majina mengine bana duh taabu kweli kweli yanafichua personal interest za watu at wrong place
 
Ok Willy,
But unachukuliaje suala la kuomba kwanza ushauri kwenye CC ya chama juu ya kuwashughulikia wabadhirifu serikalini?
Huoni kama inaleta picha kua anawaogopa so anatafuta cha kujitetea kua ni CC ndo imewafukuza na sie yeye??

- Baba yangu ameniambia mara nyingi sana kwamba huwezi kuongoza bila kukubaliana na wenzako, HOWEVER: hivi ni kweli alienda CC kuomba ushauri au CC ndio waliomuomba on their own kwa niaba ya chama,

- I mean Rais alikuwa nje, amerudi amekuta saga la CAG na mawaziri, eti ni siku hiyo hiyo aliyoshuka anawafukuza mawaziri na kutangaza baraza jipya? Siamini kwamba alienda CC kuomba ushauri, ninaamini kwamba kilikuwa ni kikao cha kawaida kila mwisho wa mwezi, lakini hata kama alienda kule for that bado ni within the rules za chama, au?

William.
 
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete

Brother Willy,
Hapa TZ wezi wa kuku ndio watafungwa tu. Sio wa Kagoda, EPA, RADA, walioingia mikataba inayofilisi hii nchi kama IPTL, DOWANS, RICHMOND nk. Hii ni babaisha ***** tu. Huu ni mwaka wa 7 wa raisi, lakini takwimu zinaonyesha ufisadi ndio unaongezeka. In fact, hapa alikuwa anataka sifa apewe yeye tu.
Huko nyumba wizi ulikuwa unafanyika, lakini uchumi uliimarika. Leo inflation rate ni 24 (tena hiyo ni official ambayo mara nyingi ni ya kuwahadaa wananchi waone mambo yako sawa, deni la taifa linakua kwa kasi ya 36%), na uchumi unakua kwa 6%, yet tunapewa maneno ya kutupa moyo kama haya.
Nione watu kama Chenge, Rostam, wakilala prison ndio nitaona kuwa hizo taasisi zimefanya kazi. Watawatoa Kafara akina Gray Mgonja, Mramba kwa sababu ni marafiki wa Mkapa tu basi. Wala rushwa hawatafanyiwa chochote
 
Kwa vijana wa zamani tunasema MAHOKAAA...Hahahahaaahaaa ahaahaaa:)
 
Mkuu, ufisadi au uovu wowote haudhibitiwi na mtu bali unadhibitiwa na mfumo wa kitaasisi! Mathalani, Rais unaweza kuwa mkali kweli kweli kwenye masuala ya rushwa, basi mfumo wa kitaasisi sio mzuri! What next, ina maana ukishaondoka madarakani basi kila kitu kitakuwa shaghalabaghala! Inasemekana Nyerere alikuwa anachukia sana ufisadi, lakini alipoondoka tu, ufisadi ukaota mizizi...why? Coz' hakuacha mfumo unaopiga vita ufisadi! Ufisadi ulikuwa unachukiwa na yeye binafsi na sio taasisi...hayo ni mapungufu makubwa! Anachofanya JK, ni kujenga mfumo utakaokuwa against na ufisadi! Mfano mzuri, ni hili la CAG! Ni utawala wa JK ndio uliamua kumu-attach DCI na TAKUKURU ili pale mapungufu as a result of CAG Report yakionekana, basi kama kuna dalili za rushwa basi hapo moja kwa moja TAKUKURU wanaingia na kama kuna dalili za wizi, moja kwa moja DCI anaingia!

Nilishapa kusema hapo kabla.....tatizo lililopo, TAKUKURU, DCI na DPP hawafanyi kazi zao inavyopaswa!! Inasemekana, hawa watu hawana meno, jambo ambalo si kweli hata kidogo! Madai kwamba wanashindwa kufanya kazi kwavile nafasi zao ni za kuteuliwa na Rais, nayo ni madai mfu!!

Well said mkuu nami naunga mkono hoja though tunarudi kule kwenye msimamo wangu na wajibu wa rais.... hapo kwenye red....Kama wateule hao wa rais hawafanyi kazi zao ipasavyo..je rais anajua?? kama anajua basi hilo ni tatizo kwasababu anaacha watu wasiofaa, wasiojua wajibu wao na ambao hawamsaidii rais.

Kama hajuibasi hilo ni tatizo kubwa zaidi....
 
Brother Willy,
Hapa TZ wezi wa kuku ndio watafungwa tu. Sio wa Kagoda, EPA, RADA, walioingia mikataba inayofilisi hii nchi kama IPTL, DOWANS, RICHMOND nk. Hii ni babaisha ***** tu. Huu ni mwaka wa 7 wa raisi, lakini takwimu zinaonyesha ufisadi ndio unaongezeka. In fact, hapa alikuwa anataka sifa apewe yeye tu.
Huko nyumba wizi ulikuwa unafanyika, lakini uchumi uliimarika. Leo inflation rate ni 24 (tena hiyo ni official ambayo mara nyingi ni ya kuwahadaa wananchi waone mambo yako sawa, deni la taifa linakua kwa kasi ya 36%), na uchumi unakua kwa 6%, yet tunapewa maneno ya kutupa moyo kama haya.
Nione watu kama Chenge, Rostam, wakilala prison ndio nitaona kuwa hizo taasisi zimefanya kazi. Watawatoa Kafara akina Gray Mgonja, Mramba kwa sababu ni marafiki wa Mkapa tu basi. Wala rushwa hawatafanyiwa chochote

- Sawa lakini je huko nyuma nani waliwahi kufungwa au kupoteza kazi kwa wizi kama sasa, I mean something is better than nothing,

1. Ripoti ya CAG hatukuwahi kuisikia, wala kiongozi yoyote kupoteza kazi kwa sababu ya CAG.

2. Inflation ipo hata USA, wacha sisi mkuu matatizo ya uchumi ni dunia nzima, suala la viongozi wezi kutochukuliwa hatua limeanza toka awamu ya kwanza, lakini angalua leo tunawajua kwa sababu ya hizi ripoti za CAG kuwekwa wazi, sio zamani wala hatukujua kama ilikuwepo.

- Rais wa sasa ana mapungufu yake, lakini sio sawa na waliopita huyu ana nafuuu sana, na hasa jinsi sasa mambo yalivyo wazi!

William.
 
Maelezo aliyotoa JK leo yametoa mwanga kuhusu namna gani anavyoshughulikia tatizo sugu la usimamizi wa fedha ya umma. Hata hivyo bado naona mtihani anao. Watanzania wanajua kuwa viongozi wengi ni wezi, wanachotaka ni actions na sio mijadala.

Kwa kujadili bungeni haimaniishi kuwa tatizo sasa limepata jawabu. Bunge la Makinda halina historia nzuri ya kujali maslahi ya umma, mfano, maelezo ya Lema kuhusu uwongo wa waziri mkuu hadi leo hayajawekwa hadharani, pia ukimya/ubabe wa Makinda kuhusu ombi la wabunge kujadili mgomo wa madaktari - ni doa kubwa sana na la ki-hostoria.

Kwa kiasi fulani naweza kuufananisha utawala wa JK na Pilato. Kwangu mimi Pilato aliamini Yesu alikuwa na hatia (kujiita mfalme wa wayahudi) lakini alijua kama angemhukumu basi wafuasi wake (Yesu) wangemletea shida yeye pilato na utawala wake wa kirumi. Wakati huo huo hakuona tishio la Yesu kwa utawala wake na hivyo angeweza kabisa kumuacha huru lakini akahofia reaction ya makuhani na wapambe wao. Na ndio maana akanawa mikono na kumkabidhi yesu kwa umma ili uhangaike naye.

Kama kuna mtu anayeijua CCM vizuri na cancer yake basi ni JK. Na ni mtu wa aina ya JK peke yake anayeweza kupambana CCM kwa kuondoa 'tumor' (cancer). Inahitajika subira na uvumilivu wa hali ya juu. Nakubaliana kabisa na wale waliosema kuwa JK ni chaguo la mungu!

CCM ilikuwa too powerful na kutokana na nguvu hizo chama hicho kiligeuka kuwa kimbilio la 'mafia-mafisadi' wasio na huruma kwa Tanzania. Wameifikisha hii nchi kuzimu and the only way kulinusuru taifa hili ni kukata ccm vipande vipande ili upande wenye tumor uondelewe. Whether huyu mgonjwa (ccm) atapona au atafia kwenye meza ya upasuaji hilo ni jingine lakini walau nchi itapona!
 
Ok Willy,
But unachukuliaje suala la kuomba kwanza ushauri kwenye CC ya chama juu ya kuwashughulikia wabadhirifu serikalini?
Huoni kama inaleta picha kua anawaogopa so anatafuta cha kujitetea kua ni CC ndo imewafukuza na sie yeye??
 
- Baba yangu ameniambia mara nyingi sana kwamba huwezi kuongoza bila kukubaliana na wenzako, HOWEVER: hivi ni kweli alienda CC kuomba ushauri au CC ndio waliomuomba on their own kwa niaba ya chama,

- I mean Rais alikuwa nje, amerudi amekuta saga la CAG na mawaziri, eti ni siku hiyo hiyo aliyoshuka anawafukuza mawaziri na kutangaza baraza jipya? Siamini kwamba alienda CC kuomba ushauri, ninaamini kwamba kilikuwa ni kikao cha kawaida kila mwisho wa mwezi, lakini hata kama alienda kule for that bado ni within the rules za chama, au?

William.

William,

..Raisi akiwa nje ya nchi haimaanishi kwamba amekwend likizo ya Uraisi.

..huyu ni Raisi wetu kwa kipindi chote cha miaka 5 haijalishi yuko nje ya nchi au ndani.

..kwa mtizamo wangu mawaziri hawa wamemchafua Raisi, serikali, na nchi nzima.

..tumefika mahali ambapo wananchi sasa wanaunganisha ubovu wa mawaziri hawa na Raisi pamoja na chama tawala.

..suala la KAMATI KUU kutoa tamko kuhusu hawa mawaziri ni jitihada za CCM kujinasua na kujikosha na lawama na utendaji mbovu wa mawaziri wa CCM.

..ile "santuri" ya wimbo wa CCM ni nzuri isipokuwa inachafuliwa na watu wachache, au Raisi ni mtu makini ila anaponzwa na washauri wake, imeanza kugoma sasa.
 
Hii mikina malichwela ni products za nepotism kwa nini inapewa platform humu JF?

- Kwani CAG imekuwepo kwa muda gani? Maaana hii ni mara yangu ya pili kuisikia, mara yangu ya kwanza ilikuwa Dr. Kikwete aliposhika utawala mambo ya mabalozi walioiba, wengine wakafikishwa kwenye Sheria na wengine walilazimishwa ku-retire na kulipa walizoiba.

- Hii ni mara ya pili nawasikia tena CAG, naomba kukuuliza walianza lini hawa CAG? Mbona huko nyuma kwenye awamu zingine hatukuwahi kuwasikia?

William.
 
Lakini jamani nauliza: Hivi JK alianza urais mwaka jana? Ameingia mwaka wa saba sasa, ni miaka mingi wa rais mwenye nia ya kupigana na ufisadi kufanya hivyo na angalau ufanisi ukaonekana kwa sasa. Mwaka 2006 alienda Wizara ya Ardhi na kusema inanuka rushwa na kwamba atahakikisha wafanyakazi pale wanabadilika au sivyo kuna wengi wako nje wanazitaka hizo nafasi zao. Hadi leo wizara hiyo bado inaongoza kwa rushwa na hajarudi pale.

Mwaka huo huo 2006 April aliuambia mkutano wa watendaji wa Halmashauri nchini kwamba hatasita kuzifuta (dissolve) zile ambazo hazitabadilika katika utafunaji wa fedha nk. Hajaifuta hata moja na leo bado anazilalamikia hizo halmashauri.

Mnasema tatizo ni mfumo? Hapana. Tatizo ni kukosa ujasiri wa kuchukuwa maamuzi na kwa JK sababu ya hilo linajulikana, hasa ukizingatia namna alivyoupata urais.

Acheni ku-beat about the bush a.k.a. ku-go around in circles a.k.a. kubwabwaja. Ukweli ni huu.
 
Quote ya maisha magumu kwa kila mtanzania sipokuwa mafisadi amesemaje?Mishahara kima cha chini amesemaje?

"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
 
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete

Hapo sasa zimefanyiwa kazi gani? Wanaomfundisha JK kujinasua wanadhani anaongea na Majuha! Hivi JK, amesahau kuwa pressure tuliyompa halali ata usingizi na leo kaja kujipoza? Je amekanusha lile swala "Huu ni upepo utapita" Mleta mada sijui unamfagilia au unataka tuchangie nini hapa kwenye mtego wako!!!!!!!
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba siasa ni kama biashara ya utumbo, huwezi kuifanya huku unaogopa harufu, I mean unajua how long nimekuwepo hapa JF, huwa yanakuja na kupita ila ukweli unasimama mpaka mwisho,

- Kwamba Dr. Jakaya M. Kikwete, huenda ni the best kuliko wote waliopita, I have said that before na ninasema tena now!, unaposema kiongozi mmoja hafai unamlinganisha na wanaofaa, ndio maana ninasema anawazidi wote waliopita! Na mfano mdogo ni hii CAG, mnasema imekuwepo toka Awamu ya kwanza, mna maana toka enzi zile tunanunua Mandege mabovu ya ATC, Gapex, BOT, mnasema CAG walikuwepo?

William.

Mkuu, naona kama unampaka Jk mafuta kwa mgongo wa chupa! There is something synical with your comments. Ni jambo lililo wazi kuwa ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma umetokea ama katika hrakati za kumweka jk mdarakani au katika kipindi cha uongozi wake. Ni kweli ofisi ya CAG imekuwako toka zamani, lakini kulikuwa hakuna wizi wa viwango tunavyoshuhudia sasa. Wewe mwenyewe ni shahidi katika hili. Dingi yako amekuwa mtumishi wa uma kwenye ngazi za juu kwa muda mrefu, lakini nina mashaka kama nyumba anayoishi ina walau nusu tu ya thamani ya nyumba za mawaziri wetu vijana. And am sure you know what I mean.
 
Lakini jamani nauliza: Hivi JK alianza urais mwaka jana? Ameingia mwaka wa saba sasa, ni miaka mingi wa rais mwenye nia ya kupigana na ufisadi kufanya hivyo na angalau ufanisi ukaonekana kwa sasa. Mwaka 2006 alienda Wizara ya Ardhi na kusema inanuka rushwa na kwamba atahakikisha wafanyakazi pale wanabadilika au sivyo kuna wengi wako nje wanazitaka hizo nafasi zao. Hadi leo wizara hiyo bado inaongoza kwa rushwa na hajarudi pale.

Mwaka huo huo 2006 April aliuambia mkutano wa watendaji wa Halmashauri nchini kwamba hatasita kuzifuta (dissolve) zile ambazo hazitabadilika katika utafunaji wa fedha nk. Hajaifuta hata moja na leo bado anazilalamikia hizo halmashauri.

Mnasema tatizo ni mfumo? Hapana. Tatizo ni kukosa ujasiri wa kuchukuwa maamuzi na kwa JK sababu ya hilo linajulikana, hasa ukizingatia namna alivyoupata urais.

Acheni ku-beat about the bush a.k.a kubwabwaha. Ukweli ni huu.

Sasa nadhani JK anaweza kujiona hivyo maana yeye ni mgeni. Miaka zaidi ya mitatu amekuwa nje ya nchi na kwa maana hiyo haijui TZ vizuri. Hapo Zak Malang, ndo hujue kuwa ukombozi bado! Kuna mijitu inadanganywa hd kwa pp!
 
"Nimefurahishwa na mjadala wa uwazi ulioendelea Bungeni na kwenye kamati ya wabunge wa CCM; nafurahi kwamba azma yangu ya kuzifanya taarifa za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ziwe zinafanyiwa kazi imeanza kutimia" Mhe. Jakaya M. Kikwete
hivi lengo la kikwete ni kweli kupambana na ubadhirifu huu au ni usanii tu wa kupata ujiko/sifa kwa kuonekana kama kweli anakerwa na ubadhirifu huo...wenye busara walisema cag apewe meno ya kuweza kuwafikisha mahakamani na kuwashtaki hawa wafujaji wa mali ya umma na ripoti yake itumike kama zile ripoti za daktari za sababu ya kifo cha mtu zinavyotumika mahakamani...ushahidi wa cag wala hauhitaji kupelekwa bungeni na kujadiliwa...kungekuwa na nia ya dhati, dpp angekuwa ameshaanza kuaanda mashtaka kwa watuhumiwa wote waliotajwa kwenye ripoti ya cag lakini kama kawaida ya sheria zetu zilizotungwa kuwalinda mafisadi itachukua miaka mpaka hawa jamaa kufikishwa mahakamani na hata wakifikishwa wengi wao kama si wote wataachiwa...kikwete akamuonyeshe mwanaasha hivyo viini macho lakini sisi wenye akili zetu hatudanganyiki...!
 
Back
Top Bottom