Madai ya Chuo Kikuu cha Iringa kutojali afya za Wanafunzi, uongozi wasema kuanzia mwakani Wanafunzi watalipa Bima moja kwa moja NHIF

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Daada ya andiko la member wa JamiiForums.com kulalamika kuwa Uongozi wa Chuo Kikuu cha Iringa, hawajali suala la afya za wanafunzi kupitia andiko hili - Chuo Kikuu cha Iringa hakijali afya za Wanafunzi, tumelipia mwezi nne sasa hakuna huduma ya Bima majibu yametolewa na uongozi wa chuo.

Prof. Ndelilio A. Urio, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa amesema:

Kwa kawaida ya Vyuo vyote Wanafunzi hulipia Fedha za BIMA ya Afya kupitia Vyuoni. Hakuna Mwanafunzi aliyekamilisha malipo na kukamilisha usajili na kukosa Card Active ya NHIF.

Mpaka sasa Wanafunzi 1,977 wamekamilisha Malipo na wana kadi active za NHIF, Wanafunzi 900 wamelipia BIMA ila hawana Number za NIDA na wamekumbushwa mara kadhaa kukamilisha taratibu za kupata number za NIDA lakini wanasuasua.

Wanafunzi 487 wamelipia BIMA ya Afya ila waliondoka kwenda field bila kukamilisha Registration kama inavyotakiwa na hivyo hawawezi kuwa na Active NHIF Card na nahisi hawa ndio wanaolalamika.

Mpaka sasa Wanafunzi 16 wa mwaka wa kwanza hawajalipia kabisa BIMA zao. Wanafunzi 150 wamelipia BIMA mwezi Februari wakati wa Mitihani na hawa taarifa zitawasilishwa NHIF wiki hii.

Aidha ili kuondokana na tatizo hili, Chuo kimekubaliana na NHIF kuwa kuanzia mwaka ujao wa masomo, Wanafunzi wote watalipia BIMA zao moja kwa moja NHIF na Mfumo wa Chuo wa "Students Records Management System" utawasiliana moja kwa moja na NHIF.

Kwa kushirikiana na Serikali ya Wanafunzi, tutafanya jitihada zote kuondokana na tatizo la BIMA ya afya kwa Wanafunzi.

Kama kuna Mwanafunzi yeyote alienyanyaswa na kutendewa isivyo anione kwa kuwa mpaka sasa sijapata taarifa ya Mwanafunzi yeyote mbali na kupata taarifa kupitia JamiiForums.
 
Ndo akili za wanachuo wa siku hizi, wanajua kabisa kuwa shida ipo sehemu fulani kwa upande wake, lakini huyo huyo anaendelea kulalamika kuwa anaonewa. 😑
 
Hii ni Aina ya wasomi viongozi wanaohitajiwa wakati huu.

Hutokeza Hadharani wakajibu hoja hata kama wameona tuu mtandaoni sio hata ofisini.

Hongera Zaidi.
 
Back
Top Bottom