Pinda awasimamisha katibu mkuu wa wizara ya afya na mganga mkuu

Kikwete inabidi afanye Maamuzi ya kuwatimua Waziri na naibu waziri.
 
Pinda hawezi kumsimamisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya.
Kumbuka wakati wa Jairo alivyoliambia Bunge kuwa ajira ya Katibu Mkuu ipo kwenye mamlaka ya Raisi, leo kapata wapi mamlaka hayo?
Angalia CHANGA LA MACHO HILO MADAKTARI.
 
cjui leo nimeamkaje! nimeenda mahala asubuhi kufuatilia ela yangu nkapata na ziada,nkafungua tv nkakutana na bunge linakubali marekebisho yaliyowatoa wanaCdm na ncrr bungeni,nafungua TBC nkaona Pinda kwa niaba ya jk amewatimua dkmkuu na katibu mkuu nyoni ili madaktari wawe na amani ktk magumzo...nadhani leo ni SIKU NJEMA KWANGU...Eeh na uyu mdada aliyenikataa hata hapokei cmu ,sasa naona anabip sasa ivi, mh Mungu ni mwema leo. Ngoja nikamalizie kazi...LEO NI FURAHA KWANGU...jk nisaidie uwatimue na mawazir
 
Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.

Ana mamlaka hayo? au kesha mpigia simu mkuu!
 
Na yeye manfiki alikuwa wapi siku zote? Si alisema anawafukuza Madakari? Mbona hajatekeleza ahadi yake? Na yeye anatakiwa awe fired pia kwani amezikanyaga kauli zake hana lolote.
 
Political-Comedy movie kapata wakumwonea, mbona kwa DJ alilialia {kama kweli} but it will still remain Political Comedy movie sababu tumeona mengi na tutazidi ona mengi kwa huo muda uliobaki.
 
Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.

'amewasimamisha'. changa la macho.


aaah, mambo ya DJ tena tunayasubiri. watu kuaga familia zao wakiwa wameuramba na kufika ofisini na kuanza kusukumiza gari ya Jairo.
 
Pinda hana ubavu wa kumfukuza Katibu mkuu wa Wizara ya afya.
Kauli aliyoitoa Bungeni Dodoma wakati wa sakata la Jairo kuwa mamlaka ya uteuzi na kufukuza/kuachisha anayo Raisi.
Leo hii kapata wapi mamlaka ya Raisi, au anataka kufanya viini macho mpaka waunde tume ya kumsafisha ili astaafu kwa heshima baadaye awe Balozi nchi za nje?
CHANGA LA MACHO WATANZANIA/MADAKTARI
 
hatimaye serikali yakubali,kile ilichokuwa ina kataa!imewasimamisha kazi katibu mkuu na mganga mkuu wa serikali,na kuongeza posho ile ya elfu kumi hadi elfu ishirin.safi sana.source Tbc 1
 
Ilifaa Pinda angejipindisha mgongo na akajiuzuru kwanza. Imekuaje leo amewatumua viongozi ambao siku ile pale karimjee alikua anakula nao sahani moja kuwalaumu madaktari? Hicho ni kigeugeu na kukosa maamuzi.anaetiwa kiini macho ni mwananchi wao wanajuana zao huko!
 
Iweje mtu namba moja anayetakiwa kuachia madaraka awasimamishe wengine?

Ndugu yangu Nitonye,hapa tunaangalia hii ni sinema,nivigumu kuamini kuwa hata sasa Rais yupo kimya,kana kwamba
mtoto wa mkulima ndiye Rais hasa ukizingatia katika kipindi kama hiki ambapo tumepoteza watu wetu wamekufa kwa kukosa huduma mahospitalini,Rais katulia nasikia fununu kaenda nje ya nchi,mimi naungana na maneno ya wana harakati waliyo yasema jana kuwa tusije fikiri kuwa rais yupo Ikulu kumbe alishaondoka siku nyiiiiingi zilizopita.
MAPENDEKEZO YANGU
najua Mtoto wa mkulima hawezi kuwa fukuza kazi hawo,yaani Katibu,Naibu Katibu,Waziri .
.1.Kwa kuwa wa Tanzania wamekufa na uhai wao hauwezi katu rudi,J.K FUKUZA hawo wote ingawaje najua kwako yatakuwa ni maamuzi magumu sana kwako ambayo najua kwako hautaweza kwani wewe ni mtu wa watu usiye penda kukwaruzana na mtu yeyote.
2.Kwakuwa Rais naye ameshindwa kuyatolea maamuzi ya haraka haya matatizo kwa sababu aliwaheshimu walioko nje ya nchi na kwenda kuwasikiliza matakwa yao naomba WaTanzania tumuombe japo tumlipe ROBERT MUGABE,ama KAGAME waje watushikie kiti cha urais japo kwa hiki kipindi kigumu cha miezi sita wakati tunajipanga cha kufanya tukitafuta serikali mbadala.Naomba kuwasilisha
:embarassed2:
 
Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.

Hapo kwenye red sijui mpaka sasa kawatimua wangapi, labda Kama sio Vasco da gama ninaemfahamu
 
Habari toka mkutanoni kati ya waziri mkuu na madaktari zinasema waziri mkuu kawasimamisha kazi katibu mkuu wa wazara ya afya na mganga mkuu huku akimuachia rais kuwatimua waziri na naibu wake.
Chanzo: madaktari walio katika kikao na waziri mkuu.

Kama kamwachia Rais amalizie basi na madaktari wasikubali mpaka na Rais amalizie. Lazima tujifunze utawala shirikishi sio utawala wa kuongozwa kama punda. Utawala wa kupokea maagizo ni mbaya sana na ndio maana viongozi wanajichanganya sana kuongoza. CCM mnasumu mbaya sana kiuongozi, lazima mbadilike. Spika wa Bunge na wabunge wa ccm wameonyesha picha mbaya sana kwa wananchi na tumejua ya kuwa tunakomoana.

Sasa ni kazi kwetu, ni operetion safisha kwa nguvu za wananchi, hata kama ni M/kiti wa kijiji ni kumfuata na mawe tumechoka. Tunaumia kwa ajili ya mtu mmoja wakati sisi ndio tunaoteseka. Tunaomba mungu elimu ya uraia ifunuliwe kwa watanzania wote na tujua haki zetu zilikofichwa na hao mafisadi wa CCM.
 
Back
Top Bottom