PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

Pasco
Wanafanya kazi kwa kutekeleza ilani na sera za CCM pamoja na kwamba ni kauli tata bado ina ukweli ndani yake, serikali iliyopo mdarakani ni CCM. Mkuu haya ya wakuu wa wilaya si ya ajabu hata kwenye nchi yenye demokrasia kama Marekani majaji wa chombo kikubwa cha sheria Marekani -US SUPREME COURT upigaji wao wa kura unategemea zaidi jaji alichaguliwa na raisi wa chama gani; wao hawaangalii makunyanzi hivi unafikiri kama majaji wa Supreme Court wangekuwa hawapigi kura kisiasa unafikiri George Bush angekuwa raisi?

Chama
Gongo la mboto DSM- in vacation Puerto Vallarta
 
CCM kutawala milele, dah watu wana ndoto za alinacha! Hakuna dola iliyowahi kutawala milele katika uso huu wa dunia, dola ya milele ni kwa Mungu tu! Huwa sijui wana CCM wanafikiria nini ni, kuna watu wamesoma lakini bado ni wajinga sana, hawajaelimika kabisa na system imewafanya wajione wao ndo wanasauti kwa wananchi wa Tanzania. Hii nchi sii ya vyama, tunazidi kuchoka tu taratibu na muda ukifika (sijui ni lini) ndo mtajua kuwa tumewachoka!
 
Yan pinda kazi yake ni kutema mabomu kila siku! Sasa jamani tumepewa massage na imetufikia!

Rc,Dc na wengine wana hakikisha CCM inashinda na wana ushawishi kwa jeshi la polisi duu pinda ni mtu wa kutoboa siri tu kila siku.

Sasa watanzania wenzangu nguvu ya umma ina hitajika kulinda kura zetu.

Pinda amezidi kutufungua mcho!
Alitufungua macho alipo sema liwalo na liwe kwenye saga la Ulimboka na sasa katufungua macho tena:
 
WM Pinda anawakilisha tabaka la viongozi wa serikali (wa CCM) waliolewa madaraka hadi wakakumbwa na upofu. Hili ni tabaka lililoamua kuweka akili zao mifukoni na kuminya common sense zao. Pinda is the worst PM this country has ever had na kwa kiasi kikubwa anachangia udhaifu wa serikali hii.
 
Kauli nyingi za Mh. Pinda ni tata na zinatapisha kwa mfano mbali na hili la waku wa wilaya na mikoa Jana pia kasema serikali yake itaendela Kutumia SHERIA MBAYA YA Magazeti mpaka itakapo badalishwa.

Maana yake yy yuko tayari kukandamiza haki za watanzania kwa kutumia SHERIA kandamizi.

Nafikiri angekuwa Rais angekuwa kanyonga wabongo kadhaa maana sheria in mruhusu! Namshauri pinda kuwa ameshavuka level ya chama ni NATIONAL FIGURE think beyond CCM brother!
 
Pasco mimi sikukiona, ila sishangai, mimi ni mwanachama haswa wa CCM, na hili ndilo tatizo kubwa la hawa viongozi wa "Serikali" wanaoingia madarakani kwa tiketi ya CCM, na CCM inaonekana kituko kwa tabia hii sijui kama wanasoma alama za nyakati.

Watu ni waelewa kupita maelezo, na hasa kundi hili kubwa mno la vijana wanaoelimishwa na darasa la ulimwengu kupitia media ambayo kila mtu anai-access.Kauli hizo zilifaa kipindi kile tunaingia kwenye vyama vingi.

Kutoa agizo la kuhakikisha wanashinda bila kutoa muongozo na kusisitiza misingi itakayowafanya washinde itapelekea muendelezo wa mbinu chafu za kijinga zinazokiletea chama aibu kila siku.

Hawa wanatugawa sijui kama wanajitambua, kwakuwa wanadhani wao ni CCM na wengine si wao wakati madaraka waliyonayo yanapaswa kuwa ya kuwatumikia watu wote bila ubaguzi wowote na hata kauli zao zisimame katka misingi hiyo.

Kauli kama hiyo alitakiwa atoe katibu Wilson au Nape kwa wadhifa wake. Mnakitia doa chama, na ndiyo mnakipeleka pabaya, hebu rejeeni misingi ya CCM mwanzo kabisa mwa katiba, yaani hiyo peke yake mkiihubiri, kwa vitendo, ni vigumu chama kingine kuwayumbisha. Mh Pinda, please!

JAMANI! Nilikua siamini sana mambo ya kishirikina siku nyingi, ila kwa hili la baba yetu PM naanza kupata wasiwasi labda amefanyiziwa. Mbona kila akiongea ni.... mh anajiharibia kishenzi. Matamko yake kila mtu anayashangaa, ina maana hajitambui au ndio kafanywa aonekano hamnazo! Napenda kusema tu haiwezekani kwa nafasi, elimu, exposure alizonazo eti awe vile. Basi maombi nayo yatusaidie hapo
 
Pasco CCM is everything in the ruleship! Hao wote ni wateule wa mwenyekiti wa chama na alegiance ipo kicham$a zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Pasco unanishangaza kidogo. Baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa ni WABUNGE kwa tiketi ya CCM. Hili tu lingetosha kukuelewesha kwa nini ni lazima wafanye kila lililo ndani ya uwezo wao kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Mkuu wa wilaya aliyesababisha Mh Wenje kulalamika Bungeni ni Baraka Konisaga, aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Kinondoni kabla hajaukwaa U-DC enzi za Mkapa. Huyu jamaa kwa tabia na hulka yake humwambii kitu kuhusu CCM.
 
Narudia kutoa maoni ambayo niliwahi kuyatoa, Waziri mkuu huyu wa ccm asiulizwe haya maswali ya ghafla, hana uwezo wa kufikiri haraka na kutoa majibu. Sasa mnaona, siku nyingine atakuja kusema na kuidhinisha kitu cha hatari kabisa na mtashindwa la kufanya. Mchelea mwana kulia, hulia yeye.
 
Narudia kutoa maoni ambayo niliwahi kuyatoa, Waziri mkuu huyu wa ccm asiulizwe haya maswali ya ghafla, hana uwezo wa kufikiri haraka na kutoa majibu. Sasa mnaona, siku nyingine atakuja kusema na kuidhinisha kitu cha hatari kabisa na mtashindwa la kufanya. Mchelea mwana kulia, hulia yeye.
Kama kuna siku Pinda aliongea ukweli ni namna alivyomjibu Mh Wenje jana. Alisema DC, RC, Waziri, Waziri Mkuu wote ni wanaCCM, watasimamia ILANI ya chama chao piga ua ili waendelee kuwa madarakani. Huu ni ukweli ulio wazi sana tu.
 
Tuelewe kuwa ndani ya katiba ya ccm wakuu wa wilaya ni lazima wawe ni makada wa ccm. Hakuna mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya anayeteuliwa bila kuwa kada wa ccm. Na wote wanaingia katika vikao vya ccm vya mkoa na wilaya. Swali aliloulizwa Pinda lilikuwa ni mtego na Mbowe alifanya hivyo ili kuwaelimisha Watanzania yakuwa ccm inatumia vibaya madaraka na uchumi wa nchi, kwa kuendelea kuwatumia wakuu wa mikoa na wilaya kwa manufaa ya chama badala ya Taifa.Sisi wananchi ndio tunaotakiwa kusema hapana itakapofika wakati ya kuchangia maoni juua ya mabadiliko ya katiba. NAjua itakuwa vigumu kwa tume hii ya mabadiliko ya katiba kuweza kuleta mabadiliko ya kweli. I do not believe if there will be a new and fair constitution under ccm goverment.
Mabadiliko yakweli yataletwa na watanzania wenyewe tusitegemee vyama vya upinzani kutuletea mabadiliko. Tumepata elimu yakutosha kutoka kwa chama mbadala (CHADEMA). Sasa ni wakati wa watanzania wapenda maendeleo na mabadiliko kufanya maamuzi.
 
umenena kaka.kwa mfumo tulio nao ktk ukusanyaj wa maon ya katba mpya iko wap legitimate expectation kwa watz kuwa katba itatokana na maon ya wananch?inawezekaje kwa mfumo huu chama kingine kuongoza dola?majb yatapatkana kwenye katba ijayo ambayo nayo wananch wamekosa iman na mchakato unaotumika kukusanya maon.totally am dissappointed kwan tunaelekea kuwa km kenya 2015!
 
Pinda alitumia mfano wa kawaida ili kila mtu aelewe! Yani kama RC au DC akifanya kazi vizuri sifa na imani ya wananchi inaenda kwa serikali husika na chama husika,kwa kua Chama chenye serikali ni CCM hivyo kufanya kazi vizuri kwa RC au DC kunaifanya CCM iendelee madarakani,Pinda yupo sahihi na Ukweli ndio huo!
 
sioni cha kumlaum Pinda ikiwa alichosema ni kweli tupu. Tatizo tumezoea kudanganywa Pinda naye kachoka kudanganya ndio maana kaamua kusema kweli,japo kwetu kweli yake imekua chungu.! Nafikiri ni muda muafaka kwa wakuu wa mikoa na wilaya wawe makada rasmi ambapo mashangingi yao yawe na bendera za vyama na sio ya taifa tena.!
 
Ndiyo maana wameanzisha wilaya na mikoa mipya isiyohitajika kwa sasa na kwa gharama kubwa za kodi zetu ili watutawale milele.i'm very dissappointed too.
 
The party is supreme hangovers zinamsumbua huyu. Hajui enzi hizo zishapitwa na wakati. Time and tide waits for no man. Tsunami la mabadiliko/change litasafisha hadi ikulu.
 
Pasco
Wanafanya kazi kwa kutekeleza ilani na sera za CCM pamoja na kwamba ni kauli tata bado ina ukweli ndani yake, serikali iliyopo mdarakani ni CCM. Mkuu haya ya wakuu wa wilaya si ya ajabu hata kwenye nchi yenye demokrasia kama Marekani majaji wa chombo kikubwa cha sheria Marekani -US SUPREME COURT upigaji wao wa kura unategemea zaidi jaji alichaguliwa na raisi wa chama gani; wao hawaangalii makunyanzi hivi unafikiri kama majaji wa Supreme Court wangekuwa hawapigi kura kisiasa unafikiri George Bush angekuwa raisi?


Chama
Gongo la mboto DSM- in vacation Puerto Vallarta

Hakuna kitu, ni siasa uchwara tulizorithi kutoka mfumo kandamizi wa chama kimoja, katiba mpya italiweka hili sawa. Mkuu wa wilaya na upendeleo wa kichama wapi na wapi?! ni kituko, wakuu wa mikoa na wilaya kuwa serikali kuu kwangu mimi ni tatizo pia. Chama unatetea upuuzi kwa hoja nyembamba za kimarekani
 
juzi tu kwenye semina ya wakuu wa wilaya na mkoa jk alisema hivi '' ninyi wakuu wa wilaya na miko ni wafanya kazi wa serikali fanyeni kazi na acheni kufanya siasa'' wakati anasema hayo pinda nae alikuwa yupo ....leo hii pinda anaropoka kivyake....

Mkuu binafsi nimehuzunika sana lkn truely nawachukia sana ma RC na DC hawana maana kabisa ona hata juzi kati RC Iringa anadiriki hata kuingilia uchaguzi wa serikali wa wanachuo-RUCO? natumaini CDM wameinukuu kauli/jibu hilo vzuri sana wakawaambie wananchi waelewe role ya RC na DC'c walivo mumiani wa kodi zao
 
Back
Top Bottom