Wanafunzi 56,132 Waanza Kunufaika na Mikopo Elimu ya Juu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Ni vicheko kwa wanafunzi 56,132 waliopangiwa kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali nchini baada ya kupangiwa mikopo ya elimu ya juu katika awamu ya kwanza inayoenda sambamba na nyongeza ya fedha za kujikimu kutoka Shilingi 8,500 hadi Shilingi 10,000.

Itakumbukwa kuwa Februari mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alipokutana na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TaAHLISO) alipokea ombi la kuongezwa kwa fedha za kujikumu na kuahidi kuwa itaongezwa kufikia Tsh. 10,000.

Akizungumza leo Oktoba 20, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul-Razaq Badru amesema kiasi cha Tsh. 159.7 bilioni kimetolewa kwa wanafunzi hao waliopangiwa mikopo katika awamu ya kwanza.

Amesema orodha ya awamu ya pili ya mikopo itatolewa Oktoba 27, lengo likiwa ni kutoka mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 75,000 katika mwaka wa masomo 2023/2024.

“Orodha hii ya kwanza inajumuisha wanafunzi wenye sifa zikiwemo kuwa wahitaji, wameomba kwa usahihi na wamekamilisha taratibu za udahili wa chuo kimoja. Tunakamilisha uchambuzi wa maombi menhine na tutaoa orodha ya awamu ya pili,” amesema Badru.
 
Mbona uzi umedoda bila responses for such sensitive news au ni fake....
 
Una uhakika ni vicheko?

Wengine wamepewa boom Tu, na wengine na ADA kidogo Tu, mambo Kama ya 2021 vile.
 
Back
Top Bottom