Luqman mohamedy
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 892
- 1,226
Mama hafahamu mwenye njaa haogopi kufa, kwani hata njaa itamuua.
Kuna muda nawaza hawa watu wamesomeshwa na mission nini? Hawajui njaa kabisa. Tuliopitia huu msoto kipindi kile tunaelewa.
=====
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameuagiza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kuwachukulia hatua viongozi wa Serikali ya Wanafunzi ya chuo hicho (DARUSO), waliotoa tamko la kuipa serikali saa 72, kulipa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, vinginevyo wataandamana.
Juzi Daruso walitoa saa 72 kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), kuhakikisha inatoa mikopo kwa wanafunzi waliokosa, vinginevyo watakutana nje ya ofisi za bodi hiyo zilizopo Mwenge jijini humo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana, Profesa Ndalichako alisema tamko hilo limetolewa kinyume cha utaratibu wa kutoa malalamiko na utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu, ambacho hakiwezi kuvumilika, hivyo ametoa saa 24 kwa UDSM, kuwachukulia hatua na apewe taarifa hatua iliyochukuliwa.
Alisema kwa mujibu wa taratibu, uongozi wa Daruso unapaswa kuwasiliana na Mshauri wa Wanafunzi, ambaye anachukua malalamiko yao na kuyapeleka kwa Makamu Mkuu wa chuo.
Lakini, taratibu hizo zote hazijafuatwa na uongozi wa chuo hicho kikongwe nchini haujui chochote kuhusu madai na malalamiko hayo. Aidha, alisema wanafunzi 45,000 wa mwaka wa kwanza, walipaswa kupewa mikopo, lakini serikali imeongeza idadi na kufikia 49,485, na Sh bilioni 172 zimetolewa kwa ajili yao na wameshapata mikopo wote waliokidhi vigezo.
Alisema jumla ya wanafunzi 128,697 wa elimu ya juu, wanatarajia kunufaika na mikopo mwaka huu, ambayo kiasi cha Sh bilioni 447 zimepangwa kwa mikopo, na hadi sasa Sh bilioni 202 sawa na asilimia 45 zimeshapelekwa HESLB.
Katika madai ya wanafunzi hao, alisema zipo taratibu za uhakiki wa vigezo na nyaraka wanazopaswa kuwasilisha wanafunzi na hivyo bodi ilikuwa inapitia vigezo na kujiridhisha, ikiwamo uwepo wa wanafunzi yatima, walemavu na uwepo wa wanafunzi waliokata rufaa, ambao taarifa zao zinafanyiwa kazi ili wakikidhi vigezo wapatiwe mikopo.
“Wakati taratibu za uhakiki zinaendelea, wanafunzi wamekuja na tamko ambalo ni utovu wa nidhamu mkubwa tena wanaipa serikali masaa 72 watekeleze madai yao vinginevyo wataandamana, nasema hivi masaa 72 ni mengi waanze maandamano leo, wanatingisha kiberiti, lakini nawaambia kiberiti kimejaa,” alisema Profesa Ndalichako.
Alisema amezungumza na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo, lakini hajapata malalamiko yoyote rasmi, zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari, hivyo tamko hilo ambalo halikufuata taratibu ni batili na utovu wa nidhamu.
“Wanafunzi wasiotaka kusoma, waondoke na kuwaacha wanaotaka kusoma, kwa sababu tamko hili kama lina jambo lingine zaidi ya masomo, tamko hili linalenga kuleta vurugu na kuvuruga masomo, tutalishughulikia kikamilifu,” alisema waziri huyo wa Elimu.
Wakati waziri akitoa uamuzi huo, HESLB imesema hadi sasa jumla ya wanafunzi 49,485 wa mwaka wa kwanza, wameshapata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 169.4 na kuvuka lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 45,000.
Imesema kati yao, wanafunzi yatima waliopoteza mzazi au wazazi wote wawili ni 10,383, wenye ulemavu 397, waliofadhiliwa masomo ya sekondari 3,128 na wengine wahitaji 35,577.
Aidha, wanafunzi 78,337 wanaoendelea na masomo, wamepata mikopo yenye thamani ya Sh bilioni 272.1. Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema pamoja na malipo hayo, kwa sasa bodi hiyo inakamilisha malipo ya fedha za wanafunzi waliobadilisha kozi, ambayo imepokelewa na HESLB kutoka Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) mwishoni mwa wiki na fedha hizo zitawafikia wanafunzi ifikapo kesho.
Alikuwa akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Menejimenti ya HESLB, Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wawakilishi wa viongozi wa wanafunzi wa chuo hicho juzi jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Makamu Wakuu wa UDSM, Profesa Killian Bernadetha (Utafiti), Profesa David Mfinanga (Utawala), wawakilishi wa serikali ya wanafunzi na watendaji wengine wa UDSM na HESLB.
“Kuna kundi la wanafunzi waliobadilisha kozi wakiwa vyuoni na taarifa hizo zilikuwa hazijatufikia, tumezipokea mwishoni mwa wiki na tu
nakamilisha malipo ambayo yatawafikia siku mbili zijazo,” alisema Badru.
Alieleza kuwa kundi lingine linahusu malipo ya vitabu na viandikwa, ambapo malipo ya awamu ya kwanza ya jumla ya Sh bilioni 13.3 yameshafanyika na awamu ya pili ya Sh bilioni 1.1 itawafikia wanafunzi ifikapo Jumamosi ijayo, Desemba 21, mwaka huu, kwa kuwa wataalamu wanakamilisha uchambuzi.
Profesa Anangisye alisema wanafunzi wote wa taasisi za elimu ya juu wanapokutana na changamoto, wasisite kuziwasilisha kwa menejimenti za vyuo ambavyo vitaziwasilisha HESLB au kwa taasisi sahihi.
“Hata nyie (Daruso) mlipaswa kuanzia kwetu na tungeyafanyia yote kazi badala ya kutoa maelekezo ya saa 72,” alisema Profesa Anangisye na kulieleza gazeti hili jana saa 12:04 jioni kwamba walikuwa kikaoni kushughulikia haraka agizo hilo la waziri wa Elimu.
Chanzo: Habari Leo
====
Maoni ya wadau

Wakati wanatoa tamko nilisikia wanasema kwamba hii ni wiki ya sita hawajapewa hela zao za mikopo na maafisa mikopo hawatoi majibu yanayoeleweka
Sasa hapo wanakosa gani?
Nakumbuka mwaka fulani kule Dodoma wakati UDOM bado haijakamilika, waliohusika na ujenzi walikuwa wachina!
Mwaka huo wanafunzi waliokuwa wanategemea hela ya bodi walicheleweshewa kama hivi hivi!
Kilichokua kinaendelea huko ni huruma tu!
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokuja na pocket money kama za Sekondari ( elfu 20, 30, 50 +) kila walipokuwa wanaomba kusaidiwa na wazazi ama ndugu zao baada ya kuishiwa hawakueleweka! Na sababu ya kutoeleweka ni rahisi tu! WAZAZI WENGI HAWANA UWEZO!
Baada ya kama mwezi bila kitu kueleweka, wale wachina na baadhi ya vibarua"walijifaidisha" mabinti kwa gharama ya kuwanunulia chakula cha siku kwa mama lishe waliokuwa wanauza chakula kule!
Fikiria unaamka asubuhi hauna hata mia tano mfukoni! Rafiki yako naye hana! Nyumbani ukiomba hawana! Halafu wakati huo huo unatakiwa uwe darasani, ufanye assignment na vitu vingine vingi!
Hivi hapa mambo yataenda? Unadhani watu watatoka na kauli laini?
Ni kweli kabisa kwa hali ya makato ya bodi yanavyoenda kwa waliokwishaanza kurejesha hasa watumishi wanalalamika riba imekuwa kubwa (wanaiita value retention fee) pengine sawa au kuzidi hata mabenki!
Lakini sote tunafahamu hali za watanzania hawakopesheki na mabenki na wengine hawana uwezo kumudu gharama za chuo!
Kwasababu waliingia makubaliano ya kuwahudumia kwa mkopo huo, kwanini wasipewe kwa wakati?
Kwanini wanapodai makubaliano yao kuzingatiwa watishiwe kuchukuliwa hatua?
Hii kweli ni sahihi?
Mbona wao kwenye marejesho hawana subira? Tena hadi figisu zimo! Wengine wamepewa mikopo ya vyuo viwili hadi vitatu wakati kimsingi walisoma chuo kimoja!
Badala ya kushughulika na chuo kilichopokea pesa, wanashughulika na mwanafunzi ambaye kimsingi hakutumia pesa hiyo! Hata pale vidhibitisho vinapotolewa bado muhanga anaendelea kuhangaishwa hadi maika miwili mitatu na makato yanabaki vile vile!
Kwa mtu aliyekulia familia bora, anapata kila atakacho, amesoma bila shida kamwe hawezi kujua shida wazipatazo hawa wanaotegemea HESLB!
Waziri Ndalichako hapo amewatusi wanafunzi, hajawatendea haki!
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari wana JF
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na msemakweli ni mpenzi wa Mungu, Dr. John Pombe Magufuli imekuwa ikijinasibu kuwa na pesa nyingi kutokana makusanyo makubwa ya kodi.
Ushahidi wa hili ni miradi mikubwa iliyoanzishwa na kuendeshwa na serikali, mfano ni ununuzi wa madege kwa pesa taslimu, ujenzi wa SGR, umeme wa Stiglers Gorge, flyovers, daraja Busisi nk.
Kama vyote hivi vinafanyika kwa uwezo wetu, nini kimetokea mpaka wanafunzi wa elimu ya juu wakose mikopo yao?
Waziri Prof. Ndalichako kunukuliwa ukijimwambafai kumiliki kiberiti kilichojaa na uko tayari kukitumia ili kuwadhibiti wanafunzi wasidai haki yao ni fedheha kwako wewe na serikali unayoitumikia!
Picha mnayotupa sisi wananchi huku ni kuwa Serikali yetu imejaa ulaghai, haina pesa imefilisika! Serikali tajiri haiwezi kutishia kiberiti wanafunzi!
Serikali wapeni wanafunzi mikopo yao ili mlinde heshima yenu mnayotuaminisha!
Wale waliosoma kwa raha sana miaka ile, ndo hawakumbuki umuhimu wa kulipwa stahiki zote kabla ya masomo kuanza ndo mwanafunzi atulie asome, wamesahau kabisa!! Mtoto katoka Sumbawanga, kapewa pesa ya kula njiani labda 50k, baba anategemea mtoto akifika atalipwa pesa na kuanza masomo; mtoto anafika anakuta eti ndo mipango inaendelea ya malipo, je arudi nyumbani ndo aje baadaye, afunge kula na kulala hadi malipo yawe tayari, au afanyeje?
Mnaojitia kuitetea serikali na Prof. Ndalichako hamjui kwamba hiyo so called Bodi ndio chanzo cha matatizo! Wanazichezea pesa za wanafunzi halafu wanajitia kuwa wakali! Na kwa nini wanafunzi waitwe toka nyumbani, kama mambo hayajakaa sawa?
Halafu ona sasa hii communication breakdown; mwenye chuo anasema kama hujalipa hadi tarehe fulani, basi! Bodi ya Mikopo na Waziri wa Elimu wanajitia wako bize "wanakamilisha mambo"; je, meanwhile, mwanafunzi anapaswa kufanyaje?
Hebu kuweni na busara mtoe mawazo yenye maana ya kuwasaidia wanafunzi. Mnataka wafanyeje ndo mjue wana shida?
Ushauri wangu, bodi ifanye kazi usiku na mchana, mambo yote yawe sawa ndio wanafunzi waitwe kutoka nyumbani kuja kuanza vyuo; short of that, ni ujinga mtupu, ubinafsi na roho mbaya zimetawala!