Abdul-Aziz Carter
Member
- Sep 27, 2023
- 7
- 23
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waliofanya mitihani ya supplementary na special hawajapata stahiki zao.
Hii ni wiki ya tano (5) sasa hii, sawa na mwezi 1 na wiki 1, Wanafunzi wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu kutokana na changamoto za kiuchumi zilizo sababishwa na kucheleweshwa kwa pesa hizo.
Ukiingia kwenye mfumo wa mkopo (Account ya chuo ya ARIS3) inaonekana tayari Bodi ya Mikopo imeshaweka tayari location, wanafanya hivyo ili ionekane Mwanafunzi yupo chuo, kinachoonekana hakijafanyiwa kazi ni chuo chenyewe kutokamilisha mchakato ama wa kutuma majibu au majina.
Changamoto hii hasa imewakuta Wanafunzi wa Mwaka wa Pili na Watatu.
Daraja letu sisi ni Serikali ya Wanafunzi, tunachofanya tunaenda kuzungumza nao kisha wao ndio wanaotakiwa kuzungumza na uongozi wa chuo.
Tunaziomba mamlaka husika kufanya uchunguzi juu ya jambo hili na kuwasaidia wanafunzi hawa kupata stahiki zao.
====