BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
UTEUZI: Rais Samia Sululu Hassan, amemteua Dkt. James P. Mataragio, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
Dkt. Mataragio anachukua nafasi ya Athumani Selemani Mbuttuka ambaye Uteuzi wake Umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine
Kabla ya Uteuzi huu, Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Disemba 2014, Dkt. James Mataragio aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPDC
August 2016 alisimamishwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TPDC
Julai 2019 Rais Magufuli Aliagiza arejeshwe kazini
Aprili 4 2021 alitolewa TPDC nafasi ikachukuliwa na Thobias Mwesiga.
Aprili 5 2021 aliteuliwa tena kuwa Mkurugenzi TPDC.
Februari 2023 alitolewa TPDC nafasi yake ikachukuliwa na Mohamed Makame na taarifa ilisema atapangiwa kazi nyingine.
Februari 2024 ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Wizara ya Nishati.