PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,570
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, sipendi kabisa kukosa kipindi cha Maswali na Majibu ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu Bungeni, ambapo Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo, Kayanza, Peter Pinda, hujibu maswali ya papo kwa papo, ile leo nilikikosa kipindi hiki.

Lakini kupitia taarifa za habari, nimemsikia Mhe. Pinda, akisema kuwa ni jukumu la wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili CCM iendelee kutawala milele!.

Naombeni wajuzi wa masuala ya utawala, mnirekebishe if I'm wrong!, kuanzia kwa rais JK na wanasiasa wengine wote ambao japo wamechaguliwa kwa tiketi tuu za vyama vyao vya siasa, lakini walio wachagua sio wanachama wa vyama vyao tuu, bali wamechaguliwa na umma wa Watanzania wote kwa ujumla wetu, rais, mbunge, diwani au wenyeviti wa mitaa, ukiishaguliwa, japo unabaki kuwa mwanachama wa chama chako lakini unageuka ni mtumishi wa umma, paid by taxpayers money, jukumu lako kuu sasa ni kuutumikia umma ambao chama chako ni sehemu ya umma huo na sio kukitumikia chama chako!.

Hii inamaanisha rais JK, japo ameshinda kwa tiketi ya CCM, kuongoza serikali ya JMT, kwa kutumia ilani ya uchaguzi ya CCM, ambapo kwa wakati huo huo yeye ndiye Mwenyekiti wa CCM, hakuchaguliwa na wana CCM pekee, amechaguliwa na Watanzania wote kwa ujumla wetu kuiongoza Tanzania na Watanzania na sio amechaguliwa na wana CCM, kuongoza serikali ya CCM kwa ajili ya wana CCM pekee!, hapana!, JK na serikali yake, japo ni CCM, lakini amechaguliwa kuongoza serikali ya Tanzania kwa niaba ya Watanzania wote na kwa manufaa ya Watanzania wote, wakiwemo watu wa vyama vingine vyote vilivyopo kisheria kwa mujibu wa katiba na sio kwa manufaa ya wana CCM!. (Of the people, by the people and for the people), hivyo hili la viongozi wa umma kutakiwa kuhakikisha CCM inatawala milele, kusema ukweli, mimi linanitatiza!.


JK ndiye rais wa Chadema, ndiye rais wa CUF na ndiye rais wa wote wenye vyama na wasio na vyama. Yeye ndiye rais wa Dr. Slaa, yeye ndiye rais wa Prof. Lipumba, yeye ndiye rais wetu sisi wote kama Watanzania, ni rais wa waliomchagua na pia rais wa wasiomchagua, anatakiwa kufanya kazi kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa kwanza na sio maslahi ya chama chake cha CCM!.

Kauli ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda bungeni leo kuwa Wakuu wa wilaya na mikoa, wako pale kuhakikisha CCM inashinda chaguzi zote ili itawale milele, haiwezi kupita bila kupingwa!. Hi inamaanisha kuwa viongozi hawa, wako kwa ajili ya kuilinda na kuitetea status quo ya CCM ili iendelee kutawala milele!. Kwa maoni yangu, this is very wrong kwa tafsiri sahihi ya Public Servants!. Kwa kauli hii ya Pinda, it goes without saying kuwa wakuu wa majeshi yetu, Polisi wetu, mahakama zetu na wakuu na vyombo vya dola, na vyombo vya kiserikali, wanateuliwa ili wahakikishe CCM haishindwi na inaendelea kutawala milele!.

Public Servant, ni mtumishi wa umma, ma RC na ma DC ni viongozi wa serikali, kwa maana hiyo ni viongozi wa umma, na watatimiza majukumu yao kwa maslahi ya umma na sio kwa maslahi ya CCM. Ndio maana Mhe. Tundu lissu aliwakataa hawa wasihusishwe ile tume ya katiba na juzi akasisitizwa hawapaswi kuwamo bungeni!.

Hata wabunge wa kuchaguliwa, ni watumishi wa umma, japo wanateuliwa kwa tiketi za vyama vya siasa, wanachaguliwa na wananchi na sio na vyama vyao, hivyo wakishashinda ubunge, wanakuwa ni watumishi wa watu na sio watumishi wa vyama vyao, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao ya kibunge kwa maslahi ya wananchi na sio kwa maslahi ya vyama vyao!. Kama ni kweli, majukumu ya ma RC na ma DC ni kuhakikisha CCM haishindwi, hii ina maana kubwa zaidi katika mustakabali wa mabadiliko halali ya serikali!.

Binafsi yangu, nimesikitishwa na kauli hiyo, and to be honest, nilikuwa na very high hopes kuhusu Pinda, kuelekea 2015! lakini sasa nimeamini Pinda pia ni wale wale!. Kwa vile CCM ni chama tawala, hivyo public servants wana jukumu la kuhakikisha CCM inashinda na kutawala milele!.

Hii inamaanisha hata kama 2015, Watanzania wataamua kuivote out CCM kupitia njia halali ya ballot box, hao public servants wenye jukumu la kuitumikia serikali mpya ya chama kitakachoshinda, tayari wako kwenye mind set ya chama kimoja kuhakikisha lazima CCM inashinda!, na jee ikitokea CCM ikashindwa kweli, jee watakabidhi madaraka kwa mshindi halali?!, jee majukumu yao yatabadilika or what does Pinda exactly meant?!.

Hii maana yake, hata ikitokea wapinzani wakashinda kwenye ballot box, lakini ushindi wa jumla ni CCM!.

Kusema ukweli, civic education kuhusu multipartism Tanzania, inatakiwa kuanzia juu ndipo ishuke chini kwa wananchi wa kawaida!.

Sasa ndio nimeanza kuelewa, no wonder kwa nini jina la Pinda, halitajwi kabisa kabisa katika presidential materials!. Maliza tuu term yako kwa amani, ukaiendeleza ile kampuni yako ya P & P, nami nitakutangazia sana ile asali yako, ila nakuomba Tanzania yetu utuachie kwa amani, hii sio Tanzania ya CCM, CHADEMA au CUF!. Tanzania ni ya Watanzania wote!.

Kiukweli, mabadiliko yakija, hizi nafasi za ma DC na ma RC ndizo ziwe za kwanza kufutiliwa mbali!.

I'm Very Disapointed!.

Paskali.

NB. Paskali ni Mtanzania mzalendo, Mwandishi wa habari wa kujitegemea ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa, lakini sio mfuasi au mshabiki wa chama chochote cha siasa!. Ni mkereketwa wa maendeleo, mzalendo kwa kutanguliza mbele Utanzania kwa maslahi ya Taifa.
 
Huyu mzee sijui hata kwa nini alipewaa uwaziri maana saa zingine namuona kama hajui nini anafanya maana mambo yake tu anaoneken mfata upepo kutoka mjengoni....
 
Pasco kakangu,

Unajua fika kuwa watumishi wengi serikalini wanafanyishwa kazi kwa mtindo huu.

Kwangu sishangai, na bado tunajigamba tuna demokrasia. Kauli hii wengi mliitarajia toka kwa Nape au Mukama, sasa ndio mjue tuna ombwe la uongozi kama taifa.
 
Last edited by a moderator:
Tulisema hapa tangu anaapishwa, kwamba huyu jamaa bomu, watu wakaona tunaendekeza tahariri.

Sasa mnaona.

Na zaidi ya Pinda, tatizo ni system iliyomlea Pinda, maana huyu ni graduate wa UDSM aliyefanya kazi Usalama miaka mingi, akakaa kwenye corridors of power Ikulu huko, akagombea ubunge akapata, akapewa u PM.

Sasa inaonekana institutions zetu zote hizi hazijaweza kumuandaa vizuri kwa kazi hii.

Kuanzia elimu ya chini mpaka ya juu shahada ya sheria, usalama, Ikulu, bungeni, uwaziri, mpaka uzoefu wa miaka yote hiyo aliyokuwa PM, bado anacheza makidamakida mpaka leo.

Pathetic.
 
Kwa maana hiyo wakuu wa mikoa na wilaya wanatumikia chama cha siasa (CCM). Mashangingi, mishahara na posho zao zinatoka kwenye CCM au hazina?

NB: From now on, wakuu wa mikoa na wilaya ni fair game, si viongozi wa serikali tena bali ni makada wa chama cha siasa. Hivyo, wananchi wana haki ya kuwasikiliza/kuwapuuza kama wanavyofanya kwa wana-CCM wengine i.e Nape & co. Naona giza!
 
CCM wana viongozi aina kadhaa wa kadhaa

1,kuna wezi ambao ni wachapakazi kidogo

2.wezi wazembe

3.wachapakazi but uwezo mdogo


sasa Pinda ndo group la mwisho
na wanaonekana better kulinganisha na wengine
 
Mkuu Pasco
Mh Pinda yuko sahihi kwa mfumo wa nchi yetu maana tumerithi ule wa chama kimoja.
Ukiangalia kwa ukaribu, RC na DC ni baadhi ya wajumbe wakuu wa CCM kwenye maeneo yao ya kazi. lakini huwezi kuona wanakuwa wajumbe wa vikao vya opposition parties.
Na hii ndo kazi yao kubwa honestly. Ameongea ukweli japo ni mchungu but in reality kama uko mikoani, utaona ndo ukweli.

RC na DC hawatakiwi tena kwenye katiba mpya. Tunahitaji RAS na DAS na DED tu. Ukiingia kwa undani, hata DAS hana kazi ya muhimu.

Pinda amewafungua masikio watu wengi na itasaidia kwenye maoni ya katiba watu kulijadili jambo hili.

pole for being dissapointed Pasco, ila huo ndo ukweli. kama huamini toka da uje uishi kwenye mikoa mingine. Utauona huu upuuzi kwa uwazi kabisa
 
FJM,

Wapinzani wanatakiwa ku-capitalize katika hili. Hutuhitaji wakuu wa Mikoa/Wilaya. Binafsi sioni umuhimu wa watu hawa zaidi ya kuliingiza taiga ktk gharama zisizo na kichwa wala miguu.
 
Last edited by a moderator:
Pasco, mkuu wangu hivi kweli wewe ulitegemea vinginevyo? Si afadhali huyu mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda kaweka wazi mjue kabisa kwamba mfumo uliopo ndio umetufikisha hapa tulipo na ndivyo itakavyokuwa hivyo jiandaeni..

Mh. Pinda anaweza kabisa kusema uongo wowote kuwapaka mafuta, lakini ukweli unabakia kuwa kipenzi cha Mungu. Pinda kasema wazi nini wanakitaka hivyo ni kujumu la vyama vya upinzani kuzipata salaam hizo. Politically anaweza kuwa wrong lakini ndivyo inavyokuwa..Tujifunze mara ngapi mkuu wangu.
 
Wapinzani wanatakiwa ku-capitalize katika hili. Hutuhitaji wakuu wa Mikoa/Wilaya. Binafsi sioni umuhimu wa watu hawa zaidi ya kuliingiza taiga ktk gharama zisizo na kichwa wala miguu.

Sidhani kama PM anaelewa madhara ya hiyo kauli yake kwa CCM. Kwa bahati mbaya sana, viongozi wengi serikalini na hata ndani ya ccm wako nyuma sana. Sintofahamu inayoondelea ni kwa sababu wananchi wamepiga hatua lakini wakubwa wanazidi kucheza zilipendwa. Viongozi wanaonekana kufanya mambo ya aibu sana na unaposikia kauli kama hii ya Pinda you have to ask yourself kama alikuwa holiday sayari nyingine ambayo hakupata mawasaliano toka Tanzania au the 'dear leader' is simply out of it?
 
Mh Pinda yuko sahihi kwa mfumo wa nchi yetu maana tumerithi ule wa chama kimoja.
Ukiangalia kwa ukaribu, RC na DC ni baadhi ya wajumbe wakuu wa CCM kwenye maeneo yao ya kazi. lakini huwezi kuona wanakuwa wajumbe wa vikao vya opposition parties.
Na hii ndo kazi yao kubwa honestly. Ameongea ukweli japo ni mchungu but in reality kama uko mikoani, utaona ndo ukweli.

RC na DC hawatakiwi tena kwenye katiba mpya. Tunahitaji RAS na DAS na DED tu. Ukiingia kwa undani, hata DAS hana kazi ya muhimu.

Pinda amewafungua masikio watu wengi na itasaidia kwenye maoni ya katiba watu kulijadili jambo hili.


Bitabo, hapa ndipo watu wanaona dhulma na matumizi mabaya ya kodi za walalahoi. Kwa miaka yote ishirini tangu mfumo wa vyama vingi viingie, tumeendelea kugharamia makada wa propaganda. Sasa hivi tuna wakuu wa wilaya 130 na ushee, wakuu wa mikoa 27 hapo kila mtu ana shangingi, anapata allowance kila kukicha. Tunapata faida gani?

Huu uvundo ni wa kusafisha kwenye hii katiba mpya, but for now they should be treated kama makada wengine wa CCM!
 
Kwa kauli ya Pinda ina maana kwamba kuanzia usalama wa taifa, polisi, jeshi, mahakama vipo kuhukikisha ccm inatawala milele huku wakitumia pesa ya watanzania?, huo ni upumbavu uliopita kiasi.
 
Pasco, mkuu wangu hivi kweli wewe ulitegemea vinginevyo? Si afadhali huyu mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda kaweka wazi mjue kabisa kwamba mfumo uliopo ndio umetufikisha hapa tulipo na ndivyo itakavyokuwa hivyo jiandaeni..

Mh. Pinda anaweza kabisa kusema uongo wowote kuwapaka mafuta, lakini ukweli unabakia kuwa kipenzi cha Mungu. Pinda kasema wazi nini wanakitaka hivyo ni kujumu la vyama vya upinzani kuzipata salaam hizo. Politically anaweza kuwa wrong lakini ndivyo inavyokuwa..Tujifunze mara ngapi mkuu wangu.
Kiongozi Mkandara,
Unafahamu hata yule Jemadari Jacki Zoka anahudhuria vikao vya juu vya CCM? Unaiona hatari ya kuwa kama alivyosema Mkuu Pasco kuwa wenye Nchi siku wakiamua kuipiga chini CCM, basi uwezekano ni mkubwa yakawa yale ya Kibaki na Wakenya,2008. Safari ni ndefu bado.
 
Nishaona dalili za kupasuana hapa! Kama wakuu wa mikoa na wilaya watapewa nafasi ya kupiga kampeni huku wengine wananyimwa vibali vya kukusanyika itakuwa ni sababu tosha ya amani kuanza kutoweka! Am worried
 
Watu husema, ukitaka kumuua mwendawazimu (unaweza kumuita silly, mzembe, dhaifu), usinyanyue mkono wako bali mpe kitanzi atajimaliza mwenyewe. Kamanda Lissu amempa kitanzi Pinda amejimaliza mwenyewe, ni suala la muda tu.

Kwa kauli hiyo, ni kuwa zile ahadi zaviongozi wetu kuwa "nitawatumikia Watanzania bila ubaguzi" inakuwa ni uongo ndani ya kiapo kitakatifu. Ikiwa wakuu wa wilaya na mikoa, jeshi, polisi, mahakama (wote kama watumishi wa umma) wapo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa CCM inashinda Liwalo naliwe, na mbaya zaidi wapo hapo walipo kwa mishahara na marupurupu ya jasho la Watanzania, hii ni dhuluma na wizi wa mchana. Nani atakayekuwa na imani tena na watumishi wa umma, akiwemo yeye Pinda? IKO HAJA YA KUREJESHA KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU HUYU.

Ninachosema, kwa ithibati ya maneno ya Pinda (anayepindisha haki ya Watanzania kuwa dhuluma kwa Watanzania), CCM imezidi kukosa uhalali wa kuiongoza Tanzania.
 
Nishaona dalili za kupasuana hapa! Kama wakuu wa mikoa na wilaya watapewa nafasi ya kupiga kampeni huku wengine wananyimwa vibali vya kukusanyika itakuwa ni sababu tosha ya amani kuanza kutoweka! Am worried

Hivi hawa ma RC na DC si ndio Anna Kilalgo aliwatetea kuwa wawemo katika uratibu wa katiba mpya? Fikiria sasa ni upendeleo kiasi gani kwa CCM watakao uonyesha! Vyeo hivi vifutwe kabisa ndani ya katiba
 
Mkuu Pasco you have a point. Mimi mchango wangu ni mfupi tu. Vipi kuhusu ukweli kwamba makamanda wa JWTZ nao huteuliwa kuwa ma-RC na DC? Kumbe jeshi pia hutumika kisiasa?
 
Back
Top Bottom