PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

juzi tu kwenye semina ya wakuu wa wilaya na mkoa jk alisema hivi '' ninyi wakuu wa wilaya na miko ni wafanya kazi wa serikali fanyeni kazi na acheni kufanya siasa'' wakati anasema hayo pinda nae alikuwa yupo ....leo hii pinda anaropoka kivyake....
 
Hivi hawa ma RC na DC si ndio Anna Kilalgo aliwatetea kuwa wawemo katika uratibu wa katiba mpya? Fikiria sasa ni upendeleo kiasi gani kwa CCM watakao uonyesha! Vyeo hivi vifutwe kabisa ndani ya katiba
bullet nimesikia katika taarifa ya habari kuwa Mh jaji Walioba kawapiga marufuku RC Na DC kuhudhuria vikao vya maoni ya katiba inawezekana walishaanza kutumia uwezo wao wakuhakikisha ccm inatawala milele
 
Last edited by a moderator:
Kwa kauli ya Pinda ina maana kwamba kuanzia usalama wa taifa, polisi, jeshi, mahakama vipo kuhukikisha ccm inatawala milele huku wakitumia pesa ya watanzania?, huo ni upumbavu uliopita kiasi.

inamaana hata wakurugenzi wa wilaya pia ni makada na ndiyo maana wanahusika moja kwa moja kwenye chaguzi mbalimbali ili kutetea chama.kazi ipo
 
Watanzania walikua na matumaini sana na PINDA,WAKAT AKIAPISHWA,LAKIN WADAU ME NAWAAMBIA HAKUNA MTU WA KUITOA TANZANIA HAPA TULIPO,REJEA MWAKA 2005 WATU WALIKUA NA HOPE SANA NA JK,TENA MATUMAIN MAKUBWA MNO,LEO ANASEMA MAISHA BORA HAYAJI BILA KUFANYA KAZI,,,,JE WATANZANIA HAWAFANYI KAZI????KODI INALIPWA NA NAN????
 
juzi tu kwenye semina ya wakuu wa wilaya na mkoa jk alisema hivi '' ninyi wakuu wa wilaya na miko ni wafanya kazi wa serikali fanyeni kazi na acheni kufanya siasa'' wakati anasema hayo pinda nae alikuwa yupo ....leo hii pinda anaropoka kivyake....

wewe unakumbuka,yeye hakumbuki........
 
Pinda kachemsha, nasubiria kauli toka CDM, CUF, NCCR, LHRC, wanaharakati. So pathetic
 
Pinda kachemsha, nasubiria kauli toka CDM, CUF, NCCR, LHRC, wanaharakati. So pathetic. Upuuzi huu. Wanahabari wamuhoji mama Anna Kilango a.k.a mama Willy@kumkoma nyani, kuhusu kuwatetea ma RC na DC katika uandaaji wa katiba na kauli ya kilaza Pindwa
 
kwa hili Pinda umekuwa rafiki yangu sana maana umekuwa ukiongea ukweli japo sitausupport ukweli wako na kauli zako nyinginezo kama Zanzibar si nchi, atakae tuhumiwa kumkata albino nae auwawe palepale, liwalo na liwe.

Unafaa sana kuwa raia wa kawaida lakin uongozi mkubwa wa uwaziri Mkuu sio hadhi yako maana u r not critical thinker that much.
 
nakuongezea mkuu Pasco
1.wakuu wa shule wote.
2.walimu wakuu wote.
3.wakurugenzi wote.
4.ma afsa utumishi wote na wakurugenzi
5.wafanyabiashara wote wakubwa
6.jeshi la polisi.. Etc etc

Pinda alisahau hao. Wote hao huakikisha CCM inaendelea tawala.
Tuna kazi nzito.
 
Pinda ametuthibitishia kuwa nchi yetu ina tatizo.

DC/RC wana mamlaka juu ya mahakimu wa wilaya mikoa kwa mujibu sheria iliyotungwa mwaka jana iliyolalamikiwa sana na Lissu
DC/RC ni wenyevitii wa kamati ya ulinzi na usalama inayompa mamlaka ya kuagiza polisi kufanya jambo lolote ikiwepo kumkamata mtu ye yote.
DC/RC ni msemaji wa mwisho wilayani hata msimamizi wa uchaguzi wa wilayani (mkurugenzi) yuko chini yake. Japo wana majukumu tofauti. je, haki itatendeka?
Sasa mkanganyiko huu + kauli ya Pinda unapata nini kama siyo vurugu.
 
Pasco,

Nadhani hujamuelewa.

Yeye alimaanisha hao ma DC na RC wanatakiwa wafanye kazi yao vizuri ili CCM ikipita kwenye kampeni 2015 iwe na cha kujivunia huko mikoani an wilayani. Wapate tambo za kusema, angalia pale tumefanya sisi na hiki na kile.
 
Pasco mimi sikukiona, ila sishangai, mimi ni mwanachama haswa wa CCM, na hili ndilo tatizo kubwa la hawa viongozi wa "Serikali" wanaoingia madarakani kwa tiketi ya CCM, na CCM inaonekana kituko kwa tabia hii sijui kama wanasoma alama za nyakati.

Watu ni waelewa kupita maelezo, na hasa kundi hili kubwa mno la vijana wanaoelimishwa na darasa la ulimwengu kupitia media ambayo kila mtu anai-access.Kauli hizo zilifaa kipindi kile tunaingia kwenye vyama vingi.

Kutoa agizo la kuhakikisha wanashinda bila kutoa muongozo na kusisitiza misingi itakayowafanya washinde itapelekea muendelezo wa mbinu chafu za kijinga zinazokiletea chama aibu kila siku.

Hawa wanatugawa sijui kama wanajitambua, kwakuwa wanadhani wao ni CCM na wengine si wao wakati madaraka waliyonayo yanapaswa kuwa ya kuwatumikia watu wote bila ubaguzi wowote na hata kauli zao zisimame katka misingi hiyo.

Kauli kama hiyo alitakiwa atoe katibu Wilson au Nape kwa wadhifa wake. Mnakitia doa chama, na ndiyo mnakipeleka pabaya, hebu rejeeni misingi ya CCM mwanzo kabisa mwa katiba, yaani hiyo peke yake mkiihubiri, kwa vitendo, ni vigumu chama kingine kuwayumbisha. Mh Pinda, please!

Mbinu wanazowafundisha ni kama Hizo za Kunyang'anya funguo za hotel Wateja wenye Mrengo Mwingine!! Ni bora wangewapa na Hadidu za rejea namna ya KUwatetea ili waendelee kuwa madarakani na sio Huo Ubabe!!
 
Pinda, hapindishi jamani, anafurahisha sana akiamua kuweka propaganda pembeni ili japo wasiojua serikali nini inafanya kiuhalisia nao wapate mwanga wa kinachoendelea ndani ya system.
 
Pinda ametuthibitishia kuwa nchi yetu ina tatizo.

DC/RC wana mamlaka juu ya mahakimu wa wilaya mikoa kwa mujibu sheria iliyotungwa mwaka jana iliyolalamikiwa sana na Lissu
DC/RC ni wenyevitii wa kamati ya ulinzi na usalama inayompa mamlaka ya kuagiza polisi kufanya jambo lolote ikiwepo kumkamata mtu ye yote.
DC/RC ni msemaji wa mwisho wilayani hata msimamizi wa uchaguzi wa wilayani (mkurugenzi) yuko chini yake. Japo wana majukumu tofauti. je, haki itatendeka?
Sasa mkanganyiko huu + kauli ya Pinda unapata nini kama siyo vurugu.

Sio Kumkamata Mtu yeyote; Hata Kuua!!
 
bullet nimesikia katika taarifa ya habari kuwa Mh jaji Walioba kawapiga marufuku RC Na DC kuhudhuria vikao vya maoni ya katiba inawezekana walishaanza kutumia uwezo wao wakuhakikisha ccm inatawala milele

Dah basi kafanya jambo la busara kweli maana jamaa wao wangetaka kuwatazama watu machoni.
 
Back
Top Bottom