Mbowe kijana wa CCM kwa kivuli cha upinzani

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
CCM kama chama dola nchini Tanzania kimefanikiwa sana kujitengenezea upinzani wake na wapinzani wake ambao kwa uhalisia nao ni Ccm nje ya Ccm. Mmoja wao ni Mbowe na chama chake cha Chadema.

Historia inatuambia, waanzilishi wote wa Chadema walikuwa Benki kuu. Yaani Mtei, Bob Makani na Mbowe na walitolewa kwa sababu maalum kutengeneza chama cha upinzani ili Tanzania itambulike na dunia kama imeruhusu mfumo wa vyama vingi na demokrasia.

Tangu Chadema iasisiwe, hatujashuhudia kiongozi tofauti ya hao watatu waliotoka BOT kwa shughuli maalim kuulaghai umma wa kimataifa juu ya uwepo wa vyama vingi na demokrasia Tanzania.

Baada ya Chadema kuasisiwa, wakaja wanachama wengi ambao hawakuwa sehemu ya mpango huo (Kuilaghai dunia) hawa wakaja kwa nia ya dhati kabisa ya kuiondo Ccm na hapo ndio Mbowe akawa mkali kama pilipili.

Tunaanza na Kaburu, huyu bwana alikuwa mwiba kweli kwa serikali ya Ccm. Mbowe ili kulinda maslahi yake mwaka 2005 alishilikiana na Ccm Bega kwa Bega kuhakikisha Kaburu anashindwa na Serukamba. Kwanza Mbowe hakumpigia kampeni Kaburu, Kaburu hakupewa sapoti na Chama kabisa mpaka alipoangushwa. Na kama zawadi Mbowe akapewa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto kabwe.

Baada ya Kaburu kikaja kizazi cha pili, kizazi cha vijana waliokuwa na uchu wa mabadiliko kweli kweli. Hapa nawazungumzia kina Zitto, kafulila na Machali. Hawa wote walisambalatishwa kama upepo. Ccm ikapumua tena.

2010 mpaka 2015 hakuna mwanamageuzi aliyeonyesha njia kama Dr Slaa, Ccm ilikuwa inaondoka. Mbowe akakumbushwa wajibu wake wa kuilinda Ccm. Akaletewa criminal Lowasa na kumpoteza Dr Slaa ambae angeweza kutunishana misuli na Magufuli. Tukapoteza tena kizembe.

Kumpongeza Mbowe kwa kuiongoza Chadema miaka 20 pasipo kuitoa Ccm ni ujinga, kuimba nyimbo za Mbowe kuwaita wanaompinga wanafiki ni ujinga. Tunatakiwa kumuhoji Mbowe kwanini ndani ya miaka 20 ya uongozi wako hatujaona matokeo zaidi ya kubadilisha bendera na kauli mbiu?

Wanasiasa aina ya Mbowe wapo wengi duniani, upinzani ni sehemu yao ya agizo la kuvilinda vyama tawala na kuhakikisha upinzani wa kweli haupatikani.

Baada ya kuonekana Mama Samia hana Ushawishi Mbowe kaamua kumfanyia kampeni kwa dirisha la upinzani. Kuandamana bila bugudha mama aonekane ni mwana demokrasia, kumsifia majukwaani na kukiri kusaidiwa nae.

Mbowe anatengenezea sana sympathy na Ccm ili aendelee kuaminiwa kama kinara wa upinzani ila kiuhalisia hizo ni niia tuu za ku block upinzani wa kweli kuaminiwa. Wanaoelewa siasa watanielewa.

Kwa leo naweka kalamu chini.
 
Nimehakiki haraka ni kweli chadema ilianzishwa na Mtei alikuwa Gavana BoT makamu wake Wa Chadema alikuwa Bob Makani alikuwa Naibu Gavana BoT na Freeman Mbowe alikuwa pia mfanyakazi BoT kipindi Chao hao na kaoa mtoto wa Mzee Mtei.Mzee Mtei ni Baba Mkwe wa Freeman Mbowe
 
Kama vyama vya upinzani kikiwemo CDM vmetengenezwa kimkakati na CCM kwa ajili ya maslahi yake. Je! Hiyo si ndiyo salama kwake! Sasa kwa nini nguvu kubwa inatumika kupitia mbeleko la vyombo vya dola kukihujumu na kutaka hata kukiua.

Tatizo lako, unaandika tena kwa kuungaunga kile ambacho kimetokea katika misha binafsi na historia ya mfanano wa sehemu walizowahi kuajiriwa viongozi hao watatu. Umekwepa kwa makusidi kuizungumzia historia ya CDM kama taasisi makini ya kisiasa.

Na hili ndilo tatizo lenu kubwa UVCCM, badala ya ku "focus" katika uhalisia wa mambo, mnatafuta stori za vijiweni na kuanza kujiaminisha kuwa ni za kweli, na kisha kujipongeza kwa siifa za uongo, na kuendekeza maisha ya uchawa!
 
Dola ihujumu chama cha siasa sidhani labda useme baadhi ya watu binafsi ndio wanahujumiwa sio wote kwenye chama wala chama chenyewe baadhi tu
 
Yale yale umekuja na ngonjera za bavicha Clam work.

CHADEMA ni sympathy oriented party. Maana yake ili kiendelee kuaminiwa inabidi CCM waonyeshe kinadidimizwa ili watanzania wasione mbadala. Mwisho wa Siku CHADEMA wanavuruga kila kitu ili kupunguza hasira za wananchi.

Hivi hukuwahi kusikia CHADEMA kuuza viti vya ubunge kwa wabunge wa CCM?
 
Dola ihujumu chama cha siasa sidhani labda useme baadhi ya watu binafsi ndio wanahujumiwa sio wote kwenye chama wala chama chenyewe baadhi tu
Hivi unataka kujisahaulisha kuhusu nini ambacho kilitokea kwa makada na viongozi mbalimbali wa CDM ikiwamo hata Mbowe mwenyewe katika utawala wa JPM miaka michache iliyopita!? Watu kuteswa, kutekwa, kujeruhiwa, kuuwawa, kubambikiwa kesi za uongo, mali zao kuhujumiwa, n.k.
 
Ina maana Lissu pia ni muigizaji? Au hawakumfahamisha mchezo mzima? Mbowe ile kukaa ndani siku 200 ilikuwa ni movie? Slaa kukimbilia ughaibuni pia ilikuwa ni movie? Escro, Richmond, Epa kashfa zote hizo za kifisadi zilizoibuliwa na vyama pinzani ilikuwa ni movie? Mh sitaki kuamini..
Hata hivyo hakuna ushuhuda wa kutosha usio tia shaka.
Hizi ni nadharia tu.
 
Nimehakiki haraka ni kweli chadema ilianzishwa na Mtei alikuwa Gavana BoT makamu wake Wa Chadema alikuwa Bob Makani alikuwa Naibu Gavana BoT na Freeman Mbowe alikuwa pia mfanyakazi BoT kipindi Chao hao na kaoa mtoto wa Mzee Mtei.Mzee Mtei ni Baba Mkwe wa Freeman Mbowe
Chadema iliasisiwa na Mzee Tuntemeke Sanga, Mzee Ngaiza, Mzee Mwakitwange, Bob Makani, Mzee Mtei na Mzee Ndesamburo

Mabilionea watupu na lengo lao lilikuwa kumuonyesha Nyerere Siasa za Dunia zinavyoendeshwa
 
Back
Top Bottom